Uislam: Ndoa na mali havihusiani?

Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa.

Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja.

Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho.

Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake.

Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini.

Kwa nini?

Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka?

Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?

Maoni

  1. Nautiakasi18/7/09 4:04 PM

    Wewe ndo mwenye mtatizo..! Kwa mafundisho ya kiislam wanaume na wanawake wote wana haki na wajibu wa kutafuta mali, elimu n.k, kabla ya ndoa na wakiwa ndani ya ndoa! Sasa unaposema eti uislam unamkandamiza mwanamke sababu mwanaume anatafuta mali kabla hajaowa, sikuelewi unaongea nini kwani yeye mwanamke alikatazwa kutafuta mali kabla hajaolewa, au unaposema wanaume ndio hutafuta mali wakati wakiwa ndani ya ndoa, aah kwani mwanamke alieolewa amekatazwa kutafuta mali??? Sasa tatizo lipo wapi? Huo ndo usawa ambao wanawake wanaulilia leo uislam ulishaweka usawa huo miaka zaidi ya 2000 iliyopita! Nyinyi wakristo ndo mnaowanyang'anya usawa sababu mnawataka wanawake wawe tegemezi kwa waume zao! Na mnawajengea uwezo wa kutokujiamini. Sababu unapomwambia mtu ukiolewa mali zote za mumeo ni zenu, tayari umeshamjengea mazingira ya utegemezi. Uislam ni dini ya HAKI na USAWA wa ukweli, umetoa nafasi na fursa kwa wote (mke na mume)kutumia vipawa vyao walivyojaaliwa na Mungu kutafuta mali kwa njia za halali! Kwa hiyo acha kushabikia kijinga jinga kwa chuki zako binafsi zidi ya uislam, ukajenga hoja za kidini dini, bila kutumia akili! Kwa kukuongezea uisla umeruhusu talaka, sababu Allah amewaumba binaadamu wote wakiwa huru, hawi mtumwa mume kwa mke au mke kwa mume, kwa hiyo kila mmoja anao uhuru wa kuamuwa kuendelea na uhusiano (ndoa) au la, huo ndo uhuru katika maamuzi, ambao nyi nyi wakristo mmemnyang'anya mwanamke, kwa kumfanya mtumwa wa mwanaume, hata kama atakuwa ananyanyasika katika ndoa, au anateseka au ananyimwa haki zaki za msingi mnamlazimisha aendelee na ndo, Jee huo si utumwa??? Think tiwce! Acha ushabiki wakipumbavu! UISLAM NI DINI YA HAKI (hakuna aliezuiwa kujitaftia elimu na mali) Usilam ni dini inayompa kila mwanadamu UHURU wa kufanya maamuzi katika mahusiano (unadai au unatoa talaka unapoona ndoa haikutendei haki)
    ACHA CHUKI ZIDI YA UISLAM!

    JibuFuta
  2. Ndugu msomaji wangu,

    Nadhani ingekuwa vema tukijadili bila jazba. Nimetoa maoni yangu, na wewe unaleta ya kwako na mwingine analeta ya kwake, ndio mambo ya mjadala hayo.

    Nimezisoma hoja zako, na kimsingi naheshimu sana maoni ya wasomaji kama wewe. Nitayaweka ukurasa wa mbele kwa ajili ya mjadala zaidi.

    Kwa sasa nitafurahi ukinielewa kuwa sina chuki na wala sina sababu ya kuwa na chuki na Uislamu wala dini yoyote niliyowahi kuijadili.

    JibuFuta
  3. Nautiakasi18/7/09 9:18 PM

    Ndugu mwenyekiti...hapana acha nikuite jina lako tu CHRTISTIAN...! as your name suggests sitegemii kupata positive responce juu ya uislam na uislam kutoka kwako! Niliyo yaeleza hapo juu si jazba ni UKWELI HALISI ULIO MOYONI MWAKO (watoto wa mjini wanasema ni nyeupe bila chenga) naweza kuisimamia kauli yangu hii popote(kwamba wewe umeitoa mada hii ukisukumwa na kuongozwa na chuki zidi ya uislam na waislam). Nna hakika juu ya hili kwani Allaha ameshatwambia katika Qur-an kwamba mnayoyaficha ni makubwa kuliko mnayoyadhihirsha (chuki zidi ya uislam)...! Inaonesha muda mrefu ulikuwa unatafuta wapi pakuanzia kuonesha chuki zako, lakini huwezi kupata uzaifu ndani ya mafundisho sahihi ya uislam (utapata kwa wanaojiita waislam sababu wengi hawafuati wanayofundishwa), huwezi kujenga hoja yenye mashiko zidi ya uislam, sababu alieileta dini hii ndie alieumba kila kila kitu, ndie mjuzi wa kujenga hoja, ndie anaejuwa ubora na uzaifu wa mwanaadamu, ndie anaejuwa haki na usawa, ndie mjuzi wa wajuzi, ni m'bora wa waliobora, na yeye ndo mwenye kumiliki vyote vya mbinguni na ardhini na vilivyoko baina ya mbingu na ardhi na kule tusikokujuwa wanaadamu (kwa akili zenu chache alaizotujaalia yeye)! ...Allaha ataitimiza nuru yake, hata kama washirikina na makafir watachukia.." (Allah)

    JibuFuta
  4. Bwana Nautiakasi (sina hakika kama ni bwana ama bibi) jazba haisaidii lolote zaidi ya kuthibitisha uelewa mdogo.
    Nikusahihishe historia. Uislamu haukuwapo miaka 2000 nyuma kama usemavyo kwa jazba. Tazama hata kalenda ya Kiislamu utajua hivyo.
    Pia unasahau kuwa sheria za Kiislamu (¿sharia) ndizo zinazomkandamiza zaidi mwanamke pengine kuliko sheria zingine zozote. Ila kwa kuwa unatawaliza na jazba, utajibu mapigo kwa jazba.
    Wakristo wanawapa nafasi wanawake katika jamii. Inathibitishwa na uwepo wa ndoa ya mke mmoja, Uislam je?
    Marufuku ya talaka, Uislam je?

    Kwa kuwa jina lako halielezi dini yako ni ipi, kama ulivyomshushua bwana Christian kwa kulihukumu jina, nina wasiwasi hata huo Uislam ni wa kubashiabashia hata kushindwa kuifahamu historia ya dini yako.

    Tunapaswa kujifunza kuheshimu dini za wenzetu.

    JibuFuta
  5. Wow!!
    Ntanena kwa maoni ya kwanza ya NAUTIKASI. Kama nilivyowahi kusema, najikita zaidi kwenye "point of view" kuliko "sound tone".
    Naona katika maoni hayo kuna mengi ambayo nimejifunza na naamini nitaendelea kujifunza mengi zaidi. Kwa ujumla kuna mengi ambayo hayawekwi bayana kwa watu wa upande wa pili wa imani na hata wale wenye dini za asili. Lakini mengi ya hayo ni yale yanayoweza kuboresha maisha yetu hata kama tunaishi tukiamini kwingine.
    Natamani kama Nautikasi angeandika kuhusu MAFUNDISHO YA MAISHA anayojifunza (kwa manufaa ya kuwakumbusha walio na imani kama yake na wenye imani tofauti) kwa kuwa nimeshajifunza mengi yanayofundishwa na dini ambayo yanakosekana kwenye maisha ya sasa na ndio chanzo cha mikanganyiko tunayoipitia ulimwenguni. Ulimwengu wa sasa hatuhimizi kusamehe, kuthamini, kupenda na hata kuheshimu. Na haya yote yanaweza kuwa kianzio cha mabadiliko ya maisha yetu hapa ulimwenguni kama watu wataelewa kwa undani ni vipi maisha yanafunzwa katika jamii tusiyoshiriki ama kufuata mfumo wao wa kuabudu.
    Hapa nimejifunza mengi sana kuongezea katika yale niliyojifunza kwenye kitabu cha Prof Mbele cha ku-embrace cultural difference.
    Asanteni nyote (Kaka Bwaya na Ndg Nautikasi) na baraka kwenu nyote.
    Pamoja tuendelee kufunzana na kujengana
    Blessings

