Mbona hutumii kipaji chako?

Tulidokeza awali kwamba ni makosa kujaribu kutafuta tusivyonavyo, ilhali tukiviacha tulivyonavyo vikiteketea bila taarifa.

Vipaji ni mojawapo ya vingi tulivyonavyo. Tunapozungumzia vipaji, tunaanisha uwezo asilia ambao tunazaliwa nao bila kujifunza. Na kila mtu ana kipaji hata kama hakijui.

Inasikitisha kuwa watu wengi wanatumia maisha yao hapa duniani kujaribu kubadili vipaji walivyozaliwa navyo. Wanakana uwezo wao na kukimbilia vitu dhaifu kama sifa za bure bure, heshima kwa jamii isiyojitambua, pesa na vitu kama hivyo.

Matokeo yake, wanakaanga vipaji vyao. Wanapotea njia. Wanafanya kazi zisizowapa furaha. Wanaishi maisha ya wengine. Hayo yote ni kwa kutokuvijua na kuvitumia vipaji vyao.

Kwa nini tusianzie na hapa tulipo? Kwa nini tusianzie na tulivyonavyo? Na kama tulivyonavyo ni vipaji, kwa nini tusivitumie?

Itaendelea...

Maoni

  1. Twashukuru sana kaka,
    Hili uliloandika,
    Changamoto ya hakika,
    Kazi tukaifanyia.

    JibuFuta
  2. Asante kwa kutukumbusha kwani kuna wengine tunasahau kama tuna vipaji. Ni somo nzuri

    JibuFuta
  3. Asante kaka mdada nasema ni kweli watu hatufanyii kazi vipaji au kwa jina lingine karama tulizo nazo matokeo yake taifa kwa ujumla linabaki kuchukua wataalam toka nje ya nchi kwa mambo flani flani lakini kama watu wangebobea kwenye fani zao wangetatua tatizo hili, na hata kama watafanikiwa kusomea kipaji chao kwa uzoefu wangu wengi wetu hawapendi kubaki hapa nchini kwa mfano madaktari walio wengi wapo nje ya nchi wakidai maslahi hayatoshi,uchumi wa nchi pia unasababisha hali kama hii unasomea ualimu wakati kipaji chako ni muimbaji sidhani kama utafundisha kwa moyo wanafunzi,kitu kingine sasa hivi soko la uigizaji hata wasio na kipaji wameparamia fani hii nadhani unalifahamu hili.

    JibuFuta
  4. Kama mdada alivyosema,hali ya maisha kuwa ngumu(uchumi mgumu) unachangia sana watu kutokutii matakwa ya vipaji vyao. Wakati mwingine tunalazimika kuangalia uwezekano uko wapi, ndio maana si wote ambao ni waalimu walipenda kuwa waalimu, madactari vile vile , mapolisi n.k unakuta si vipaji vyao bali mashinikizo fulani fulani yakiwemo ya ugumu wa maisha. Mtu anaweza kuambiwa asomee masomo ya uhasibu( hata kama si kipaji chake) kisa tu nafasi hiyo imeshaandaliwa mahali fulani hivyo mtu analazimika.

    Utaratibu wa elimu yetu unachangia sana watu kushindwa kutambua vipaji vyao. Ukweli ni kwamba kwa namna ya usomaji wetu, ili mtu afanikiwe ktk masomo, asilimia kubwa ya mda lazima utumike kwenye kusoma hivyo muda wa kufanya mambo mengine mbali na kusoma unakuwa mdogo.

    Binafsi naamini kwamba kama sitajihusisha na mbambo mbalimbali kulingana na mazingira niliyopo, kukitambua kipaji changu itakuwa vigumu sana.

    Walezi/wazazi wananafasi kubwa sana ya kuwaongoza watoto wao toka wakiwa wadogo ktk kuja kuviishi vipaji vyao, na hakika huo ndio muda muda muafaka kabisa.
    Kutambua kipaji chako ukubwani ni kazi ngumu sana.Ndio maana hata kuwa watu wanaombiwa kuwa wana kipaji fulani lakini ukweli ufanisi wa asifiwacho unakuta umetokana na uzoefu tu na si kipaji chake.

    Mwisho kabisa, kama inawezekana, hints za kugundua kipaji ziwekwe wazi na hili litasaidia wengi.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Pay $900? I quit blogging

Heri ya mwezi mpya!