Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2006

Hiki ni kichekesho cha MMEM!

Mwishoni mwa mwaka jana, Wizara ya elimu iliitia "kash kash" asasi isiyo ya kiserikali iitwayo HakiElimu. asasi hiyo ilikuwa na matangazo mengi katika vyombo ya Habari yakielezea kwa kina hali halisi ya elimu nchini. Msisitizo wao ulikuwa katika kumulika matokeo ya Mpango wa (Maendeleo) ya Elimu ya Msingi, yaani MMEM. Kwa wengi wetu, matangazo hayo yalikuwa yakiutoboa ukweli wa wazi mkabisa ingawa Sirikali haikuutaka. Ukweli wenyewe ni pamoja na kuwapo kwa ubadhilifu mkubwa wa fedha za Mpango uliofanywa na walimu wakuu wakishirikiana na wakubwa kinyume na malengo husika. Ushirikishwaji duni wa wananchi katika Mpango mzima lilikuwa ni tatizo lingine lilobainishwa, kutokuwapo kwa kipaumbele cha kujenga shule za wanafunzi wenye ulemavu, mbinu zisizofaa zinazotumiwa na walimu katika ufundishaji na mengine mengi. Hayo yalikuwa kweli tupu, na haikuhitaji shahada ya uzamili kuujua. HakiElimu hata hivyo, walikuwa wamefanya utafiti wa kutosha katika hilo. Sirikali kwa kutumia ngu

Kondomu na UKIMWI, wapi na wapi?

UKIMWI unatowesha maisha ya watanzania wengi kwa kasi isiyo ya kawaida. Na bahati mbaya, janga hili linaangamiza maelfu kwa maelfu ya vijana wanaopotoshwa na wazee kwamba watumie kondomu, eti kinga thabiti ya kuwalinda na UKIMWI. Vijana ambao kimsingi ni nguzo muhimu katika Taifa kwa nyanja zote. Nimesikia mijadala mbalimbali inayojaribu kuhalalisha matumizi ya kondomu. Yupo Pardi Maarufu anayepigana kufa na kupona, kupitia magezeti kuhakikisha kuwa anawaweka sawa wazinzi na washerati wote ili watumie kondomu. Sumaye na Watawala wengine, wameonyesha bidii sana katika kuangamiza jamii kwa kusisitiza matumizi ya kondomu. Kondomu ambazo zimeendeleza maambukizi ya UKIMWI kwa kasi ya kutisha. Yeye anasema anawagawia watoto wake “kinga” kila siku ili wakafanye mambo yao kwa nafasi zao. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba, hivi kondomu zimesaidia kwa kiasi gani kupunguza maambukizi ya UKIMWI? Pamoja na matangazo yaliyotanda kila kona ya miji yetu na katika vyombo vya habari,

Makala hii ingesomwa tungekuwa tulivyo?

Nimeirejea makala ifuatayo kwenye maktaba ya Mheshimiwa Ndesanjo. Kimsingi napenda uandishi wake. Nimekumbana na makala hii ambayo sina hakika kama ilisomwa na watanzania. Nasisitiza kwamba tuna kazi ya ziada kuwabadilisha wapende kusoma. Unapokuwa na jamii ya watu wanaopenda udaku inakuwa tabu. Mtoto anakua anakuta baba ni mpenzi wa magazeti ya udaku. Na yeye anakuwa mdaku hali kadhalika. Akiwa kwenye mtandao hataacha kuangalia ngono. Masuala nyeti hana muda nayo. Nina wasi wasi kama tutaweza kufikisha ujumbe wa kubadilika kwa jamii ya jinsi hii (isiyopenda maandiko). Ndio maana hata suala la elimu ya uraia limekuwa gumu, maana andiko lenyewe lenye elimu hiyo halisomwi. Tutafute mbinu ya kuwabadilisha watu wa jamii yetu ambao nadiliki kusema wanateketea. Sijaribu kusema kwamba wanabalika, lakini nadhani, kasi hairidhishi. Sijui kama tunaweza kuwakuta huko huko kwenye magezi ya udaku?

Hivi makala hizi zinasomwa kweli?

Leo nilikuwa natembea tembea nyumbani kwa Ndesanjo Macha. Nimejifunza mambo mengi nyumbani kwake. Makala nyingi zimejaa maudhui mazito ambayo kusema kweli yana nafasi kubwa katika kuibadilisha jamii ya kitanzania. Tatizo ni kuwa Watanzania wengi anaowaandikia hawana muda na makala ndefu kama zake. Wanataka makala za ngono, fupi fupi zenye masimulizi ya kimapenzi! Makala kama zake, sina hakika kama kweli zinasomwa na wengi, hasa vijana ambao kama wangezisoma zingewasaidia. Swali nililotoka nalo ni kwamba makala kama hizi zinawasaidia wanaozisoma? Hivi wanazisoma hata hivyo?