    JibuFuta
  6. Nautiakasi19/7/09 4:08 AM

    Mkristo kama unavyojiira wewe ndo hujui historia ya uislam...kwa kukusaidia tu kalenda inayotumiwa na waislam hivi sasa haihusiani na kuanza kwa uislam, inahusiana na tukio la kihistoria la waislam kuhama kutoka makka kwenda madina (hajra)! Bimaana katika uislam hiyo kalenda ina reflect tukio hilo, kunazia muda huo ndo waislam wakawa wanakalenda yao, LAKINI Uislam umeanza tangu wakati wa binaadamu wa kwanza ambae ni nabii ADAM hiyo ndo hostoria sahihi ya uislam, Allah anasema uislam ndio mila ya ibrahim, yakob, issa (wewe unamwita yesu) na ndio mila ya muhammad, yoyote atakeishi kinyume na mila ya baba yenu ibrahim atakuwa mwenye kuangamia! Kwa hiyo uislam upo tangu mwanzo wa maisha ya mwanaadamu. Kuhusu hoja yako kwamba uislam unawakandamiza wanawake naona umeongea kiujumla sana kiasi kwamba naweza kukuita mpayukaji! Uislam umeruhusu mwanamme aowe wake mpaka wanne kwa masharti ya kuwa na uwezo wa kuwatunza na kuwa muadilifu kama hawezi awe na mmoja tu, hayo ndo mafundisho, ni bora hao waislam wanaoowa wake wawili au watatu au let us say wanne, lakini jamii inajuwa na watoto wanazaliwa na kulelewa wakiwajuwa wazazi wao na jamii ikiwatambua, lakini nyinyi wakristo mnajidai kukataza wake zaidi ya mmoja wakati huo huo, mnakuwa na vimada zaidi ya 5, mwisho mnaishia kuzaa watoto wengi wa nje amabo wanageuka kuwa kero (watoto wa mitaani) sababu jamii haiwatambui kama baba ndie mzazi, zaidi ya hapo mnatia kichefu chefu kwa kulazimisha kuishi maisha ya kinadharia wakati yanapingana na asili ya mwanaadamu, unapomwambia mwanaume aliekamili asiowe (faza)mwanamke aliekamili asiolewe (watawa)! Hivi hii inaingia akilini???
    Rejea historia ya ukristo ndo utajuwa kwamba wao ndo wakwanza kumfanya mwanmke kuwa matangazo ya biashara na kuwa chombo cha starehe cha mwaname!
    Mkristo uislam umekamilika sababu si dini ya kutengenezwa na kikundi cha watu ambao wanamapungufu hii ni DINI toka kwa mjuzi wa wajuzi, m'bora wa walio bora, mfalme wa wafalme nae ni Allah ametakasika! yeye asie lala, wala kusahau, asiepatwa na dhara ya aina yoyote, yeye ayajuwaye ya siri na dhairi na yaliyofichikana zaidi ya siri!Allah akujaalie siku moja uione haki! Yote yanawezekana kwa yeye atutiaye nguvu!

    JibuFuta
  7. Bado huna hoja Nautiakasi. Huna hoja kwa sababu hata tuhuma zako kwa wakristo ni hearsays.
    Lakini ushahidi upo wazi kuwa ninyi mwawakandamiza wanawake. Kuruhusu mtu mmoja kuwa na wake wanne, ni kumgeuza mwanamke kuwa chombo.
    Lakini si kweli kuwa watoto wa mitaani wametokana na wakristo wenye vimada. Labda uniambie hivyo kwa tafiti ipi yenye kujibu kwa muktadha halisi.
    Sheria za kikristo hazimkandamizi mwanamke, tofauti na ninyi mnaomhukumu mwanamke mzinzi pasipo kumhukumu mwanaume aliyezini naye.
    Tazama hata siasa za Tanzania, mijadala ya mahakama ya kadhi, OIC na mafuta za Zanzibar. Vyote vinaongozwa wazi na fikra za udini na ubinafsi wa kiislam.
    Mfano halisi, ni waislam kusema kuwa wanaopinga mahakama ya kadhi na OIC watasomewa albadiri.
    Hiyo ni ishara dhahiri ya dini yenu isivyo staarabika na kukosa uvumilivu kwa imani za wengine.
    Kama kawaida ya waislamu, na hili utalijibu kwa jazba. Sitostaajabu kwani ndivyo mlivyo na itakuwa vigumu kubadilika.

