Habari za siku ndugu msomaji. Binafsi sijambo. Nafurahi kurejea kibarazani baada ya heka heka za huko na huko. Itoshe kuhusu mimi, nikukaribishe tena humu ndani. Leo ningependa kukusimulia kisa kimoja. Nikuase kwanza, kwamba usilazimike kunielewa vibaya. Sijawa na tabia ya kuona makosa zaidi niwapo mahali ama nikutanapo na watu. Maana siamini kwamba binadamu ana kazi ya kushabikia makosa kuliko jema moja. Nisijitetee sana. Jumapili hii nilipata fursa ya kuhudhuria ibada kwenye kanisa la 'kisomi'. Washirika wa kanisa hili, wengi wao ni wale ambao umande haukuwazuia kuhudhuria shule. Wamesoma. Pamoja na ukweli kwamba wote walikuwa weusi kama mimi, lakini ilikuwa bayana kwamba kiingereza kilikuwa 'nguzo' ya ibada hiyo. Hilo halikuwa tatizo kwangu. Maana inaeleweka kwa wengi wetu kwamba, kusoma kunathibitishwa na umahiri wa kusema kiingereza. Nshazoea hili. Pamoja na ukweli kwamba kiuhalisia kiswahili ndicho kinachotawala madarasani lakini watu hatutaki kuukubali ukweli...
kaka Bwaya, hapa kazi hipo.Darasa kali, kazi kwelikweli
JibuFutaUkweli ndiyo huo,jamii imetufundisha kuukubali uongo ili tujisikie nafuu.
JibuFutaKaka bwaya kuna kitu ninajiuliza ni kwanini tulipokuwa wadogo tuliambiwa kumpa mtu kitu kwa mkono wa kushoto ni kukosa adabu?Wanablog naomba msaada wenu?
Kweli kabisa,Ndg Bwaya.Ndio maana baadhi ya watawala wanachotaraji katika hotuba zao ni makofi,vigeregere,shwangwe,vifijo,nderemo,makofi,nk...akizomewa,basi hapo hapakaliki.
JibuFutaTatizo kubwa ni kwamba tukiambiwa ukweli huwa tunakasirika na kuwa wakali, lakini pamoja na hayo mi bado napenda kuambiwa ukweli ila tu uwe kwenye soft language kidogo
JibuFutaYule bwana aliyewahi kusema kuwa dunia hii ina umbo la bapa kama meza alionekana mkweli, lakini yule aliyesema kuwa dunia ina umbo la duara aliswekwa lupango kwa na mfalme kwa kusema uongo.
JibuFutakaka Bwaya leo hii ukisema kuwa njia hii ya kuchagua viongozi wetu kwa kutumia nadharia ya Wagiriki wenyewe wanaita Demokrasia haitufai bali turejee kwenye zile njia zetu za asili za kuwapata viongozi walizotumia mababu zetu utaonekana mwehu na juha.
Habari za hapa Kaka Bwaya.
JibuFutaNimepita hapa kibarazani kwako kujitambulisha kuwa nimefungua kijibaraza changu kitakachokuwa kikijihusisha zaidi na masuala ya vijana.
Nimekuwa nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu, na sasa nimeamua na mimi nijitose uwanjani ili kuongeza mchango katika kuielimisha jamii.
Niko ntayari kuelimishwa na kukosolewa pale nitakapoonekana natoka nje ya mstari.
Natarajia ushirikiano wako.
Digna
Bennet na Digna karibuni sana. Nafurahi kuwapokea kama wadau muhimu wa kibaraza hiki.
JibuFuta