Watoto Waliokosa Masomo Nchini Libya Wafundishwa kwa Njia ya Skype

Hali tete ya kiusalama nchini Libya imewafanya watoto washindwe kwenda shule tangu mwezi Oktoba. Kwa kuwa watoto hawawezi tena kuhudhuria masomo katika shule zao, El-Zahawi aliwaza ni kwa nini asisogeze madarasa karibu na huko walipo? Na hapa ndipo Shule ya Skype ya Benghazi ilipozaliwa rasmi.


"Tulianza na akaunti ya mtu binafsi pamoja na Skype", anasema El-Zahawi akiwa mjini New York. Aliweka taarifa za mradi wake huu katika mitandao ya kijamii akiwaomba raia wa Libya kumsaidia. Katika muda wa wiki moja amepata "matokeo makubwa na ya kutia moyo kabisa." Pia alipata habari kuwa kuna kampuni moja ya Teknolojia ya Mawasiliano ilitaka kumfadhili.

Haifa El-Zahawi anaishi nchini Marekani. Aliondoka wakati Libya ilipokumbwa na ghasia za mapinduzi mwaka 2011. Kwa sasa anatafuta kazi akiwa kama daktari wa afya ya kinywa. Lakini pia, anautumia muda wake katika mradi mwingine wa kipekee: Anafundisha watoto nchini Libya.



Children in Tripoli in August 2011. Photo by MITSUYOSHI IWASHIGE. Copyright Demotix
 Watoto wakiwa huko Tripoli, Agusti, 2011. Picha na MITSUYOSHI IWASHIGE. Haki miliki Demotix

Hata hivyo, masomo kupitia mtandao wa intaneti yana changamoto zake. Upatikanaji wa mtandao wa intaneti usiotabirika ni kikwazo kikubwa kinachochangiwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara linalowakabili raia wa Libya. "Tunajaribu kwa kadiri tuwezavyo kuhakikisha wanafunzi wanapata masomo papo kwa hapo, lakini kutokana na changamoto zilizopo ... tunajaribu kurekodi masomo na kisha kuyapakia mtandaoni," El-Zahawi anasema.

Lakini, pamoja na changamoto hizi, Shule ya Skype ya Benghazi hadi sasa imekuwa na mafanikio makubwa. "Familia zimetutumia picha zinazoonesha wanafunzi wakifanya kazi wanazopewa na mwalimu wao," El-Zahawi anasema. "Pia, wanavaa sare zao za shule."

Wazo kuu la kuanzisha shule hii, El-Zahawi anasema ni kurudisha matumaini kwa familia na watoto "wanaohitaji elimu." Anaogopeshwa na habari kama hii ya hivi karibuni ya kuchinjwa kwa watu kadhaa nchini Libya na kundi la ISIS, na anaamini kuwa kwa kuwaelimisha watoto wa Libya kutasaidia kukomesha kuenea kwa ukatili huu.

"Tunahitaji kuwapatia elimu watoto wetu," anasema, "elimu tu ndiyo itakayotusaida kupambana na hali hii."

Makala haya yaliandaliwa na  Shirin Jaafari  kwa mara ya kwanza yalionekana kwenye tovuti ya PRI.org na kuchapishwa tena kwenye tovuti ya Global Voices.

Maoni

  1. KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل

    KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل


    KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?