    JibuFuta
  8. fred katawa19/7/09 10:10 AM

    Hongera Bwaya kuleta hii mada imenifunza mengi kuliko nilivyotarajia.

    Wakati fulan tunpojadili masuala ya imani hasa za dini,tujaribu kuweka imani zetu pembeni na kuangalia uhalisia wa mada husika.

    Nautiakasi na Mkristo wanatetea imani zao pengine bila kuangalia uhalisia wa mada husika.

    Uislamu na Ukristo dini zote zaweza kuwa zinadai kuwa haziwanyanyasi wanawake lakini tunashuhudia wakristo na waislamu wakiwanyanyasa wanawake.

    Suala la unyanyasaji wa wanawake lipo ktk iman za din nyingi.Ukisoma amri kumi za Mungu ktk Biblia waweza kugundua kuwa ziliandikwa na wanaume na hazionyeshi kuwa mwanamke ana haki sawa na mwanaume.

    Nashauri tusome vitabu vya dini kama vitabu vingine na sio kujichukulia kuwa sisi ni sehemu ya vitabu hivyo.
    Amani kwenu nyote

    JibuFuta
  9. Msomaji wangu hunitendei haki kuniamulia msimamo wangu kwa kutazama jina nililopewa na wazazi wangu.

    Ninaweza kuwa Mkristo lakini si mara moja nimeandika kuhoji baadhi ya mambo katika Ukristo (soma kwenye maktaba mwaka 2006 na 2007). Wakristo hawakujibu kwa jazba.

    Labda ili turudi kwenye hoja nikuulize: Usawa unaotetewa na dini yako uko wapi kama mwanamke haruhusiwi kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja?

    Nipatapo fursa nitapandisha hoja zilizotokana na maoni yako na yale ya msomaji wangu anayejiita mkristo.

    JibuFuta
  10. Nautiakasi19/7/09 4:59 PM

    Mkristo
    1.Hukumu kwa wazinzi katika uislam,ni wanawake na wanaume wote wanaangaliwa na sharia kwa usawa, bimaana mzinzi mwanamke na mzinzi mwanaume wote wanapata hukumu sawa, kama mwanamme hajaowa au kama mwanamke ni mwanamke hajaolewa wote wakithibitika kuzini wanachapwa viboko 100.
    Na kama wote wapo kwenye ndoa zao, basi wote wanapigwa mawe mpaka kufa! Sheria zote katika uislam ziko sawa kwa jinsia zote.
    2.Kuhusu talaka, nlishakueleza kwenye comment yangu ya kwanza (isome tena)

    3. Kuhusu hayo mambo ya albadir, hapo itakuwa nawazungumzia waislam si uislam, si kila muislam anafuata uislam kwa usahihi, kama ilivyo si kila mkristo anafuata ukristo. Huwa siwezi kuongelea matendo ya mtu au watu au kikundi cha watu, najikita zaidi kwenye mafundisho sahihi ya kundi la hao watu au mtu! Lakini kwa kuelewesha tu albadiri ni neno tu linalo "symbolize" dua (au tuseme mashtaka) ya kikundi cha watu au mtu kwa muumba wao, sasa hao unaodai wanasoma albadiri ni kuwa wanataka kumshtakia muumba wao juu ya hiyo kazia wanayoipata kwenye kudai haki yao (sina hakika na hadihti yako lakini kama ni hivyo ndo hivyo)! Au waona njia ipi bora kumshtakia Mungu, mungu akafanya analoona sawa au kuingia mitaani wenyewe wakadai haki yao? Jibu unalo kwa kichwa!

