Bila upendo, usihangaike kuonya!

Kuna watoto hawajawahi kujua kupendwa kukoje. Tunazungumzia watoto wenye wazazi.

Watoto wanavalishwa. Wanalishwa. Wanasoma shule za 'watakatifu.' Lakini hawajawahi kujihisi kupendwa!


Wazazi wanazo pesa, lakini si mapenzi kwao. Wazazi wanapendana wao (chumbani of coz), lakini hawaonyeshi mapenzi ya kweli kwa watoto wao.

Na ni bahati mbaya ilioje kuwa kila mtu anahitaji kupendwa. Athari za kutokupendwa ni mbaya.

Watoto wasiopendwa, ni vigumu kujielewa. Ni vigumu kujiamini.
Ni vigumu kusikiliza na kushaurika. Ni wakaidi. Wagomvi.

Watoto wasioujua upendo wa wazazi, huutafuta upendo huo kwa marafiki, ambao nao pia hawaujui upendo.
Ni rahisi kudanganyika. Ni rahisi kuangukia mikononi mwa 'mafataki'. Kile tunachokiona kwenye tangazo la TAMWA kwamba 'sidanganyiki', bila upendo wa wazazi, ni ndoto.


Kama unatumia muda mwingi kuonya wanao bila kuwaonyesha upendo, bado una kazi ya kufanya.

Maoni

  1. hii mada imenitouch sana umeandika kwa ufupi lakini point imeeleweka..,unachokisema ni kweli tena sanaa..upendo ni kitu muhimu sana especially kwa mtoto na kwa kila binadamu period..,well spoken kaka

    JibuFuta
  2. labda ni vyema kukosa msosi ukapata upendo

    JibuFuta
  3. Nimenukuu kwa vile nimeipenda mistari huu ni muhimu sana. "Watoto wasiopendwa, ni vigumu kujielewa. Ni vigumu kujiamini.
    Ni vigumu kusikiliza na kushaurika. Ni wakaidi. Wagomvi."

    Ni kweli upendo ni muhimu kwani mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!