Mahusiano yenye ‘utulivu’ bila amani
Chanzo: stock.adobe.com Hivi umewahi kutaka kumwambia mtu jambo unaloona ni muhimu lakini ukakosa namna nzuri ya kumwambia?Unatamani ujumbe ufike lakini maneno sahihi ya kuubeba huna. Unafanyaje? Wengine huamua kuacha. Kuliko kumwuumiza mwenzako, huona bora mtu uugulie maumivu ndani kwa ndani. Mwingine hajali. Huamua bora ‘kutema nyongo’ hivyo hivyo bila kujali maumivu yatakayoyasababishwa na ujumbe. Wanachosahau, matokeo yanayotokana na k u jiumiza kwa kuuzuia ujumbe yanaweza kuwa sawa na madhara ya kuuachia ujumbe kiholela bila kujali maumivu ya atakayeupokea. Mawasiliano ni sayansi yenye nafasi nyeti katika mahusiano. Ukikosea kanuni, mawasiliano yana nguvu ya kuleta uharibifu mkubwa unaoweza kugharimu afya ya mahusiano. M awasiliano ni sanaa pia. Namna unavyosema jambo ni muhimu wakati mwingine kuliko hata ujumbe wenyewe. Ukishindwa kuchagua maneno sahihi na mazingira sahihi ya kusema jambo unaweza kufubaza uzito wa ujumbe wako. Thamani ya unachokisema inabebwa pia...