'Testi' ya namna unavyojithamini

Jipime. Jipe alama kwa uaminifu, ili kujielewa namna ulivyo.

Mwongozo:
0=Sikubali
1=Kiasi sikubali
2=Sina jibu
3=Kiasi nakubali
4=Nakubali


| Najifurahia jinsi nilivyo mf. umbo, rangi, elimu nk

| Nadhani watu wananikubali nilivyo

| Nikikosolewa ama kupingwa mawazo yangu huwa sipati shida

| Huwa naumia nisiposifiwa pale nnapohisi nastahili
kupewa sifa

| Wanavyonifaham na kuniona wengine, kwangu si muhimu

| Ninachofanya si muhimu, kama nilivyo mimi mwenyewe

| Huwa sitegemei kukosea ninapofanya jambo

| Sina hofu na mwonekano wangu mf. mavazi, sura nk

| Ninajua kuukubali uwezo na udhaifu wangu

| Ninajua kwa hakika nilivyo mtu wa pekee

Sasa jumlisha alama zote:

0-20 fanya kazi ya ziada kujithamini na kuona thamani uliyonayo ambayo huijui.

20-30 ni nzuri. Unajiamini na kujichukulia vizuri.

31-40 maana yake unajiamini kupita kiasi. kujiamini kupita kiasi ni tatizo katika kuhusiana na watu!

Maoni

  1. Habari kaka Bwaya!Jielewe kweli nimejielewa maana mdada nilikuwa naweka tu point huku naogopa je nitaangukia wapi? Asante nimejitathimini na kumbe najithamini sasa.siku njema!

    JibuFuta
  2. Nimefurahi sana nimejikuta kama nipo shule ya msingi tena. Na nimepata jibu nzuri Je ni lazima kusema nipo wapi?

    JibuFuta
  3. 31-40, he! Kumbe kujiamini kupita kiasi nako kuna madhara, hii inamaanisha kuwa mtu ktk kategori hii hajajielewa.
    Bwaya wasemaje?

    JibuFuta
  4. Yasinta matokeo yanaweza kuwa hadharani ama siri. Muhimu ni majibu yanayopatikana. Hata hivyo naamini hutasita kutujulisha matokeo.

    Mdada, safi sana. Hongera kwa kujithamini.

    Kissima, ni kweli. Kujiamini kupita kiasi huleta majigambo, nyodo na tambo zisizo halisi. Kwa hivyo, ni rahisi kuhitimisha kuwa huko ni kutokujitambua!

    JibuFuta
  5. Kaka Bwaya nimepata jambo jingine hapa.Nafikiri kujiamini ni kujiamini tu, hakuna kujiamini kupita kiasi.Kwani majigambo, nyodo,kujionyesha kuwa ni zaidi n.k hazi zote naziona ni defence mechanisms tu, mtu wa aina hii hana kule kujiamini hivyo anajaribu kuleta kujiamini kupitia mambo niliyoyataja hapo juu. Ni mtazamo tu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia