Blogu zetu na uhuru wa maoni

Blogu ni nyezo ya kuuwezesha uandishi wa raia. Kutupa fursa ya kupaza sauti zetu bila masharti.

Vyombo vya kizamani vya habari havitupi fursa hii. Mengi ya yanayotangazwa na kuandikwa ni yale anayoyataka mmiliki ama Mhariri. Wasomaji, wasikilizaji ama watazamaji hubaki na haki ya 'kumeza' kilichoandaliwa. Na hata maoni yao yanapoletwa, kazi kubwa huwa ni kuyaminya yalingane na msimamo wa mmiliki ama mhariri.

Jambo hili ni tofauti katika blogu. Huku, msingi mkuu ni majadiliano. Anayeandika, hufanya hivyo akialika mawazo ya wasomaji yanayoweza kuwa bora kuliko yake.


Kwa hivyo, nimwombe msomaji wangu mmoja anayeficha jina lake kuutumia huru huu, kusema kile anachodhani ni sahihi kwa njia yoyote anayoona inafaa lakini sio kujaribu kusitisha mijalada inayomkwaza.

Vilevile, si lazima sana kuficha jina. Kama una uhakika na unachosema, kwa nini ujifiche kwenye kichaka cha majina bandia?

Maoni

  1. bwaaaauya

    ki\uficha jina ni moja wapo ya uhuru wwa blogu ambao lazima tuuupokee. kwani mimi nina uhakika gani kama wewe unaitwa Christian Bwaaya? au wewe una uhakika gani kama mimi ni mimi na ile picha pale ni sura yangu kweli? mmbona wewe sura yako kwenye picha umeweka kisogo?

    ni uhuru ndg, usione soo

    JibuFuta
  2. Nakubaliana wewe mia kwa mia.

    Pengine kuna haja ya kufikiri zaidi kuhusu wazo na wala si aliyelitoa. Kwamba mtu yule yule anaweza kuja na majina tofauti ya kila wazo analopata, kwa sababu anazozijua yeye. Hilo lisiwe tatizo.

    Kwamba Kamala (ambaye hatuna hakika kama ndiye mwenye jina hilo) akawa Nautiakasi, halafu huyo huyo akawa Msolopa ili tu kusema kile alichonacho. Huu ndio uhuru tusioupata kwenye nyenzo zilizopendwa.

    JibuFuta
  3. Nafurahi kwani blog ni zaidi ya uhuru wa kueleza fikra zako.
    Sidhani kama kuna ulazima wa kuficha jina.
    Kwani, blog zaidi ya kuibua majadiliano ambayo hukuza uelewa, pia hujenga urafiki.
    Hivyo sidhani kama ni uungwana kuwa na rafiki asiyependa ajulikane.
    Ni wangu mtazamo.

    JibuFuta
  4. bado ni sehemu ya uhuru, wahaya husema; ka'kitandugao

    JibuFuta
  5. Ndio Mtanga. Tunaweza kuanza kukutana kama wanajuimuya ya blogu, tukazungumza ana kwa ana na kubadilishana mawazo. Sasa inakuwaje kwa wale ndugu zetu wanaotumia majina bandia wakati pengine tungependa kukutana?

    Kamala. Nimekupata vizuri sana, kwamba kujenga urafiki nalo ni jambo la uhuru. Ndio.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia