Malezi yanavyochochea ubabe katika jamii
Natamani tutafakari jambo hili kwa kina. Nyumbani tumemzoesha mtoto fujo —fimbo, makofi, matusi na aina nyingine za ubabe. Sisi wazazi tunaamini hatuwezi kulinda mamlaka yetu bila kumsababishia mtoto maumivu iwe kwenye mwili wake au hisia zake. Ukiangalia yanayoendelea nyumbani hakuna mazungumzo yenye upendo na mtoto. Tunaamini amani na utulivu kwenye ngazi ya familia ni pale tunapokuwa na watoto wasiofikiri, wasiouliza, wasiothubutu kutofautiana na wazazi ambao ndio mamlaka katika familia. Shuleni mtoto anakutana na mwalimu anayeamini njia pekee na ya uhakika kulinda heshima na mamlaka yake darasani ni vitisho, fimbo na kila aina ya ubabe kwa mwanafunzi. Ukiangalia mbinu za ufundishaji wake huoni wapi anaamini katika ushirikishwaji wa mwanafunzi. Tangu asubuhi mpaka jioni zoezi linalotawala ni wanafunzi kupokea maelekezo na kuyakariri. Mwalimu anaamini nidhamu ni pale amani na utulivu vinapotawala darasani. Hii, huenda ndio sababu shule zinahangaika na wapiga...
Maoni
Chapisha Maoni