CCM ni maarufu Kigoma kwa 40.2%, ikifuatiwa na CHADEMA kwa 27.2%

Utafiti huru uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umeonesha kwamba mgombea yeyote wa nafasi ya Urais wa Chama cha Mapinduzi angeweza kuchaguliwa na wapiga kura wa Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa asilimia 40.2% ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu jioni ya leo.


Aidha, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kingejipatia ushindi wa asilimia 27.2 wakati Chama kipya katika siasa za Tanzania, ACT Tanzania, kikionekana kuwa chaguo la asilimia 6.5 ya wananchi waliohojiwa katika kipindi hicho.

Utafiti huo ulifanywa leo mwandishi wa makala hii alipotembelea Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa shughuli zake za kikazi. Baada ya majukumu yake kukamilika saa 10 alasiri, shauku ya kutaka kujua upepo wa kisiasa mjini hapa ilimfanya aamue kuingia mitaani kufanya utafiti mdogo. Kazi hiyo ilifanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 jioni siku ya Alhamisi ya Februari 26, 2015.

Methodolojia
Jumla ya washiriki wa Utafiti huu walikuwa 92, wanaume wakiwa 58 na wanawake 34. Nane waliharibu kura zao. Usawa wa kijinsia haukuzingatiwa katika idadi ya washiriki 100 waliokusudiwa.

Washiriki walipatikana kwa njia ya nasibu kwa kukutana nao wakati mtafiti akiwa matembezini katikati ya viunga vya manispaa ya Ujiji/Kigoma yaani Mwanga, Hospitali ya Maweni, Kigoma stendi, Kibirizi na Ujiji. 

Mtafiti alihakikisha mshiriki ananaswa akiwa peke yake. Na ikiwa mshiriki alikuwa kwenye kundi/au aliambatana na mtu mwingine, mtafiti alimwomba mshiriki faragha kwa kumhoji akiwa peke yake. Aliokuwa nao/aliyekuwa naye hakuhojiwa/hawakuhojiwa. 

Kadhalika, washiriki walipatikana kwa njia ya mtawanyiko kwa maana kwamba mshiriki aliyehojiwa baada ya mshiriki mmoja, ilibidi apatikane kwenye umbali wa zaidi ya mita 50 kuongeza nafasi ya mtawanyiko.
 
Umri haukuulizwa, isipokuwa katika mazingira ambayo mtafiti alikuwa na wasiwasi na umri wa mshiriki kutokutimia miaka 18. Ikiwa mshiriki alikiri kutokufikisha miaka 18, hakuhojiwa.
Hata hivyo, kwa ujumla mtafiti alihakikisha washiriki wanawakilisha makundi yote ya umri kuanzia miaka 18 mpaka wazee. Jinsia ilizingatiwa ingawa si kwa idadi iliyo sawa kama inavyoonekana hapo juu.


Uulizaji wa Swali
Mtafiti alimsalimia mshiriki na kujitambulisha kwa ufupi. Kisha, alimwarifu mshiriki lengo la utafiti na kumtaka asitaje taarifa zake binafsi kulinda faragha yake. 

Kisha swali lililoulizwa kwa washiriki wote lilikuwa, “Ikiwa uchaguzi ungefanyika leo, na ukapata nafasi ya kupiga kura kumchagua Rais mpya wa Tanzania, Je, ungemchagua mgombea wa chama gani?” Mshiriki alihakikishiwa kwamba jibu lolote atakalolitoa litakuwa sahihi.


Matokeo

Mchoro unaoonesha mhutasari wa takwimu za utafiti huu. Chanzo: Mwandishi wa makala haya
Washiriki 37, sawa na asilimia 40.2 walisema wangemchagua mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Washiriki 25, sawa na asilimia 27.2 walisema wangemchagua mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakati washiriki 6, sawa na asilimia 6.5 walisema wangemchagua mgombea wa Chama kipya cha ACT Tanzania. 

Ingawa washiriki 2, sawa na asilimia 2.17 walisema wangemchagua mgombea wa Chama cha NCCR Mageuzi, ni mshiriki mmoja tu, sawa na asilimia 1.09 alisema angemchagua mgombea wa Chama cha Wananchi, CUF.

Hata hivyo, washiriki wapatao 21, sawa na asilimia 22.8 ya waliohijiwa walisema hawajaamua/hawachagui vyama na kwamba wanasubiri kujua wagombea watakaojitokeza.

Washiriki nane waliharibu kura zao kwa kutaja dini, kabila na vigezo vingine badala ya majibu ya moja kwa moja kama vile 1) kutaja chama au 2) maelezo yanayoonesha kwamba mshiriki hajaamua. 

Ukomo na tafsiri ya Utafiti 

Matokeo ya Utafiti huu yananaakisi maoni ya washiriki katika mitaa ya Manispaa ya Kigoma kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu siku ya Alhamisi ya tarehe 26 Februari, 2015 pekee. Hayawezi kutumika kuelezea hali ya kisiasa kwa maeneo mengine ya Kigoma zaidi ya hayo yaliyotajwa. 

Hata hivyo, kwa kuwa asilimia 22.8 ya waliohojiwa hawajaamua, ni vigumu kubashiri kwa hakika, ni mgombea yupi angeweza kushinda katika kipindi cha Utafiti ikiwa majina ya wagombea yangekuwa yanafahamika.  

Kadhalika, njia ya kuuliza swali kwa mdomo inaweza kumfanya mshiriki atoe majibu tofauti na yale ambayo angeweza kuyatoa ikiwa angeulizwa kwa maandishi au bila kuonana na mtafiti. Kuna uwezekano wa mshiriki kutoa majibu anayodhani yanatarajiwa na mtafiti ingawa jitihada zilifanyika kupunguza athari hiyo.

Je, matokeo haya yanatoa taswira gani katika kuelezea mwenendo wa siasa za Kigoma?

Utafiti huu, ni matokeo ya shauku ya mwandishi wa makala haya kuelewa hali ya kisiasa mjini Kigoma kwa njia ya kisayansi. Kwa namna yoyote ile, kusudi la utafiti huu, halihusiani na taasisi inayomhusu mwandishi wa makala haya.

Maoni

  1. Pamoja na tahadhari ulizmatokeoota kuhusu namna ya kutafsiri matokeo ya utafiti wako mdogo, maoni yangu ni kwamba CCM imeanguka, au inaanguka, tukizingatia kuwa huko miaka iliyopita, CCM ilikuwa ikizoa asilimia kubwa kabisa.

    Vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, vinapanda chati, kuanzia 0% hadi hapa vilipo sasa.

    JibuFuta
  2. Nakubaliana na wewe, Profesa. Vyama vya upinzani vinazidi kupata nguvu. Kwa mfano, upo uwezekano, tena mkubwa tu, wa kundi la asilimia 22.8 la 'wasioamua', kuungana na kundi la asilimia 27.2 + 6.5 + 2. 17 + 1. 09 na kuidondosha CCM kiurahisi katika maeneo ya Kigoma Mjini.

    JibuFuta
  3. Thank you for the information of his article

    jual obat bius

    obat tidur

    JibuFuta
  4. This blog is so nice to me. I will continue to come here again and again. Visit my link as well. Good luck
    http://www.apotikobatcytotec.com ( Obat Aborsi )
    http://www.doktersahabat.com ( Cara Menggugurkan Kandungan )

    JibuFuta
  5. Obat Perangsang Wanita di Apotik Alami Harga Murah Paling Ampuh

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia