Nini hukifanya kitabu kuwa kitakatifu?

Niliyapenda maswali ya mwanazuoni Kamala. Sijayajibu, nikisubiri wengine wayajibu kwa haki.

Ninaandika kinachotoka moyoni na nimekitafakari muda mrefu.

Ninahitaji kuuelewa 'utakatifu' wa vitabu fulani tunavyoviogopa.



(picha kwa hisani ya 3.bp.blogspot.com)
Vinaongoza 'ushabiki' wetu kidini, na vinafikirika kuwa mamlaka ya ufahamu wetu.

Tukiwa wakweli, vitabu hivi viliandikwa na watu. Hata kama wengine walidai kuwa 'mabomba' ya ujumbe kutoka kwa Mungu, lakini walikuwa watu.

Tafsiri 'sahihi' ya vitabu hivi inahitaji imani. Akikisoma asiye na imani, anapata ujumbe tofauti na yule mwenye 'imani.'

Sentensi zinazoeleweka, zinapindwa-pindwa kukidhi mukhtadha wa kiimani.

Ningependa kujua hasa, vipo vitabu vingapi vitakatifu? Utakatifu wa kitabu unatokea wapi na ni nani mwamuzi wa utakatifu huu? Je, kitabu kitakatifu hakiwezi kusomwa bila uumini na kikaeleweka vizuri zaidi? Je, kitabu kitakatifu ni kweli tupu?

Maoni

  1. Mimi naamini kitabu kitakatifu ni kila ambacho watu wenyewe wameamua kuwa ni kitakatifu. Ni mawazo yangu!!!

    JibuFuta
  2. Swala la vitabu vitakatifu linabaki pale pale kuwa ni imani.

    Imani ni nini?
    Wakoloni walipoleta dini waliweka misingi fulani ktk ndani ya dini ambayo kila mmoja alilazimika kuifuata. Sasa hiki kinachoitwa imani ni taratibu na kanuni zilizowekwa ktk dini enzi hizo.Pengine heshima pamoja na utakatifu wa vitabu ambavyo leo hii huitwa vitakatifu ilikuwa ni miongoni mwa kanuni na taratifu zilizokuwa zimewekwa.


    Imani hairithiwi, mtu binafsi anaweza kuanzisha na pia kuachana na imani regarding kwamba utu na dhamani ya binadamu inalindwa.


    Izingatiwe kuwa kanuni na taratibu za mahali fulani zaweza kuwa ni imani za jamii hiyo zinapotumika muda mrefu.


    Watu (watoto) wanavyoamini kuwa wakiwaruka wenzao wale waliorukwa watakuwa wafupi,mtu akichapwa na ufagio au mwiko hata pata mke,kupita katikati ya watu waliosimama barabarani ni vibaya. Haya ni baadhi, yapo mengine mengi.Haya yangepewa mkazo unaotakiwa na yakawekwa kwenye vitabu yawezekana kabisa leo hii kitabu hiki kingekuwa kitakatifu na imani juu ya haya ingekuwa kubwa na kingeaminiwa kama vitabu vitakatifu vya leo vinavyoaminiwa.


    Ya mila nayo yangewekwa kwenye vitabu ingekuwaje?

    JibuFuta
  3. Kissima,

    Kwa hiyo, kama wazee wetu wangepata nyenzo, wakayaandika masimulizi yale ya kimila katika kitabu, leo hii tungekuwa na kitabu kitakatifu kama vile vya Wayahudi, Wahindi na Waarabu?

    JibuFuta
  4. Tena ingekuwa na nguvu kuliko hii tunayoisujudia hivi sasa kwani ingepewa uzito mkubwa kutokana na kigezo kwamba yalimo yangekuwa yanahusisha na yangetokana na mazingira yetu moja kwa moja.


    Mtu mwenyewe anaweza kujijengea imani yake mwenyewe na akiamua imani ile ife anaweza hivyo imani hufa na huzaliwa.

    Mimi naweza kuweka imani kuwa kwa kusaidia wengine nitakuwa huru na nitakuwa na mafanikio.Kama ninaimani na hili hakika lile nilitakalo litafanikiwa.

    JibuFuta
  5. Kitabu Chochote kitakatifu kinachodai kuwa ni ufunuo kutoka kwa Muumba huwa kinafanyiwa (falsification test) kikiweza kupita hapo basi kinakuwa hakiwezi kupingika. Quran ni kitabu ambacho mtume Mohamed alifunuliwa na Mungu na kuwaamuru wafuasi wake waandike, hakuna Qurani ya Abubakar wala ya Omar. Si kama Biblia ambayo imeandikwa na waandishi baadaye baada ya Yesu kuondoka, ndiyo maana utaona kuna kitabu cha Mark, Luke, Mathew, John.Ningependa watu waweze kupata Kitabu Injili halisi kilichoandikwa kwa lugha ambayo Yesu aliyokuwa akiizungumza kama kipo na si hizi Biblia tunazozisoma ambazo zimefasiriwa katika lugha mbalimbali ili tuweze kuupata ujumbe halisi.

    JibuFuta
  6. Mimi bado nipo nyuma kiuelewa kuhusiana na mambo haya ya dini na imani.
    Nashukuru hili ni darasa zuri sana kwangu.

    JibuFuta
  7. Ndugu anony, unataka kuniambia kuwa mpaka sasa Kurani haijaandikwa kwa lugha nyingine zaidi ya kiarabu?

    Hata hao waliopewa amri ya kuandika kurani nao ni waandishi pia.Huoni kwamba kama angeandika Mtume mwenyewe ingekuwa kitu tofauti?

    Hata hao uliowaorodhesha kama waandishi ni wafuasi wa Yesu kwani hata kuandika tu habari za Yesu tu huo tayari ni ufuasi na utume.
    Wewe mwenyewe kama ni muislam kwa kuwa unamwamini Mtume Muhamad, wewe ni mfuasi na ni mtume vilevile.

    JibuFuta
  8. ni kwamba, vitabu vyoote viliandikwa. baadhi ya maandishi kwenye vitabu hivyo ni ndoto, matamanio, matarajio, furaha, mitizamo na ubinafsi.

    ukisoma vizuri utaona ujinga mwingi kuliko akili au busara. anyway tafsiri ndio muhimu kwani jinsi unavyotafisiri ndivyo inavyokuwa.

    wale wanaofuata vitabu 'vitakatifu' mna hali ngumu kwani baadhi ya mafundisho kama ya Yesu (mfano) sio halisi katika vitabu. baadhi ya waanzilishi wanaongelea 'experiences' za kukua kiroho au kile walichokiona katika meditations japo sisi tunazungumzia hisia. 'experiences' za 'higher' regions haziwezi kuzungumzika zikaeleweka wala kundikwa zisipoteze maana kwani huwa ni pana kiasi kwamba hazienei kwenye maandiko na hivyo mpaka ziandikwe huwa zinapunguzwa uhalisia wake mpaka mtu afanye na ku-experience mwenye na sio kutumia akili bali roho na sio kuamini bali kuona.

    hii ni moja wapo ya upugufu katika vitabu viitwavyo vitakatifu na ndio maana ukivisoma kwa makini unakuwa na kupanda daraja na kuuona ukweli mkuu.

    JibuFuta
  9. DUH swala lanikunisha kichwa tu hili!:-(

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia