Wazazi wanaweza kukwepa lamawa?

Nilibahatika kushuhudia ugomvi mzito wa wazazi wenye hasira kali kwenye daladala. Halmanusra wamteketeze rafiki yangu.

Ilivyokuwa ni kwamba konda alimporomoshea matusi ya mwilini abiria mwenzetu. Kuona vile, kila abiria alimsulubu konda kwa kosa la kushindwa kuudhibiti mdomo wake.

Basi, rafiki yangu kuona vile, akawaomba wazazi wale kutokumlaumu konda, akidai kuwa kosa hasa ni la wazazi wa konda yule.

Kauli ile ilileta tafrani la kutisha kiasi kwamba mashambulizi yote yalihamishiwa kwa rafiki yangu.

Japo mjadala ule haukuweza kufikia tamati nzuri, lakini ulinipa tafakari.

Kwamba, kwa nini wazazi walewale wanaogeuka mbogo pale malezi yao yalipohusianishwa na udhalimu wa watoto wao, hao hao hujipiga piga kifua wanapohusishwa na mafanikio ya watoto wao?

Kwanini mtoto anapoharibika wazazi hukwepa kuwajibika moja kwa moja lakini watoto wanapofanya vizuri, wazazi kudai sifa kwa lazima?

Maoni

  1. Hiyo ilikuwa kali kuliko!
    Mi' nina mtazamo wangu. Kuwa maisha na tabia ya mtu yeyote ukubwani, huwa imeathiriwa na malezi aliyopewa.
    Kwa mantiki hiyo, binadamu akiwa na vitendo vichafu ukubwani, itazame familia yake. Hapo utagundua kuwa kama hawakuwa wakimgombeza, kumchapa na kumkandamiza mara kwa mara katika utoto wake, basi walikuwa wakigombana wao mara kwa mara. Hali hiyo ikasababisha athari katika makuzi ya mtoto.
    Hivyo wazazi hawapaswi kukwepa lawama kwa kuharibika kwa mienendo ya watoto wao.
    Vivyo hivyo, hata katika mafanikio yawayo yoyote yale katika maisha ya mwanadamu, basi wazazi ama walezi wake huwa wameacha athari.
    Ni hayo tu!

    JibuFuta
  2. Pamoja na wazazi kulaumiwa lakini pia kijana lazima nae abebe lawama kwa upande wake. Si kwa sababu wazazi walikuwa masikini basi na watoto wawe masikini.Kwa sababu kijana ameshakuwa na akili ya utambuzi hana budi kujikomboa mwenyewe kutoka ktk athari zile za makuzi mabovu.

    Ikumbukwe pia mazingira anayofanyia kazi kijana huyu yanamchango mkubwa sana ktk tabia yake.

    JibuFuta
  3. mdada ninasema kwa upande mwingine kwa kitendo kama hicho mazingira pia yanachangia, mtu kama huyo au mtu wa aina hiyo amelelewa vizuri na wazazi au walezi wake vizuri kabisa ila alivoanza maisha yake pamoja na jamii iliyomzunguka nina maana majirani au marafiki na hali ya maisha ikamchanganya basi anajiona hana thamani katika jamii na ameshakata tamaa ya maisha kila analotamka kwake anaona sawa.mfano mzuri watoto wa wachungaji wako tofauti na wazazi wao mambo wanayofanya uraiani je alaumiwe nani?

    JibuFuta
  4. Kissima, athari za makuzi mabaya si jambo linalohisika katika ufahamu (unconscious) kwa maana kwamba mwathirika hawezi jua kiuwazi kwamba ameathirika.

    Unapomshauri mtu huyo ajikomboe, huoni kwamba utakuwa unamkabidhi kazi inayozidi uhalisia?


    Mdada,

    katika watu ninaodhani wanajisahau ni hao wachungaji. Wanatumia muda mwingi kuchunga kondoo kuliko kuchunga watoto wao. Kwa hiyo haishangazi kwamba watoto wao mara nyingi wanachora mshazari wa kitabia ambazo kimsingi ni mwangwi wa udhaifu wa wachungaji wenyewe...

    JibuFuta
  5. A person becomes what the parents invest in him. We are the product of parential genes which convey the traits we may have.

    There is no way an honest parent may deny the reflected behaviours in his child because on addition to the genetic truth, the influence of his parenting style plays a role on what the child will become.

    The argument made by Mdada and Kissima are doubtful since a child to not choose the personalities they happen to have.

    The question of the environmental effect is of no use to blame the child himself.

    Strong parenting style may guide a child to overcome the environment variables on his own. Parents make a narrow escape in this respect.

    I like the discussion.

    JibuFuta
  6. Bwaya, ukizungumzia swala la unconsciousness ina maana kwamba hata wazazi hawapaswi kulaumiwa bali wale mababu zetu wa zamani.
    Mimi naamini kuwa tabia hizi zinaweza kubadilika, ni swala tu la kujielewa na kuweka azimio la kuachana na tabia zisizofaa(ukombozi binafsi)

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Kama sio utumwa ni nini hiki?