Uislamu ulianza lini?

YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi.


Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia.

Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana.

Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye aliyekuwa Mwislamu wa kwanza. Kwa mfano, ukisoma Sura. 6: 163 anasema yeye ndiye wa kwanza kwa Waislamu hii ikiwa na maana kwamba yeye ndiye mwanzilishi wa Uislamu na kwamba Uislamu haukuwapo kabla yake.

Lakini katika maeneo mengine, Qur’an inadai kuwa Musa ndiye Mwislamu wa kwanza. Soma Sura 7:143. Sasa Mussa inajulikana kabisa ndiye mhusika mkuu wa dini ya Uyuda.

Kwa mshangao mkubwa zaidi, mahali pengine inadaiwa kwamba Adam, Abraham na Yesu wote walikuwa waislamu!

Hili, kwa hakika ni jambo la ajabu sana. Unapodai Yesu alikuwa Mwislamu, wakati mafundisho yake yanapingana pakubwa na Uislamu, huo ni ushahidi wa mkanganyiko ambao kwa hakika yeyote anapaswa kuuona bayana.

Kwa maoni yangu, dini hii yaweza kudai kuanza tangu kuumbwa kwa Ulimwengu ili tu kuonyesha kwamba yenyewe ndiyo ya kweli kuliko nyinginezo.

Ukweli uko wazi kwenye Qur’an yenyewe (hata kama inajichanganya) kwamba Muhammad ndiye alikuwa mwanzo wa Uislamu ndio maana anaitwa 'mtume' yaani mleta Uislam.

Sasa sisemi Uislam ni Dini potofu. Hiyo sio kazi yangu. Lakini sikubaliani na wanaodai kwamba Uislamu ulianza tangu enzi za Adam. Ndivyo ilivyo pia kwa Ukristo, dini nyingine yenye asili yake kule kule Mashariki ya kati.

Mambo mengine ni muhimu kuyaelewa hata kama yanaonekana kuwa kinyume na ‘ukweli’ wa kidini. Ikiwa unadhani kwa kujadili haya maana yake ni chuki kwa Uislamu, basi unahitaji kujielewa sasa hivi. Maana ni wazi umejitia kifungo cha hiari.

Itaendelea...

Maoni

  1. Ni mambo ambayo watu hawataki kabisa kuambiwa. Lakini hakuna haja ya kukikumbatia kitu na kukataa kuambiwa ukweli.
    Nakushukuru kaka Bwaya kwa kuweka mambo wazi.

    JibuFuta
  2. Mie nasoma na natoa maoni.
    Nasubiri pia kusoma maoni

    JibuFuta
  3. Nautiakasi21/7/09 9:12 PM

    Ha ha ha ha CHRISTIAN BWAYA aka SIMBA ULANGA , hatimae kobe ametoka kwenye gamba lake...! (patamu hapo)umejificha sanaa, sasa ndo umejidhihirisha. Twende kwenye hoja zako dhaifu.

