Ya Santiago na nguvu za Kiraia

Mkutano uliokusanya wanablogu, wanahabari, wanaharakati na wanateknolojia watokao katika nchi mbalimbali umemalizika.

Siku mbili za mwanzo zilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali kutoka hapa Chile na sehemu nyinginezo ikiwa ni pamoja na Kampuni za google, Yahoo, You tube na wengineo.

Kilichokuwa muhimu sana katika siku hizo mbili za mwanzo, ni kutizama mifano ya namna uandishi wa kiraia (mablogu, twita, facebook, simu nk) ulivyoweza kushika kasi katika nchi mbalimbali zinazoendelea.

Unaweza kusoma muhtasari hapa kuona namna blogu zinavyoleta mageuzi nchini Madagaska kupitia jumuiya ya wanablogu iitwayo Foko.

Nilizungumza na Lova Rakotomalala juzi na nilishangazwa na jinsi jamaa wanavyoweza kufanya mambo makubwa katika mazingira magumu yanayofanana na yetu. Madagaska wamekuwa mfano mzuri wa nguvu ya uandishi wa kiraia.

Siku zile mbili za mkutano zilitupa ushahidi wa wazi wazi wa namna uandishi wa kiraia unavyopamba moto katika nchi zinazoendelea. Bofya hapa uone mifano michache ya mageuzi yaliyoletwa na sauti za kiraia katika nchi mbalimbali. Kisha ujehapa uone Bi. Anne Nelson anavyopima nguvu hiyo ya kiraia.

Je, blogu zimeleta mabadiliko gani katika jamii yetu ya Kitanzania? Je, tumeweeza kugeuka kuwa chanzo muhimu cha habari, maarifa na weledi kwa raia wenzetu? Je, tunapiga hatua mbele au tunarudi nyuma?

Maoni

  1. Mimi nafikiri kwa masuala ya blogu hapa Tanzania katika kuelimisha na kutoa habari, bado tuna safari ndefu. Mafanikio makubwa bado yapo katika kufahamiana wanablogu na kupata habari nyepesi nyepesi tu. Chache ndio huwa zinakuwa na maelimisho ya maana

    JibuFuta
  2. Ngoja nikusomeni vizuri.Kazi nzuri sana.

    JibuFuta
  3. Kazi nzuri Mkuu!Ngojea niviinilie viungo ulivyotuwekea kwanza

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?