Zijue changamoto zinazowakabili wanao

Watoto wa sasa wanakulia katikati ya shinikizo gumu la kimaamuzi. Taarifa zilizozagaa, na zinazopatikana kirahisi ni upotoshaji. Magazeti mengi yananadi ngono na mienendo mingine ambayo kama mzazi usingependa mwanao aiige. Vipindi vya televisheni vinajaribu kuonyesha kana kwamba kusalitiana ni jambo la kawaida.

Watoto wanakua wakijua ngono inafanywa na yeyote kwa wakati wowote ule.

Niliwahi kusoma ushauri aliopewa kijana mmoja aliyekuwa akilalamika kujisikia hukumu kila anapofanya ngono na rafiki yake. Yule 'mshauri' akamjibu 'usijisikie hukumu...ifurahie.' (Na bado tunajiuliza kwanini watoto wengi wanapata mimba siku hizi?)

Wakati huo wewe mzazi uko bize na kutafuta hela. Huna mazungumzo ya maana na mwanao. Unashauri kwa ukali na kwa kuchelewa.

Sasa kama wewe huongei, na wapo wanaoongea kwa sauti, unadhani upande upi utashinda? Wa kwako?

Zijue changamoto walizonazo wanao.

Maoni

  1. Ahsante kaka Bwaya.

    Wakati mwingine wazazi hawazungumzi na watoto kwa sababu ya kutingwa kutafuta pesa. Wakati mwingine ni kwa sababu wazazi hao wamekuwa mafataki. Dhamira zao zinawasuta. Wanaona haya kutoa maonyo tena.
    Tutafanyaje?
    Kila mahali ni ushawishi tu. Watoto na wadogo zetu wanakutana kila mahali na matangazo yanayowachochea kuhamasika.
    Fikiria dunia ya sasa. Mwanafunzi kuwa na mpenzi anaona jambo la kawaida.
    Mwaka jana mwezi Machi nilikuwa mahali nikipoza koo na kinywaji, pembeni yangu kulikuwa na binti watatu wa shule ya msingi. Walikuwa wakimpa ushauri mwenzao aliyemfuma mpenzi wake (pengine fataki) na msichana mwingine siku ya jana yake.
    Ushauri waliokuwa wakimpa na maongezi yote ilikuwa ni upuuzi mtupu.
    Kizazi hiki na vijavyo ni balaa tupu.
    Ni hayo tu.

    JibuFuta
  2. Mtanga,

    nakubaliana wewe. Malezi kwa kipindi hiki ambapo taarifa nyingi potofu ziko hadharani yana changamoto kubwa.

    Ikiwa wazazi watazitambua changamoto za watoto wao, na kujibidiisha kuzikabili, suala la kuwajengea watoto maamuzi sahihi kwa maisha yao litawezekana.

    JibuFuta
  3. Mtanga,

    nakubaliana wewe. Malezi kwa kipindi hiki ambapo taarifa nyingi potofu ziko hadharani yana changamoto kubwa.

    Ikiwa wazazi watazitambua changamoto za watoto wao, na kujibidiisha kuzikabili, suala la kuwajengea watoto maamuzi sahihi kwa maisha yao litawezekana.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging

Haiba ni nini?

Heri ya mwezi mpya!