Mwaliko wa Mkutano wa Global Voices, Dar es Salaam, Novemba 1, 2014

Tunayo furaha kubwa kutangaza mkutano wa Global Voices unaotarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Tanzania siku ya Jumapili, Novemba 2, 2014 kuanzia saa 6 mchana hadi saa 10 adhuhuri. Mkutano huo utafanyika kwenye Kituo cha Teknolojia na Mambo ya Jamii, KINU, washirika wa Global Voices Swahili hapa nchini.

Mikutano ya Global Voices ni mikusanyiko midogo inayokusudiwa kusaidia kuwaunganisha waandishi na watafsiri wa Global Voices na wasomaji pamoja na wadau wa habari za kiraia katika maeneo inakofanyikia mikutano hiyo.

Wakati mkutano huu ukifanyika, mikutano ya namna hii itakuwa ikifanyika pia kwenye miji ya Accra, Beirut, Tunis na Belgrade.

Mkutano huu wa Dar es Salaam unakuwa fursa ya mara ya kwanza kabisa kwa Global Voices kukutana na wasomaji wetu nchini Tanzania. Katika agenda za mkutano, kadhalika, kutakuwa na mada kuhusu Uandishi wa Kiraia Tanzania itakayotolewa na Ndesanjo Macha, ambaye ni mwanablogu wa kwanza nchini Tanzania, namna ya kukusanya na kuandika kwa ajili ya wasomaji wa Kitanzania, itakayotolewa na Constantine Manda wa Vijana FM, umuhimu wa kuandika katika lugha ya Kiswahili, itakayotolewa na Zamda Ramadharan, Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyinginezo.

Unaweza kuona agenda kamili za mkutano huo hapa.

Kama unapenda kushiriki, tafadhali jaza fomu ya kujiandikisha. Tukio hili liko wazi kwa wote ingawa nafasi ni chache sana.

Hapa unaweza kuona ramani ya namna ya kufika kwenye Jengo la Conservation lililo kwenye barabara ya Ali Hassani Mwinyi, karibu na Ofisi za Airtel, Moroko, mahali utakapofanyikia mkutano.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: christianbwaya [at] gmail [dot] com

Makala haya yalichapishwa awali na Global Voices.

Maoni

  1. nawatakieni yote mema na nasikitika kwamba sitaweza kuhudhuria

    JibuFuta
  2. Asante sana Yasinta kwa kututakia heri. Tutapatikana kwenye mtandao wa Twita unaweza kutufuatilia bila wasiwasi wowote

    JibuFuta
  3. Nawapongeza sana kwa kuanzisha Global Voice na pia kuwashirikisha wengine kujua zaidi kuhusu uandishi wa Kiraia.Nilikiwa kama mdau wa masuala ya uandishi nilipenda sana kuhudhuria, ila kwa sasa nipo masomoni Arusha.Naweza kumtuma mwakilishi wangu wa kampuni?
    Henry Kazula.
    Mwandishi,Jielimishe Kwanza!

    JibuFuta
  4. Ndugu Henry asante sana kwa kutambua juhudi hizo. Kwa kuwa ufanisi wa mkutano ni wadau kama ninyi, unaweza kabisa kumtuma mwakilishi. Muhimu ni kuhakikisha anajaza/umjazie fomu ya kujiandikisha. Nimeweka kiungo chake hapa chini. Karibu sana.

    https://docs.google.com/forms/d/1DxhL6XfJoDSZwDbObeqk0a22gpuY_Soj_JF80CAI3yI/viewform?c=0&w=1

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?