    Ndugu CHRTISTIAN, kabla sijajibu swali lako, naomba nikuulize namie swali. Mathali ingekuwa hivyo unavyotaka (mwenyewe waita usawa) mwanamke aolewe na wanaume zaidi ya mmoja (let us say 4), halafu akapata mimba hivi mtoto atakuwa wa nani? (Utatoa jibu rahisi kwamba tufanye DNA test, lakini kumbuka maisha yalikuepo kabla ya DNA test kujulikana, na yapo hata kwa wale wasiojuwa na wasiofikiwa na hizo DNA test)!
    Sasa ukiwa unaona ugumu wa jibu hilo, Allah ndie alieumba mke na mume, ndie alileta uislam anajuwa hata yale tusioyajuwa, pengine alishaona hilo (ingawa sio sababu rasmi)Allah anajuwa mengi zaidi ya hilo. Ila utata huu kwa wanaume hakuna, hata aowe wake 4 mtoto wake atakuwa wake tu!
    Kimantiki upo uwezekano mkulima mmoja kulima mashamba manne peke yake atavuna chake peke yake hakuna utata hapo, lakini shamba moja kulimwa na wakulima wanne mbegu zaina moja, kwakweli wakati wa mavuno hatuwezi juwa yamkulima ipi ndio ilichepuwa na ya yupi ndio ilikufa, hapa lazima kuna kuzulumiana tu, na uislam si dini ya zulma, ni dini ya haki na usawa. Hilo ni jibu la ki logic zaidi kama unaweza kuhangaisha ubongo wako kidogo tu, hakuhitaji kuwa na elimu ya chuo kikuu!

    Halafu swali lako nila kitot sana, pengine ulipouliza ulikuwa ndo hivyo unaongozwa na utashi wa chuki zidi ya uislam na si hekima zako nnazo zijuwa bwana bwaya, sasa mwanamke aolewe na waume zaidi ya mmoja hivi huyu mwanamke unamtakia usawa au unamtakia matatizo, hivi ulishakaa ukatafakari japo dakika 2 kabla hujabonyeza key board kuuliza. Mathali wewe Christian ndo ungekuwa Christina then unaolewa na waume wa nne (marijali kweli) kila siku una zamu kwa kila mwanaume, hivi baada ya mwaka ungekuwa mwanamke wa aina gani? Ha ha ha I cant imagine. Bwana we alieweka hizi sheria anamjuwa mwanamke nje ndani (sababu ndie aliemuumba), amemuhifadhi na kumlinda mwanamke, ingawa kwa wasiotumia akili zao kama wewe wanaona usawa ni kila kitu kufanya sawa,sio kanuni hiyo kila mahali, kwa mfano hata kueka jiwe kwenye mguu mmoja wa meza na kwengine usiweke kitu lakini meza ikatulia pia ni usawa, silazima huku ukiweka jiwe na basi na miguu yote ya meza uweke jiwe chini! Bwaya ndugu yangu vipi?

    JibuFuta
  11. Nuru Shabani20/7/09 9:04 AM

    Kamala uko wapi?Tunakungoja.
    Asante Bwaya kwa kutupa darasa manake tumejifunza.

    JibuFuta
  12. booonge la mjadala. ukitaka kujua ni kwa kiasi gani watanzania hawana vipaumbele na wanaongozwa kwa hisia na silika zaidi, basi wewe gusia mambo ya kibubusa a.k.a dogma au amri kutoka kwa wakoloni wetu a.k.a dini! ndipo utajua mambo meengi juu ya hisia kutawala. hii inajidhibitisha bungeni juu ya OIC na mahakama ya kadhi, wabunge hugawanyika sio kivyama tena bali kidini na mkristo hupinga huku mwisilamuakidai kwa nguvu zote utadhani dini hizi zina 'jema' lolote zilizotutendea tangu kuja kwake hapa Afrika. linganisha maisha yetu ya kabla ya ujio wa dini hizi na baada.

    sasa bwaya unasema uisilamu ndo hivyo, je ni kweli ukristo haumkandamizi mwanamke?

