Pa kuanzia, ni pale uliko

Ni vizuri kuanza na kile ulichonacho, na si kile usichonacho.

Fursa mara zote, huwa pale ulipo na katu si kule ulipokuwaga.

Suala la msingi ambalo kila mmoja anapaswa kuliweka sawa, si kile ambacho angeweza kukifanya kama angekuwa na muda, elimu na namna ya kufanya, lakini kile ambacho angepaswa kukifanya kwa kutumia vile alivyonavyo.


Mara nyingi tunapuuza vile tulivyonavyo, na kupoteza nguvu nyingi kutafuta kile tusichonacho. Matokeo yake tunajikuta tunapoteza hata kile tulichonacho.

Ni hivi. Yafaa sana kufanya kiwezekanacho, kwa kutumia ulichonacho, pale pale uliko.

Usiozeshe ulichonacho kwa kutamani usichokuwanacho.

Pengine unadhani huwezi kukitumia ulichonacho. Ukweli ni kwamba huwezi jua uwezacho mpaka kwanza ujaribu. Anzia na uliko kufikia unakotaka kwenda.

Pengine hujui ulichonacho. Nikwambie? Niseme, sisemage?


Itaendeleaga...

Maoni

  1. kwa maana nyingine tunashauriwa kuisahi maisha tuliyonayo sasa, kwani sasa ndiyo wakati pekee tuliohao na tuwezao kujivunia kuliko jana (kabla) na kesho (baadaye), enjoy every momnt you have!

    asante kwa hili ndg

    JibuFuta
  2. Tumshukuru Mungu kwa uzima!
    mdada nasema kweli mara nyingi tunapuuza vile tulivyonavyo kwa kupoteza nguvu nyingi kutafuta kile tusichonacho unajua nini kutojiamini pale ulipo na kutamani usipopaweza mpaka unajikuta unapotokwa na hata ulichonacho.Tumia elimu au ujuzi ulionao ili kufanikiwa

    JibuFuta
  3. Ni vizuri kuanza na nafasi iliyopo na ni vema ikitumiwa vizuri.Pia izingatiwe kuwa nafasi/nilichonacho ndicho kitakachosaidia kupata kingine.
    Cha msingi hapa ni mipango mizuri na endelevu.Mtumizi mazuri ya muda na kutoa uzito unaostahili kama kaka Bwaya alivyoainisha kwenye mada iliyotangulia.

    Ni vizuri sana ktk maisha tukiwa na njia mbadala mbali na vile vitu tuvitegemeavyo zaidi.Kwa mfano kijana anayesoma ktk shule fulani kama atakuwa ameshapitia kozi kadhaa basi atakuwa huru sana ktk kusoma kusoma kuliko yule ambaye anategemea kule kusoma tu(japokuwa hapa mtu anaweza kubweteka)
    Ni hayo kwa sasa.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?