Global Voices: Dunia inaongea, unasikiliza?



Nimeamua kukata shauri na kujiunga na Jamii ya wanablogu wa Global Voices katika ukurasa wa Kiswahili. Ninajitolea kuusogeza ujumbe karibu na wasomaji wa kiswahili kwa kutafsiri makala zinazoandikwa na wanablogu wengine.

Global Voices kimsingi ni jamii ya wanablogu kama 200 waliopo duniani kote ambao wanafanya kazi kwa pamoja kukuletea tafsiri na ripoti za yanayojiri kwenye ulimwengu wa blogu na uandishi wa kiraia. Global voices inapaza sauti ambazo kwa kawaida huwa hazisikiki katika vyombo vya habari vya kimataifa.

Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu jamii hiyo, halafu ukaribie kuchangia maoni kwenye ukurasa huo wa Kiswahili na kubadilishana mawazo na wanablogu wengine.

Ndesanjo Macha , mtu aliyefanya kazi kubwa kutangaza teknolojia ya blogu kwa lugha ya kiswahili nchini na mmoja wa wahariri waandamizi wa Jamii hiyo, alikuwa na na haya ya kusema.

Maoni

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?