Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Kujizuia

Madhara ya Kutoa Ushauri Kienyeji na Kuugeuza Unasihi kuwa Ushauri

Picha
Utamaduni wa (kutoa na kuomba) ushauri umejengeka kwenye misingi ya hekima ya wazee walioona mengi, uzoefu wa mtu mzima unaompa uhalali wa kutoa mwongozo wa kufuata kwa anayemzidi.  Hata tunaposikia unasihi (counselling), aghalabu, mawazo yetu yanaenda kwenye taaluma ya kushauri watu na kuwaambia cha kufanya ili kutatua matatizo yanayowakabili. Wapo, tena wengi, wanaotafsiri ‘counselling’ kama ushauri. Counselling sio ushauri. Katika makala haya, ninajenga hoja kuwa kutoa ushauri ni jambo la hatari na kwamba linaweza kusababisha madhara makubwa kwa anayeshauriwa lakini pia hata anayeshauri.  Kadhalika, ninalenga kuonesha, japo kwa ufupi kuwa hata kwenye unasihi msingi wa kwanza wa kuzingatia kwa mtoa huduma (aliyefuzu) ni kuepuka kabisa kutoa ushauri kwa mtu. Nakusudia kuonesha nini hasa huwa ni malengo ya unasihi. stefanamer/Getty Images Ushauri ni nini?  Unaposema unamshauri mtu unakuwa na maana gani?  Ushauri, kwa kifupi, ni maelekezo mahususi unayompa mtu, maamuz...

Unajua kugombana bila kufukua makaburi?

Picha
Picha: pixabay “Msitumie vibaya elimu zenu bwana,” Godi anaanzisha sogo kijiweni. Unamkumbuka?  Kaona kukaa haitoshi. Kasimama kabisa. Mikono inapepea hewani kusisitiza hoja, “Haya mambo yameanza leo? Ndoa zilikuwepo tangu enzi na enzi na hapakuwa na shida. Sasa nyie leo mnasema eti sisi wanaume ndio hatujui mahitaji ya wanawake? Mbona wazee wetu hawakujua hayo yote na bado ndoa zilidumu.”   Siku hizi ukitaka kuwachokoza wanaume ongelea matukio ya wanawake kunyanyasika. Salu kakaa pembeni anausoma mchezo. Tabasamu lake linaunga mkono hoja.   Hata hivyo, naona naye uvumilivu umemshinda. Kaamua kuulinda uanamue, “Hizi harakati zenu za kuwabeba wanawake zitatuharibia ndoa. Mie nawaambieni. Mnawatetea sana wanawake na watapata vichwa kweli. Wakitushinda tuwaleteeni basi.” Joto limepanda. Hisia hizi za akina Salu si za kupuuza. Mgogoro unapotokea kwenye ndoa, anayebebeshwa mzigo wa kutokufanya wajibu wake, mara nyingi, ni mwanamke. Msikilize Peki anavyogongea muhuri dh...

Kuuishi Wito Wako, Unahitaji Nidhamu ya Kujifunza

Picha
PICHA: findingmastery.net/ Nimekutana na vijana wengi wanaotaka niwaonyeshe njia ya mkato ya kufanya kazi za ndoto zao. Wanafikiri kupata kazi inayoendana na vipaji na tabia zao ni jambo la siku moja. Ingawa huwa ninawasaidia kujiuliza maswali ya msingi yanayowachochea kugundua hazina iliyolala ndani yao, bado husisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo mrefu wa kuona yasiyoonekana kwa macho. Nitatumia mfano wa Robert Green, mwandishi nimpendaye aliyeandika vitabu maarufu vya ‘The 48 Laws of Power, ‘Mastery’ na ‘The Art of Seduction.’ Ingawa tangu akiwa mdogo aligundua alitaka kuwa mwandishi, Robert hakuwa na uhakika anataka kuandika masuala gani.   Baada ya kumaliza chuo, Robert alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kazi hiyo, hata hivyo, haikumwendea vizuri. Mhariri wake alimshauri, ‘Tafuta kazi nyingine ya kufanya. Wewe si mwandishi. Hujui kupangilia mawazo yakaeleweka. Nakushauri ukatafute maisha mengine.” Robert anasema alijisikia vibaya kwa ...

Umuhimu wa Kusema Hapana kwa Ngono Kabla ya Ndoa

Picha
PICHA: eskimi.com Majuzi niliwaambia wanafunzi wangu wakitaka kuwa na ndoa bora hapo baadae, lazima wajifunze kuacha ngono kabla ya ndoa. Kusikia hivyo, walicheka mithili ya watu waliosikia kichekesho kipya cha mwaka. Sikushangaa. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, wastani wa umri wa kijana kuanza ngono ni miaka kati ya 14 na 15. Wanafunzi wangu walikuwa na kati ya umri wa miaka 21 na 23.