    Qur ani haijawahi na haitawahi kujichanganya, utajichanganya mwenyewe tu kwa kuisoma ukiwa "bias" na ukiwa hutaki kuielewa (sababu si ngumu hata chembe kuielewa). Kwanza lazima uelewe Qur ani sikitabu cha hadithi (kama hadithi za shigongo) kwamba ukisoma nusu aya inatosha kujenga hoja na kuandika pumba zote hapo juu ulizoandika. Kwa mfano tu kuna aya inasema "..ole wao wenye kuswali.." Kama akitokea mwehu akaishia hapo, atajaza maktaba kuwaambia wehu wengine kwamba uisla wenyewe unawaambia ole wao wenye kuswali, wakati aya zambele zimefafanuwa ole wake mwenyekusali yupi? yule anaeswali kwa kujionesha! Sasa hizo aya zako zinazosema muhammad ni muislam wa kwanza, ungejiuliza kivipi?wa mwanzo kwa wapi? Kama aya moja ni simple reasoning haihitaji kufika hata darasa la 7, Nimekwambia Muhammad alikuja KUHUISHA Uislam, inaamana kwa wakati wake uislam ulikuwa umekufa, kwa hiyo yeye akawa muislam wa kwanza kwa nyakati zake (haimaanishi kwa tangu dunia ianze), sababu tayari kuna aya nyengine inasema na wewe mussa ndio muislam wa kwanza, itoshe hiyo kukufundisha tena kwamba na Mussa alikuwa Muislam wa kwanza kwa Nyakati zake, sababu kwa wakati wake huo uislam ulikuwa umekufa, mungu alileta mitume kwa kila zama ili kuhuisha uislam, sababu ulishakuepo zamani. Ni kuulize swali hivi ukiskia mwanao anaambiwa ameshika nafasi ya kwanza kwa somo la hesabati darasani mwanao mwaka 2009,halafu ukamsikia jirani nae anasema mwanawe alikuwa mwanafunzi wa kwanza mwaka wa somo la hesabati 1998, shule hiyo hiyo, jee utakuja hapa uandike kwamba habari zinajichanganya??? Hivi unapata muda wakufkiria kidogo???
    Halafu unaposema Yesu mafundisho yake na falsafa zake hazina uhusiano, naomba nijue unaongea kama MKRISTO au Mwenyekiti wa Mdahalo. Kama unaongea kama mkristo uko sahihi, sababu ndo mafundisho yako yanavyokufunza, siwezi kulazimisha uamini nnavyoamini mimi.Zaidi mimi siamini kitabu chako kilichokupa hayo mafundisho na falsa za Yesu. Kama unaongea kama Mwenyekiti wa mdahalo, HAUKO SAHIHI hata kidogo, Rabda ungetoachanzo cha maelezo yako kwamba falsafa na mafundisho ya Yesu hayahusiani na uislam, chanzo hicho kisiwe AGANO JIPYA (bible). Mimi naongea kama Muislam, tunamini bila ya tone la shaka kwamba Yesu Ibn Maryam ni Muislam na mafundisho na Falsafa zake zilikuwa ni zakiislam, chanzo changu ni Qur-ani na baadhi ya aya za bible (injili) ambazo hazija haribiwa kwa kutiwa ufundi na wanaadamu. Wote tunaona kwenye bible yesu akiwafundisha wafuasi wake kutawadha (kutia udhu) na akiwasisitiza wafanye hivyo, wote tumeona yesu akiswali kwa kusujudu na mambo tele tu yanayoendana na uisla ambayo ukristo hata hawayakaribii yamo ndani ya bible hiyo hiyo bwana CHRISTIAN unayotumia kujuwa histori.
    Nakuja ngoja nikaswali...!

    JibuFuta
    Majibu
    1. Walter
      Kwanza kabisa nikupongeze kwa uelewa wako ambao nafikiri sio mmbaya uko sahihi japo hapa naomba kidogo tuwekane sawa ; kwanza swala la kutawadha au kusujudu au kuvaa mavazi fulanifulani haya yasikufanye ujenge hoja kuwa Yesu alikuwa mwislamu au kusema mkristo.Ieleweke wazi kuwa Yesu kipindi hicho alikuwa kwenye jamii ya watu ambao alizaliwa na kukuta tamaduni zao za kuvaa, kusali n.k ni sawa na Yesu angezaliwa katika kabila la kimasai bila shaka angevaa lubega .kwa hiyo aliwatawadha wanafunzi wake kwakuwa ilikuwa ni desturi ya watu wa jamii hiyo walikuwa wanajua maana yake ni nini lakini ndani yake kulikuwa na jambo la kiroho alilifanya Bwana Yesu na ndio maana ukisoma vizuri hapo utakuta anawaambia kuwa hamuelewi ninachokifanya maana yake hakuwatawadha kama wanavyojua wao. Kwa hyo ndugu tupende kusoma maandiko na hakuna din inayoruhusiwa kumsema mwenzie bali inapaswa tuheshimu tu imani za watu wote

