Unayatumiaje masaa ishirini na mane?

Binadamu wote ni sawa kwa maana nyingi. Usawa mmoja wapo ni kiasi cha muda ambacho kila mmoja wetu anacho.

Kila binadamu anayo masaa ishirini na mane kwa siku. Masaa yaliyotimia yenye dakika sitini.

Kinacholeta tofauti, ni namna tunavyoyatumia masaa haya kwa faida. Kile tunachofanya katika kila 'lisaa' linalopita mikononi mwetu.


Wakati wapo wanaoweza kupangilia mgawanyo wa muda kwa siku inayofuata, na kutathimini adabu waliyo nayo kwa kile walichopanga, wengi tunajikuta tunafanya yale tusiyoyapanga na hivyo hatuna namna ya kutathmini matendo yetu ya siku.


Watumiaji wazuri wa muda wanao uwezo mzuri wa kusema 'hapana sikupanga hili' wakati watumiwaji wa muda hawana uwezo huo.


Ninaposhindwa kusema hapana mahala ambapo nilipaswa kufanya hivyo, ni namna bora zaidi ya kuteketeza muda.

Ikiwa tutaweza kudhibiti matumizi ya muda, tutakuwa tumeweza kuyadhibiti maisha yetu.

Maoni

  1. nini kimekufanya uja na mada hii? kwa sababu hujaonekana mpaka watu (hasa mzee wa C/MOTO) wakadhani ulikuwa labda mmoja wapo wa abiria wa ndege zile? unamaanisha huna nidhamu ya muda wa ku-blog? unamaanisha wanaokutembelea wana nidhamu mbovu ndio maana haupo? umeona baadhi ya watu wakipoteza muda wao vile usivyopenda?

    kwa nini, kwa nini, Y?

    (tuelewane; sina lengo la kukukwazwa wewe wala msomaji yeyote)

    JibuFuta
  2. Habari kaka! unatubeep au umerudi jamani,tulimis topic zako hasa mimi mdada mpk nikakutext.

    JibuFuta
  3. Ndugu Kamala,

    Nimekuja kubaini kwamba ni utovu wa nidhamu ya muda ndio ulinifanya nipotee bloguni. Baada ya kujitathmini, nikagundua kuwa hata kama ni kweli mambo yalipandana, lile na hili, yale na hayo; kama ningekuwa na adabu ya muda nisingepotea kivile. Kinachochangia upotevu wangu (mara nyingine) ni kukosekana utaratibu wa kuheshimu kila wajibu nilio nao kwa uzito unaostahili.

    Mafunzo hayo niliyoyapata, nilidhani yangeweza kushirikishika na wenzangu ambao wengi wao tulijadiliana kwa kirefu nyuma ya pazia katika kipindi chote cha ukimya wa blogu hii.

    Mdada,

    Nimepiga kabisa 'sijadipu'. Karibu tujadiliane.

    JibuFuta
  4. Karibu sana kaka Bwaya, hakika umepiga kweli kweli, tena full dola mzee.
    Ulichosema ni sahihi, tukiutawala muda vizuri, kamwe hatutasingizia majukumu, mambo kusongana na kadhalika.

    JibuFuta
  5. nimekupata vyema Bwaya. lakini maisha haya kuna nyakati za deadlines, duh hata kupost kitu kidogo inakuwa noma. niewahpitia nyakatika kama hizo japo kublogu pia kuna umuhimu na nafasi yake.

    JibuFuta
  6. Kissima na Kamala nakubaliana nanyi. Mpangilio sahihi wa majukumu tuliyonayo hutupa nafasi ya kufanya mambo mengi katika ufanisi wake.

    Nilichokibaini ni kwamba mara nyingi ni rahisi sana kuyatelekeza majukumu yale yanayotegemea zaidi hiari bila deadline, huku tukiyatahayarukia yale yanayoonekana kuwa na deadline.

    Kwa msingi huo, nadhani kama anavyosema kamala, ni muhimu kujiwekea deadline hata katika yale majukumu yanayoonekana kuwa na hiari fulani kama haya ya kublogu.

    Katikati ya utitiri wa majukumu, bado ni kweli kwamba zipo dakika nyingi sana huzipoteza kwa porojo na mambo mengine yasiyo na ulazima. Laiti kama tungeweza kuzitumia vyema dakika hizo kwa ukamilifu, hicho kinachoitwa kuwa bize kisingekuwepo. Na tungeweza kuyatimiza majukumu yetu yote kwa ukamilifu basipo kujiahidi siku nenda siku rudi bila utekelezaji wa maana.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging

Haiba ni nini?

Heri ya mwezi mpya!