Michael Jackson na athari za malezi

Si muda mrefu nilikuwa nikitazama ibada ya maziko ya Michael Jackson.

Kwa wengi, Michael ni alama ya watu wasiojikubali. Wengi wanamlaumu kwa uamuzi wake wa kujifanyia marekebisho sura yake. Wengine wakamwita 'Wacko' yaani chizi.

Kama umefuatilia historia ya uhusiano wake na wazazi wake utabashiri nini kilikuwa chanzo cha yote hayo.

Uhusiano wake na baba yake haukuwa mzuri. Mzee si tu kwamba alikuwa mkali sana, lakini pia alikejeli maumbile ya mwanae huyo. Nadhani yapo zaidi ya haya yasiyosemwa wazi. Maana fikiria hata wosia aliouacha Michael umeonya kuwa wazazi wake wasihusishwe na mirathi. Hata katika maziko, wazazi hawakuongea!

Inasemwa, wakati Michael anaanza kujikwatua, mzee alimwonya sana pasipo mafanikio.

Kisiki kwa wazazi wengi: Wanadhani kumwonya mtoto msiyehusiana nae kwa karibu, mtoto aliyekufuta akini mwake, kunasaidia...!

Mzazi usifanye kosa la Mzee Joseph Jackson.

Maoni

  1. Habari kaka Bwaya!Mdada nasema ni kweli kabisa MJ hakujikubali alivyo mpaka kufikia hatua ya kujibadilisha,wenzetu wazazi huko nje hawaplay pati kubwa katika makuaji yao kama sisi kwetu hata kama umeoa bado mzazi anakuwa karibu na wewe.Kwa hilo asilaumiwe sana mzazi ni yeye mwenyewe kumkosoa Mungu kuwa sikupenda uniumbe hivi nilitaka niwe hivi tena wapo wengi sana kama hao huku kwetu kama wanaojibadili rangi tunaita kujichubua nawaona kama MJ tu na wao maana unamkosoa Mungu kuwa hukuhitaji mkuwa mweusi ulitaka kuwa mzungu mfano mwingine ni mashoga hawa wanaobadili jinsia nao pia wamo kwenye hilo kundi ni kujikana huko kote,makundi haya yote wakulaumiwa si mzazi hili swala tuliangalie kwa unandani zaidi jamani tunakoelekea siko.

    JibuFuta
  2. Mdada,

    Kujichubua si jambo njema. Ni kitendo chenye madhara mengi yasiyo na sababu.

    Kwa bahati mbaya sana, kitendo hiki ni matokeo ya kiwango hafifu cha kujifahamu mtu mwenyewe.

    Tunachojaribu kukifanya ni kudodosa chanzo hasa cha tatizo. Kwamba malezi yasiyolenga kumjenga mtoto kisaikolojia yanaweza kuwa chanzo.

    Lakini mdada, wewe hujatengeneza nywele zako?

    JibuFuta
  3. La hasha ntakuwa nilitoka nje ya mada kabisa japo mimi ni rasta

    JibuFuta
  4. Mungu Hakutupa magari, Wala nyumba, wala simu, wala viatu,na kadha wa kadha, je tunafanya makosa kuviunda vitu hivi na kuvitumia?
    Mungu hakukosea kutupa utashi(ishara ya kwamba vipo vingi ambavyo hakuviweka wazi, ila kwa utashi alituachia tuimalizie kazi ya uumbaji)

    La msingi hapa ni kwamba yatupasa kufanya lolote tuwezalo ilimradi tu haliondoi na wala haliharibu utu na thamani ya binadamu yeyote yule.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!