    na bwana Nautiakasi, unadhani uisilamu na ukristo vina tofauti yoyote ya msingi kwamba kuna aliyeko juu ya mwingine? siamini hivyo. maswala ya kiroho yakiangaliwa kiakili na 'kiintellectual' ni noma ila ya kiangaliwa kiroho au kwa kutumia 'science of the soul' basi yanaeleweka na kuondoa ubishi wa kiakili na kihisia.

    je mwanamke anasemaje juuya kunyanyaswa? bahati mbaya sisi hatuna dini na hatukuchagua dini zaidi ya kuchaguliwa na nimelisema sana hili. ni vigumu kwa mtu yeyote kuwa jasiri na kuachana na dini za kigeni, achilia mbali kuiona kweli nayo kweli ikamfanya kuwa huru.

    kuna umiliki wa watoto hapa, nani kasema tunamiliki watoto? watoto wetu ni matokeo ya matamanio yetu na hivyo wao huja duniani kwa mikabala yao na sisi hatuna hata hatimiliki kwao na ndiyio maana tunakufa na kuwaacha. wao ni viumbe tu sasa mtoto atakuwaje wa mwanamke au mwanamume? ndo yale ya kumlazimisha mtoto kuishi unavyotaka wewe badala ya anavyotaka yeye ikiwemo kumchagulia masomo na dini.

    sasa je, mwanamke ananyanyaswaje na dini? lakini dunia hii maisha ya mwili yasiyomjua Mungu kiroho ila tunamjua kihisia, kimavazi na kiakili, ni wapi au ni nani asiyekandamizika na kunyanyasika?

    je sisi tunaweza vipi kumpatia mwanamke ahueni hiyo? sio kwamba tunajidanganya tu? si mambo ya miili tu haya? kwani mali za ndoa na zisizo ni nini? mali za dunia hii humpatia ridhiko gani mwanadamu la kweli zaidi ya kuwa mzigo na laana kwake? je ni kitu gani tutaondoka nacho? nani alikuja na mali duniani? si hata ukinyanganywa zote utapata nyingine na labda nzuri zaidi?kwani tulikuja na nini duniani? tunahitaji kumiliki kitu kikubwa hapa duniani zaidi ya dini na mali, na kitu hicho ni sisi wenyewe. hapo ndipo mambo yatakapoeleweka.

    kwa wanaoshambulia na kutetea uisilamu, twambie uisilamu nini na mwisilamu ni nani ili tupate pa kuanzia vizuri. ni vyema kuzisoma dini zoote na kuzielewa badala ya kug'ang'ania chachetu! hatuhitaji sana kutetea dini kama kuzihishi na sio kuzihishi kwa nje tu bali ndani.

    mimi kama Mhaya, naona mwanamke anaweza kunyanyasika kwa sababu ya kuzarau mila zetu na kutukuza za wengine. Hata hivyo msimamo wangu ni kwamba mwanamke ni kiumbe muhimu sana kuliko mwanaume ndio maana anakuwa mpole na kuacha mtende mtakavyo kwa upole wake ndio ahueni yetu. uanaume wetu unajidhiirisha ndani ya mwanamke na sio vinginevyo!

    ndo hayo tu kwa leo. samahani kwa kuchelwa kuchangia, mjadala niliuona zaman ila sema ndo hivyo biiiiiiize kama nakandia dini za wenzangu vile

    JibuFuta
  13. habari kaka Bwaya!mdada nasema huyo kaka hajakuelewa nahisi ni wale wanaokuwa kwenye mihadhara ya kiislam maana mh jazba du!anaongelea vimada wakati hiyo ni mojawapo ya dhambi au halijui hilo kwa hiyo waislam wanaoa wake wengi kuepusha vimada au? tena wenye shule zao ndio unakuta ana mke mmoja wengine mh wake wanne ambao wamebobea madrasa. Sorrrrrrrry

    JibuFuta
  14. mmh! nimeshusha pumzi. lakini ukweli ni kitu cha msingi sana pasipo kujali tumezaliwa na familia zilizorithi dini zipi na hatimaye nasi kuzirithi dini hizo.

