Waholanzi na utamaduni wa baiskeli, sisi tunakimbilia magari binafsi

 Wakati sisi tunashindana kwenda kazini na magari ya bei mbaya, wenzetu wanakuja kazini na baiskeli. Hapa ni Ede, Uholanzi. Baiskeli ndio usafiri maarufu. Jambo hili si la kawaida. Fikiria, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo Kikuu achilia Profesa wake, apande baiskeli kwenda chuoni. Kwa hakika ni jambo unaloweza kuliewa pale Dar es salaam.

Waholanzi wakiwa wamepaki vyombo vyao vya usafiri. Picha:Jielewe

Katika mazingira haya ambapo kila mtu anatafsiri maendeleo kwa kuangalia vitu, na katika mazingira ambayo kila mtu yuko tayari kuonekana naye yupo hata ikibidi kwa mkopo, almuradi aendeshe gari, ni vigumu kupata ufumbuzi wa 'kero' ya kudumu ya foleni jijini Dar es Salaam.  Kila mmoja anafikiri kutatua kero hii kwa kuongeza gari barabarani.
Foleni itoke wapi kwa mazingira haya? Picha: Jielewe



Kituo cha elimu MDF, Ede, Uholanzi. Picha: Jielewe

Hebu fikiri kama watu wangeamua kutumia usafiri wa umma, huu huu uliopo, magari mangapi yangeondoka barabarani? Saa nyingine, inachekesha. Magari 40 yanayohangaika kupenya kwenye mataa ya Ubungo yanaweza kuwa yamebeba abiria kati ya 40-42! Kila gari, mtu mmoja! Hivi hao wote akiamua kupanda baiskeli au kutumia usafiri wa umma, foleni itaendelea kuwa hivi?

Matatizo mengine ni mtazamo tu. Maendeleo ni zaidi ya kumiliki gari. Nimejifunza.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia