Mwanaume Anayejitambua Hatishwi na Mafanikio ya Mwanamke
PICHA: Ayo Martins |
Upo
ukweli usiosemwa wazi kuwa wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio. Wanawake
waliosoma, wenye mali na fedha, wenye madaraka makubwa katika jamii, wanakuwa
na mtihani mkubwa kuanzisha na kudumisha uhusiano na wanaume.
Hali
hii inachangiwa na mambo kadhaa. Kwanza, hulka ya wanaume kuwa kichwa cha familia. Ni dhahiri wanaume wengi wanapenda kujihakikishia
hadhi ya juu kuliko wanawake. Kwa mfano, mwanaume wa kawaida anatamani kujihakikishia
nafasi yake kama kiongozi wa familia kwa uwezo wake wa kumwongoza, kumwamrisha
na kumdhibiti mwanamke.
Katika
kuhakikisha kuwa hilo linawezekana mwanaume huyu hujitahidi awe na sifa za
ziada kama vile kuwa na umri mkubwa zaidi, fedha zaidi na madaraka zaidi. Haya
yote kwa pamoja yanajenga utamaduni wa kutafuta mwanamke dhaifu asiye na sifa
alizonazo yeye ili kujihakikishia madaraka zaidi.
Lakini
pili, kwa upande mwingine, baadhi ya wanawake nao wana hulka ya kupenda kupambana
na mamlaka ya wanaume. Pengine kwa kuchoka kunyanyasika na kuwa chini ya
udhibiti wa wanaume , inapotokea wanapata mafanikio kuwazidi waume zao, huanza kutishia
heshima na hadhi ya mwanaume.
Kwa
mfano, mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kifedha kuliko mumewe anaweza kuanza
kujiona hana sababu ya kumsikiliza mume wake. Fedha zinakuwa ni fursa ya ‘kujikomboa’
dhidi ya utawala wa mwanaume jambo ambalo linaweza kuwatisha wanaume.
Hata
hivyo, ni muhimu kuzingatia kuwa katika
siku za nyuma, tofauti ya kijinsia ilikuwa dhahiri. Mila na desturi za wakati
huo, kwa mfano, zilimnyima mwanamke fursa ya kujengewa uwezo sawa na mwanaume.
Katika familia nyingi, mtoto wa kiume ndiye aliyepewa upendeleo kielimu na
kijamii. Upendeleo huo ulimwezesha mtoto wa kiume kuwa na nafasi nzuri ya
kupata mafanikio zaidi ya mwanamke. Katika mazingira hayo, haikuwa ajabu kwa
mwanaume kumzidi mwanamke.
Mambo
yamebadilika. Wanawake wa kileo wanayo fursa sawa na wanaume katika maeneo yote
muhimu ya maisha. Wanawake wanakwenda shule sawa na wakati mwingine hata
kuwazidi wanaume. Fursa ya kusoma imewafungulia milango wanawake kuajiriwa na
kupata nafasi ambazo hapo awali zilikuwa haki ya wanaume.
Hapa
tunapata masomo mawili makubwa. Mosi, mwanaume wa sasa hawezi kuendelea kutegemea
udhaifu wa mwanamke kama kigezo cha kujihakikishia hadhi ya kuwa kichwa cha
familia. Kuendekeza ukandamizaji dhidi ya wanawake kama namna ya kulinda heshima
ya mwanaume ni jambo lisilowezekana.
Tulikofika
haiwezekani tena kurudi nyuma. Mwanaume mwenye mawazo ya kumzidi mwanamke
kielimu, kifedha, kimadaraka kama mbinu ya kujihakikishia heshima ya kichwa cha
familia anaweza asifanikiwe.
Somo
la pili ni haja ya kuondoa utata wa kimajukumu baina ya wanawake na wanaume. Mambo yamebadilika kiasi cha kufanya iwe vigumu kujua wajibu wa wanaume ni upi na kipi ni wajibu wa mwanamke. Mume, kwa mfano, anafikiri kazi yake kubwa ni kutoa fedha. Fedha zinampa
ujasiri.
Changamoto inakuja pale anapokutana na mwanamke asiye na shida na hizo fedha zake. Anachanganyikiwa hasa pale anapojikuta pamoja na kutoa fedha zake bado hapati yale mamlaka anayotamani kuwa nayo. Asichokijua ni kwamba shida ya mwanamke sio fedha kama anavyoamini bali kutokufanya wajibu wake asioufahamu.
Mwanamke naye anafikiri akishafanikiwa basi hana haja ya kumpa mwanaume nafasi yake. Kimsingi, kusema 'hampi nafasi' ni kumwonea kwa sababu hajui kwa hakika nafasi ya mume wake ni ipi. Mazingira haya ya kuchanganyikiwa yanafanya iwe lazima kuzitambua nafasi zetu katika familia.
Changamoto inakuja pale anapokutana na mwanamke asiye na shida na hizo fedha zake. Anachanganyikiwa hasa pale anapojikuta pamoja na kutoa fedha zake bado hapati yale mamlaka anayotamani kuwa nayo. Asichokijua ni kwamba shida ya mwanamke sio fedha kama anavyoamini bali kutokufanya wajibu wake asioufahamu.
Mwanamke naye anafikiri akishafanikiwa basi hana haja ya kumpa mwanaume nafasi yake. Kimsingi, kusema 'hampi nafasi' ni kumwonea kwa sababu hajui kwa hakika nafasi ya mume wake ni ipi. Mazingira haya ya kuchanganyikiwa yanafanya iwe lazima kuzitambua nafasi zetu katika familia.
Tukianza
na upande wa mwanaume, kujitambua ni muhimu. Huwezi kujiamini kama hujitambui. Mwanaume
anayejiamini anaelewa fika kuwa kichwa cha familia maana yake ni uwezo wa kuelewa
majukumu. Kichwa cha familia ni kuwa kiongozi. Kiongozi hujitoa, huipa familia
nafasi ya kwanza, kuheshimu mahitaji halisi ya mke na watoto wake.
Mwanaume
anayejiamini hana haja ya mwanaume kumshusha mwanamke ili yeye anufaike na
udhaifu wa mke wake. Mwanaume asiyejitambua hufikiri kumfokea, kumpiga, kumdhalilisha,
kumwamrisha na hata kumdhibiti mwanamke ndio kuwa kichwa cha familia. Hii si
kweli. Huwezi kuwa kichwa cha familia kwa kutegemea uduni wa unayemwongoza.
Mwanaume
wa sasa anahitaji kuelewa kuwa yeye mwenyewe ndio tishio la kweli kweli la hadhi
yake. Asipojiamini na kuelewa nafasi yake atakuwa anahatarisha nafasi yake kama
kichwa cha familia. Ndio kusema mwanaume imara, mwanaume anayejiamini, anayejitambua
na kuelewa wajibu wake, hatishwi na uimara wala mafanikio ya mwanamke.
Inaendelea
tatizo kubwa wanaume walio wengi wamejenga mtazamo hasi kwamba mwanamke akiwa na mafanikio zaidi ya mume wake hujenga kiburi na dharau kwa mumewe, ila kama ulivyosema hii ni kutokana na kutojiamini kwa mwanaume na kutoelewa nafasi yake katika familia ndio huona kuwa wanadharaulika kwa wake wao.
JibuFuta