    JibuFuta
  15. Ukisoma maoni ya jamaa utaelewa inakuwaje maswala ya kiislamu siku hizi yanajadiliwa na serikali.Utadhani ina nia njeeema kumbe ilikuwa inacheza na akili za kiwango cha natiakasi.Pinda kawapiga chenga ya mwili saivi wamsahau kadhi na OIC mpaka 2012. Haha haha ama kweli kazi ipo

    JibuFuta
  16. Try to bolt from the blue a smack of dullness away from provisions cook with adipose greater explanation [url=http://onlineviagrapill.com]buy viagra[/url]. Fall sense someone the royal motion to own you affable of quick-wittedness that you are in comestible healthiness [url=http://ambiendrug.com]buy ambien[/url]. Conference up gloominess pine syndrome [url=http://virb.com/symbalta]flagyl[/url]

    JibuFuta
  17. viagra online without prescription viagra dosage dogs - online pharmacy sells viagra

    JibuFuta
  18. buy tramadol online tramadol to get high - can tramadol for dogs be crushed

    JibuFuta
  19. buy tramadol tramadol 50 mg abuse - buy tramadol cod next day delivery

    JibuFuta
  20. generic cialis buy cialis no prescription australia - best price cialis 20mg

    JibuFuta
  21. buy tramadol no prescription overnight legal buy tramadol online us - ultram tramadol hci tablets

    JibuFuta
  22. generic tramadol online tramadol take get high - tramadol withdrawal bloating

    JibuFuta
  23. xanax online pictures generic 2mg xanax - xanax side effects in dogs

    JibuFuta
  24. cheapest xanax long term effects xanax xr - xanax online pharmacy

    JibuFuta
  25. generic xanax generic xanax no imprint - xanax sleeping pill side effects

    JibuFuta
  26. buy tramadol without a script tramadol addiction 2010 - tramadol 50 overdose

    JibuFuta
  27. carisoprodol 350 mg carisoprodol soma side effects - generic drug carisoprodol

    JibuFuta
  28. xanax online suboxone xanax and alcohol - generic xanax pill colors

    JibuFuta
  29. buy cialis online buy cialis 2.5 mg - buy cialis levitra

    JibuFuta
  30. http://buytramadolonlinecool.com/#30807 cheaptramadolonline - tramadol purchase online usa

    JibuFuta
  31. buy klonopin online klonopin nursing implications - klonopin wafers roche

    JibuFuta
  32. buy tramadol tramadol 50mg tablets uses - can i order tramadol online legally

    JibuFuta
  33. http://landvoicelearning.com/#97734 tramadol 50 mg ratiopharm - generic tramadol no prescription

    JibuFuta
  34. tramadol 100 discount pet medications tramadol - tramadol ultram dosage

    JibuFuta
  35. http://buytramadolonlinecool.com/#30807 tramadol 50 mg white pill - tramadol hcl 75mg

    JibuFuta
  36. order carisoprodol where to buy carisoprodol online - carisoprodol side effects withdrawal

    JibuFuta
  37. Ningewashauri wote mnaochangia hasa katika mijadala ya dini.
    kuna wanaoingiza mada ili kudhalilisha dini ingine hali ya kuwa ya kwake haijui vizuri.
    kuna wanaochangia mada wakisukumwa na jazba na wengine wanasukumwa na dini.
    Mathalani katika mada hiyo sitegemei Mkristo yeyote akaitetea mada hiyo wa sitegemei Muislam yeyote asiitetee mada hiyo. hivyo nishauri kuna mambo mengi ya msingi yanayounganisha nchi yetu na wananchi wote wakiwemo wakristo, waislam, wahindu, wapagani na wa dini zingine. mada ya ardhi, Migogoro ya Kisiasa n.k ndio vitu vya msingi wakatai huu wa kuelekea katika uchaguzi na kura za maoni ya Katiba.
    inatosha kwa leo

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Kama sio utumwa ni nini hiki?