      Futa
    2. Jmn kunamambo yanaitaji imani san yesu nina muhamadi ni nani tunapaswa kujiuliza wote kwa pamoja ni manabii sindio sasa basi usilamu ulikiwepo toka mwanzo ukisoma tibabu cha NEHEMIA 12.40 masheeh walikuwepo na wakristo natulikuwa tukiabudu na kusujudu pamoja sisi ni wamoja tangu mwanzo tatizo letu zote ni ubinadamu tunahitaji ama moja anahitaji kujiona yuko juu ya mwenzake wajamani si ni wanadamu tuliubwa kwa udungo na kwenye umbaji hakuna mkristo wala muslimu wajameni

      Futa
  4. Tukizungumza tukitetea dini flani flani tutaishia kukitetea dini hizo hizo.

    Kisome kitabu chako kama vitabu vingine. Jifunze dini nyingine kama unavyojifunza dini yako.

    Usijifungie kwenye kibiriti cha dini uliyoirithi kwa wazazi wako.

    Panua uelewa wako kwa kujifunza falsafa za dini nyingine kama Ubudha, Uhindu, Ushinto, Uyuda, Ukristo na kadhalika.

    Swala njema, japo nahisi itakuwa kwa kiarabu lugha ya waanzilishi wa dini yako.

    JibuFuta
  5. Mkuu binafsi na ku-respect ktk mambo mengine, lakini kwenye haya masuala ya dini kulingana na maelezo yako huna ulijualo.
    Dini zote mbili huzijui aya unazosoma unazisoma nusu nusu,acha mambo ya dini zungumzia vitu unavyovijua lakini masuala ya dini huyajui mkuu.
    Acha kufuata mkumbo.

    JibuFuta
  6. Kuna kitabu nasoma, kinaitwa,
    "CULTS WORLD RELIGIONS AND YOU"
    Kinazichambua hizi dini za mapokeo, najifunza mengi humo.
    naomba mkitafute kinaweza kusaidia kumaliza huu utata.......

    JibuFuta
  7. Shabani,

    asante kwa kitabu. Nitakitafuta.

    JibuFuta
  8. Nilitaka kusahau:

    Msomaji wangu unayetumia jina la msolopa sasa hivi,

    Si mara zote anaponadika mtu lazima awe anajua. Mara nyingine mtu huandika kuuliza.

    Mie siandiki kuelimisha kama unavyofikiri. Naandika kutafuta maoni ya watu wa namna yako wanaojua. Naandika kukufanya utuambie unachojua ili hatimaye ikiwezekana tuelimike. Kusudi hilo hata hilo halitatimia kama utasubiri nijue kila kitu ninachoandika.

    Bila shaka tumeelewana 'mkuu' unayejificha.

