Blogu zakutanisha wanablogu...!


(picha mali ya Mtanga wa Mwananchi mimi)


Habari za kukutana kwa wenzetu watano nilizipokea kwa furaha kubwa. Hii kwa hakika ni hatua kubwa na ya kupigiwa mfano. Bila shaka, kama wanavyofikiri wanablogu wengine, huu utakuwa mwanzo mzuri kwa wengine wetu tukukutana mmoja mmoja na hatimaye wote kwa wakati mmoja kama walivyofanya wenzetu hawa.

Hongereni sana Mwananchi mimi, Hadubini, Mtambuzi, Lundunyasa na Chacha Wambura kwa kutuonyesha njia.

Wapo watu wanadhani matumizi ya majina bandia yanawasaidia. Niliona mjadala fulani kwenye mtandao wa Jamii forums ambao kwa kweli ni vigumu wanachama wake kukutana kama walivyofanya wenzetu. Bonyeza hapa uone na utafakari.

Tuachane na hao wasitaka kufahamika. Turudi kwa wenzetu waliweza kuutumia mtandao mpaka wakaweza kukutana siku ile. Hivi ndivyo Ndugu Fadhy anavyosimulia tukio hili:

"Muda huu hapa hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. Tunamshukuru sana Mungu kwani leo tumeweza kukutana tena bloggers kama unavyotuona pichani. Kutoka kushoto ni Fadhy Mtanga (kutoka Dar), Shaban Kaluse (kutoka Dar), Chacha o'Wambura (Kutoka Musoma)na Emertus Chibuga (kutoka Kigali Rwanda). Tumekuwa na wakati mzuri sana pamoja. Tumeweza kuwa pamoja na Simon Kitururu kwa simu kutokea Nairobi Kenya na Yasinta Ngonyani akiwa Sweden. Na tunamtarajia Markus Mpangala si punde.huu ni mwanzo mzuri wa ushirikiano wa bloggers.

Tunaamini tunaweza kupiga hatua nyingine zaidi ya hii kwa kukuza ushirikiano miongoni mwetu na ushiriki wetu katika mitandao hii ya jamii.

Udugu una mwanzo wa aina kadha wa kadha. Kublog kumejenga udugu.

Tunasema hii ni lifetime experience ambayo inaleta raha moyoni. Hebu fikiria raha uipatayo kukutana na mtu uliyekuwa ukiwasiliana naye kwa njia ya mtandao. Unawehuka kwa furaha isiyo kifani..."


Naye Ndugu Shabani Kaluse akatupa muhutasari wa yaliyozungumzwa:

" Naweza kusema kuwa wiki iliyopita imeacha kumbukumbu kichwani mwangu kutokana na tukio muhimu la kukutana na wanablog wenzangu pale katika Hoteli ya Movenpick.

Ni siku ambayo nilikutana na Chacha o’Wambura Ng’wanambiti na kaka Fadhy Mtanga na Kaka Chib ambapo tulibadilishana uzoefu juu ya Blog zetu hizi.

Mazungumzo yetu yalilenga zaidi katika kupanua wigo wa kublog na kuingia katika utunzi wa vitabu vya maarifa na riwaya. Lengo ni kupanua wigo wa yale tunayoandika ili yawafikie wananchi wengi wasioweza kupata habari za mtandaoni kutokana na ufinyu wa mtandao kutowafikia wananchi wengi vijijini na uelewa mdogo juu ya tasnia hii ya mtandao

Pia tuliazimia kujenga mkakati wa kuwalinda wanablog wa kike ili wasije wakatoweka katika tasnia hii ya blog na pia kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujitokeza na kuanza kublog na kuzungumzia matatizo yao na yale yanayoikabili jamii kwa ujumla.

Nisingependa kuzungumza mengi juu ya kukutana kwetu kwani Chacha na Fadhy wameshazungumzia maazimio tuliyofikia katika kikao chetu hicho..."

Kisha mkutano wao uliendelea mpaka nyumbani:



"...Lakini cha kufurahisha zaidi ni pale Fadhy aliponitembelea nyumbani kwangu maeneo ya Tabata na kupata wasaa wa kukutana na familia yangu.

Tulizungumza na Fadhy hadi saa mbili za usiku..."


