Mhe. Zitto ni mwanablogu


Pamoja na kutumia nyenzo za uandishi wa kiraia kama twitter, facebook na majamvi ya kijamii kama Jamiiforums nk, Mhe. Zitto Kabwe ni mwanablogu. Na blogu yake imesheheni elimu na maarifa ambayo tunayahitaji kwenye majikwaa haya ya kiraia.

Ameitambulisha blogu yake siku chache zilizopita (tarehe 25 Mei) kwa maneno machache yafuatayo:

"Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi kama invyostahili. Nimeamua kuanzisha blogu hii mpya ili liwe jukwaa la kujadiliana jinsi ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Karibu kwa maoni, ushauri na hata makatazo!"

Bonyeza hapa kumsoma, halafu uone namna mwanasiasa huyu kijana alivyotofauti na wanasiasa wazee wasiojua kingine zaidi ya redio na magazeti ya kila wiki. Hawajui kwamba zama hizo zilishapita na hazitarudi tena.

Karibu sana Mhe. Zitto.

Maoni

  1. Mie nilianza kublog tarehe 23 May 2010.
    Kumbe tulikuwa na wazo moja ndani ya wiki moja

    JibuFuta
  2. Ni habari njema sana ndugu Bwaya. Tutajifunza mengi kutoka kwa mwanasiasa huyu kijana na mzoefu.

    JibuFuta
  3. role of youth in socio-economic and political transformation

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

UmahiriHisia (Emotional Intelligence) ni Nini?

Jifunze Uhusiano wa Malezi na Vilema vya Haiba (Personality Disorders)

Kutumia UmahiriHisia (Emotional Intelligence) Kuelewa Unavyojisikia

Kutumia UmahiriHisia (Emotional Intelligence) Kuimarisha Mahusiano

UmahiriHisia (Emotional Intelligence) Unavyosaidia Kurekebu na Kumudu Hisia

UmahiriHisia (Emotional Intelligence) Unavyochochea Motisha na Kujituma