    JibuFuta
  9. Salamu(amani) juu yenu, naomba watu wafahamu ya kuwa uislamu si dini iliyopewa jina na muasisi fulani na kusema kuwa wafuasi wake waitwe waislamu, la hasha, bali Uislamu jina hili ukilitafsiri kwa lugha y kiswahili ni amani, kujisalimisha, kunyenyekea ndiyo maana yake. Mtume Muhammad (S.A.W) si muanzilishi wa dini hii, na emeeleza wazi kuwa uislamu upo yaani (kujisalimisha kwa Mungu) toka kuumbwa kwa ulimwengu. Allah aliumba ulimwengu ili vitu vyote vimtii na kujisalimisha kwake, lakini viumbe hawa wawili (majini na watu) walipewa khiari na matamanio, na huo ndiyo mtihani wenyewe tulioumbiwa nao, ambao watu tunaelekezana, kuelimishana, kujadiliana, kuzozana mpaka tunafikia hata kugombana na kutoana roho katika mambo hayo.Ni kwamba watu walioishi mwanzo walikuwa na mfumo wao wa maisha walipewa muongozo wa kuishi na Muumba kwa kuwapelekea mjumbe kutoka kwake, hivyo basi kutokana na vitabu vya dini havipingani kabisa kuwa Adam na Hawa(Eva) walipewa muongozo na Allah na kuambiwa wasiukaribie mtu huo walioukatazwa, kwa kuwa walikuwa na khiari na matamanio ndiyo yaliyowafanya walikhalifu amri hiyo na kutokea yaliyotokea kwa kuwa walikuwa wanyenyekevu wakaomba msamaha na hatimaye wakasamehewa, siyo kama Ibilisi(Shetani) ambaye hakuwa mnyenyekevu na kuangamia.Watu wasifikirie Uislamu ni dini ya Muahammad (S.A.W) na kwa ajili ya waarabu tu, hapan kwani tukisoma historia ya kiislamu tunamkuta Bilal (R.A) muadhini wa mtume ambaye alikuwa muahabesh(muafrika), tunamsoma Salman Farsi (R.A) ambaye ni mfarsi(Muiran), kuna wakina Bukhari watu kutoka sehemu za Urusi na Mayahudi wengi tu waliosilimu. Mtume alilingania dini hii kwa wafalme wengi tu wa pande za ulimwengu. Kwa hiyo Uislamu ulikuwepo kutoka kuumbwa kwa dunia na mpaka mwisho wake.Dini nyingine huenda zilikuwa ni za usahihi kutoka kwa Allah ila baada ya kupita muda baadhi ya watu waliharibu dini hizo ikiwa kwa ujinga au maslahi yao binafsi. Ikiwa Allah kaumba ulimwengu na vilivyomo ndani yake hivyo hahitaji chochote kutoka kwetu, isipokuwa unyenyekevu wetu tu, na huo ndiyo Uislamu wenyewe, na kitu kikubwa ni kumpwekesha yeye tu bila ya kumfanyia ushirika. Na huo ndiyo ulikuwa ujumbe wa mitume wa Mungu. Uislamu si jina la mtu au mahala au kitu bali ni kitendo cha mtu kujisalimisha, kunyenyekea kwa Muumba na haikuanzishwa na mtu bali ni mfumo wa Allah aliouweka kwa waja wake ambao wanataka kufaulu duniani na akhera.Shukran.

    JibuFuta
  10. Mie napata shida kidogo. nilifikiri bwaya anadadisi tarehe dini hizi tunazoziita 'zetu' zilianza. sidhani kama anaongelea dini ipi iko karibu na mungu na nyingine iko mbali. kinachotakiwa kuwa karibu na mungu ni roho yako tu hata kama wewe si wa 'kule' ama 'huku'. namaanisha usiibe, usisengenye, usizini, tenda mema, samehe, usiwe na kisirani, acha tamaa, saidia masikini, na kadhalika na kadhalika. Fanya haya yoote na usifanye ambayo hata wewe usingependa kufanyiwa halafu tuone mungu akunyime ufalme wa hiyo pepo eti kwa sababu hukuwa mwislamu ama mkristo. Sana sana mabishano (badala ya kufundishana) yanatupotezea-ga muda saaana wa kufanya vitu vingine.

    JibuFuta
  11. Kazi nzuri na yenye kuleta changamoto njema. shukran

    JibuFuta
  12. Bwaya kama upo katika kutafuta haki kati ya uislam na ukristo ipi ni dini ya kweli ambayo ndio hasa ni dini waliyokuja nayo manabii na inayoridhiwa na mungu mwenyewe basi wakati unatafuta ukweli ingia katika msako huo wewe kama wewe usiingie na imani yako, acha akili na moyo wako ukiwa huru kabisa ndio utauona ukweli ulipo kirahisi zaidi vyenginevyo itakuchukuwa mda mrefu sana kuuona ukweli......qur aan haina makosa yoyote kuhusiana na nani hasa alikuwa muislam wa mwanzo ila ufahamu wako mdogo ndio tatizo linalokusumba ww kumjua ni nani hasa muislam wa mwanzo.....