Unasemaji ndugu msomaji. Blogu ni viwanja vya kutukanana na kukashifiana kama wanavyofikiri wengine au ni namna tu tunavyoweza kuzitumia?

Maoni

  1. kwa kwli mwanzo ni mzuri na naamini huu ni mwanzo tu wengi tutakuja kutana tu .

    JibuFuta
  2. Kwa kweli kwangu ilikuwa ni furaha kubwa kukutana na watu... ambao labda kama isingekuwa mambo ya blogu, nisingefanikiwa kukutana na watu hawa muhimu. Ni kweli huu ni mwanzo mzuri, kwani kwa kukutana na wanablogu hawa, niliweza pia kuongea na Mt Kitururu na Da Yasinta kwa njia ya simu. Yaani nilinenepa ghafla kama unavyoniona kwenye picha. Ahsante Bwaya kwa kunikumbusha furaha niliyoipata.

    JibuFuta
  3. Mambo hayo ni mazuri, na wanablogu tunayaunga mkono. Nami nilishajieleza hivyo kule kwenye blogu ya Ndugu Mtanga.

    Nitakuwepo Tanzania kuanzia Juni 8, na ninategemea kukutana na wanablogu kadhaa.

    Mimi huwa sionekani kwenye haya mahoteli makubwa kama Movenpick. Daima utanikuta huko u-Swazini. Sasa sijui itakuwaje.

    JibuFuta
  4. ni mambo poa. Niseme kitu kimoja nimewahi kuhudhuria mkutano wa wanabidii na kuna jama aliropoka kwamba ' of cousre mie ifichi jina langu' nilishtuka sana nikabaini kuwa msimamo wangu wa kutojihusisha na wanabidii ni kutokana na unafiki kama huu na kamwe sitjihusisha nayo. watu wanatumia majina feki siyo wakweli. halafu kuhusu kasfa na kutkana kwakweli inashangaza hebu mtazame mdogo wetu huyu wa clouds fm anaitwa DIVA hii ni blogu au nini? kuna wakati watu wanamtukana sana, lakini nadhani tatizo ni mhusika mwenyewe kutayarisha mazingira hayo. jamii forum na wanabidii siwezi kujihusisha nayo ingawaje watayarishaji wake ni rafiki zangu hasa Yona Maro. lakini nipo pembeni. blog ni ukweli kabisa

    JibuFuta
  5. Kaka Bwaya napenda kukushukuru sana kwa kuthamini kukutana kwetu.

    Siwezi kuficha, tukio lile limeacha kumbukumbu muhimu sana kwangu. Nilijiona kama mtu mwenye bahati sijui ya aina gani. Kama kaka Chib asemavyo, alinenepa ghafla, basi nami vivyo hivyo.

    Tunatarajia huu uwe utaratibu wa maisha. Kama wenzetu wasanii walivyo na utaratibu wa kukutana, nina amini nasi tumeanza kujenga utaratibu huo. Ni jambo la kufurahia sana.

    Tutazame mbele zaidi. Hao ma-anon waendelee na kupoteza kwao muda, haiwasaidii lolote.

    JibuFuta
  6. Profesa mbela usiwe na wasiwasi kuhusu mahali pa kukutania. mbona kikao chetu mie na Fadhy Mtanga kiliendelea hadi Uswahilini pale Buguruni?

    Tunaweza kukutana Pale Kimboka By Night, kuna mengi ya kujifunza ukiwa pale.....

    Bofya hii link ili kujua yanayojiri pale Buguruni uswahilini:

    http://kaluse.blogspot.com/2010/05/mkutano-wetu-na-wanablog-wenzangu-na.html

    JibuFuta
  7. Hata kama tukikutana wote na JUMUWATA bado imezikwa basi haina uzito wowote ule.

    JibuFuta
  8. Tuangalie namna ya kukutana zaidi na zaidi. Tukipanua wigo wa mikutano yetu, itatuleta karibu zaidi kuliko wanachama wa nyinginezo maarufu kwa vibomu lakini hawataki kutambuana kwa majina halisi.

    JibuFuta
  9. Kaka Bwaya naungana nawe. Kukutana kwetu kutakuwa chachu ya ushirikiano mzuri zaidi.

    JibuFuta
  10. Umoja ni nguvu.Malengo mazuri !

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?