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kwa Mimi nashangaa mashehe wanaieleza historia ya yesu vizuri tu kwamba alizaliwa pasipo mbegu ya mwanaume na wanajua alifanya mambo makubwa magumu ambayo hakuna mtume yoyote Wala nabii aliefanya wanajua kwa Yesu alimfufua Lazaro aliyezikwa kwa muda wa siku nne wanajua na wanajua kwamba hao wayaudi walimuua lakini hawataki kabisa kusema mbele ya imma kwaaamba Yesu kristo alifufuka siku ya tatu Tena alivyozikwa usiku ule wakawatuma walinzi wakawaaambia kaeni hapa kaburini muone ujanja wake kama atafufuka usiku wa j mosi saa sita ukashuka mwanga mkaliiii wenye mithili ya jua ambao katikati yake alikua malaika mkuuu wa mbingini Gabriel wale walinzi wakazimia kwa woga malaika akaviringisha jiwe kwa kidolee yessuuu akatoka kaburini akiwa mzimaaaaaaaaaaa hili hawasemi hawasemi ktk wafilipi neno linaema Mungu akamkirimia jina lipitalo majina yote ili kila ulimi umkiri na kila goti lipigwe kwa masihi Yesu kristo

      Futa
  13. ni sawa kama unatafuta ukweli sio kwa njia hiyo ya kuchambua kitu usichokijua.
    we huijui so tafuta waliokua na elimu ya hicho unachotafuta uelimishwe.
    hapo umesema Qur ana inakupa maelezo yanayokizana inamaana huna elimu juu ya Qur ana wala neno uislam ulichofanya wewe ni kuchukua aya moja na kua ndio kigezo chako.
    kumbuka kua Qur ana sio kama gazeti ukiwa unasoma unaanza mwanzo na kumaliza mwisho.

    JibuFuta
  14. Hoja amabazo hutumika kudhibitisha ya kwamaba yesu ni muislamu na sio mkristo huwa zinanishanagza sana. kwa mfano; Kutawadha, Kusujudu, Kuingia katika msikiti, kuingia ktk masinagogi. sababua zinazonifanya nishangae ni kama zifuatazo. Je msikiti (sinagogi) ilikuwa nyumba ya ibada tu kwa dini ya kiislamu, ikiwa waumini wa Kiyahudi waliabudu katika masinagogi ambamo kristo nae alaibudu kwa nini tusiseme alikuwa muumini wa dini ya kiyahudi?. Je ikiwa wayahudi walitawadha kwa nini tusiseme yesu alikuwa muumini wa dini ya kiyahudi?. ikiwa tunasema yesu hakuingia kanisani kama hoja ya kumtenganisha na ukristo kwa kutoa mfano wa hekalu, na kwa sababu mabudha husari katika Mahekalu Je ni hahalali kusema yesu alikuwa budha?.

    JibuFuta
  15. Namuomba Bwaya afanye utafiti kabla hajaandika hasa maswali ya dini yanataka kufanya utafiti wa hali ya juu .Hasa ukiandika kupitia mtandao maana wasomaji wake wana uelewa tofauti katika dini.

    JibuFuta
  16. Ndugu Abdi Salumu Fadhili ninakuunga mkono maneno yako kuhusu kumjibu huyu ndugu Christian Bwaya Maelezo yake inaonyesha ameyakopi kwenye wikipedia. inaonyesha hajuwi kuwa Dini ya Kiislam hakiuanzishwa na Mtume Muhammad S.A.W. Bali yeye huyo Mtume Muhammad S.A.W. alikuja kuiendeleza hiyo Dini huko Uarabuni. Ndugu Christian Bwaya kama huelewi Dini ya kiislam Muanzilishi wake ni nani ? Jaribu kuuliza au fanya utafiti wako usijisemee maneno wakati huna uhakika nayo unakufuru wewe.

    JibuFuta
  17. cha msingi nikufata sheria za mungu kumi...basi upumzike hyo siku yake ya sabato..napia ujue chanzo cja dini zote za leo..ivi unajua freemason iliaza edeni...baada kaini kuumua abeli..yule ndie mwazilishi wa freemasoni..so dini hizi za kikristo na za kiislam zilitokea kwa ajili ya kupinga uonfizi wa shetani yani lucifer ambae ndie mkuu wa freemasoni..lakini dini ya kwanza ni ya wayahdi ..fatilia vzuri maandiko au soma kitabu kilichoandikwa na john robbinson..kina itwa proofs of a conspiracy against all the religions and govement of europe..acha ubishi jifunze maandiko upate maarifa

    JibuFuta
  18. kwanza kabla ya yote unafaa ujuwe nini maana y aneno islam home for you

    JibuFuta
  19. QUR'AN 7:143-144

    (143) - وَلَمَّا جَاءَ مُوسَىٰ لِمِيقَاتِنَا وَكَلَّمَهُ رَبُّهُ قَالَ رَبِّ أَرِنِي أَنْظُرْ إِلَيْكَ ۚ قَالَ لَنْ تَرَانِي وَلَٰكِنِ انْظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي ۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا ۚ فَلَمَّا أَفَاقَ قَالَ سُبْحَانَكَ تُبْتُ إِلَيْكَ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُؤْمِنِينَ

    Na alipo kuja Musa kwenye miadi yetu, na Mola wake Mlezi akamsemeza, alisema: Mola wangu Mlezi! Nionyeshe nikutazame. Mwenyezi Mungu akasema: Hutoniona. Lakini utazame huo mlima. Ukibaki pahala pake basi utaniona. Basi alipo jionyesha Mola Mlezi wake kwa mlima, aliufanya uvurugike, na Musa akaanguka chini amezimia. Alipo zindukana alisema: Subhanaka, Umetakasika! Natubu kwako, na mimi ni wa kwanza wa Waumini.

    (144) - قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنِّي اصْطَفَيْتُكَ عَلَى النَّاسِ بِرِسَالَاتِي وَبِكَلَامِي فَخُذْ مَا آتَيْتُكَ وَكُنْ مِنَ الشَّاكِرِينَ
    (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Musa! Mimi nimekuteuwa wende kwa watu na Ujumbe wangu na maneno yangu. Basi chukua niliyo kupa na uwe katika wanao shukuru.

    JibuFuta
  20. QUR'AN 6:162-164

    (162) - قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
    Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.

    (163) - لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ
    Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.

    (164) - قُلْ أَغَيْرَ اللَّهِ أَبْغِي رَبًّا وَهُوَ رَبُّ كُلِّ شَيْءٍ ۚ وَلَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ إِلَّا عَلَيْهَا ۚ وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ ۚ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّكُمْ مَرْجِعُكُمْ فَيُنَبِّئُكُمْ بِمَا كُنْتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ
    Sema: Je nitafute Mola Mlezi asiye kuwa Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ndiye Mola Mlezi wa kila kitu? Na kila nafsi haichumii ila nafsi yake. Na habebi mwenye kubeba mzigo wa mwenziwe. Kisha marejeo yenu ni kwa Mola wenu Mlezi, naye atakuambieni mliyo kuwa mkikhitalifiana.

    JibuFuta
    Majibu
    1. Makundi:
      Lazima kuna dini ambayo imezitangulia nyingine; si kweli kwamba zote zilianza kwa pamoja, mimi ni Mkristu hivyo nafahamu kidogo kuhusu dini hii kwamba imeanzishwa lini, na nani, mazingira yapi, na ilikuwaje, kwa upande mwingine, je Uislam ulianzishwa lini, nani wahusika wa kwanza, ilikuwaje, maandiko ya kabla ya mohamad ni yapi? yako wapi? yalitumiwa na nani, kwanini ihuishwe mara kadhaa (Na Musa na Mtume Muhamad), lini ilipotea, kwanini?, na maswali mengineyo ambayo yatotoa uhalisia wa dini hii kuanzishwa kable ya Ukristu

      swali la pili:
      Ni kweli kwamba Musa wa kwenye biblia ndiye huyohuyo wa kwenye Masaafu? Kwanini?
      Ni kweli kwamba Yesu wa kweye biblia ndiya Issa Bin Mariam,? Kwanini?
      Je ni nini kinachodhihirisha kuwa watu hawa ni walewale kwa pande zote?
      Je misikiti ndio masinagogi? na wale waliosali na Yesu walikua ni waislam?
      Pia kuna sehemu katika biblia ambapo Yesu alihubiri: Je aliwahubiria Waislam au Wayahudi?.

      Futa
    2. Kabby.
      Ukitaka kuyajua haya mambo vizuri lazima uanze kusoma Biblia kwa kuwa ndicho kitabu cha kwanza kuandikwa. Hiyo Quran imeandikwa karne tano baadaye ambayo hiyo ni miaka 500. Sasa kama mnasema uislam ulikuwepo tangu mwanzo je ulikuwa ukitumia kitabu gani? Na kama mnasema kuna maandiko yamechezewa, je kitabu cha maandiko ambayo hayakuchezewa kiko wapi? Maana mnasema Quran imeletwa kwa sababu kitabu chenu cha mwanzo kilichezewa je mwanzo mlikuwa mnatumia kitabu ga ni na kiko wapi ili tupate kukisoma wote tuone yaliyomo?

      Futa
  21. nafikiri lengo la bwana bwaya ni kuchokoza ili aibue hisia za watu katika mazungumzo ili watu wengi waweze kuchangia mada hii. Kama lengo lake ni hilo nikweli wengi wamechangia na tumepata faida kubwa kwa mjadala huu. Kikubwa tu ambacho bwana bwaya naweza kukushauri wakati mwengine ukihitaji kuandika kuhusiana na masuala ya dini ama imani zenye wafuasi ni vyema ukaandika katika mfumo wa swali zaidi ili kutoa nafasi kwa wanaojua waweze kuelimisha watu kwa ulichokiuliza na si kuandika kana kwamba unauhakika na unachokiongea. Hii itapelekea wachangiaji wanaoamini katika hiyo imani kuchangia "with negative emotion" na kusababisha elimu uliyopanga watu waipate ishindwe kupatikana

    JibuFuta
  22. Mkorogo wa quran. Unamsilimisha adam akiwa kaburini, ibrahim akiwa kaburini.

    JibuFuta
  23. Ahsante elibariki, nimekupata vilivyo naomba ndugu waislamu mtudhihilishie kuwa Musa, yesu na wengineo wa kwenye Qur'an kuwa ndio wa kwenye bible na kwa kuongeza tudhibitishieni pia kuwa Allah ni Yehova

    JibuFuta
  24. We ndio umechemka kweli

    JibuFuta
  25. Kwanza Quran yenyew inasema muhamadi kajakukamilisha uislamu wew inasema kaanzisha muhamadi haya waweza nilitea sehemu katika Quran inayosema uislamu umeanzishwa na muhamad

    JibuFuta
  26. Ktk kitabu chake maisha yako nabii mohamad, kinasema, yeye 'na mkewe ndio wa kaanza kuwa waislam, 'na ktk kitabu cha asili yake majini, kinasema, mwislam wa 3 aliyesimamishwa 'na mohamedi ni SHETANI, ambapo adamu 'na hawa, wa kushindwa kumsilimu

    JibuFuta
    Majibu
    1. Wewe ndiyo hujielewi kabisa.

      Futa

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Pay $900? I quit blogging

Haiba ni nini?

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Heri ya mwezi mpya!