Kama sio utumwa ni nini hiki?
Habari za siku ndugu msomaji. Binafsi sijambo. Nafurahi kurejea kibarazani baada ya heka heka za huko na huko. Itoshe kuhusu mimi, nikukaribishe tena humu ndani. Leo ningependa kukusimulia kisa kimoja. Nikuase kwanza, kwamba usilazimike kunielewa vibaya. Sijawa na tabia ya kuona makosa zaidi niwapo mahali ama nikutanapo na watu. Maana siamini kwamba binadamu ana kazi ya kushabikia makosa kuliko jema moja. Nisijitetee sana. Jumapili hii nilipata fursa ya kuhudhuria ibada kwenye kanisa la 'kisomi'. Washirika wa kanisa hili, wengi wao ni wale ambao umande haukuwazuia kuhudhuria shule. Wamesoma. Pamoja na ukweli kwamba wote walikuwa weusi kama mimi, lakini ilikuwa bayana kwamba kiingereza kilikuwa 'nguzo' ya ibada hiyo. Hilo halikuwa tatizo kwangu. Maana inaeleweka kwa wengi wetu kwamba, kusoma kunathibitishwa na umahiri wa kusema kiingereza. Nshazoea hili. Pamoja na ukweli kwamba kiuhalisia kiswahili ndicho kinachotawala madarasani lakini watu hatutaki kuukubali ukweli...

Naona chombo cha kuweka vumbi za sigara na mtu maisha yamemshinda
JibuFutabwaya amini usiamini hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kufupisha maisha ya bin adamu na hakuna kitu chochote ambacho kinaweza kurefusha maisha ya bin adamu hata kama ni hizo arv wanazotudanganya nazo.
JibuFutakila mmoja wetu awe na starehe anayoipenda.kama mimi natumia sigara,pombe na kufanya zinaa ni maisha yangu kwani hapa sitokuwa nafupisha maisha.
amani kaka.
Sio sigara tu kaka Bwaya, hata vyakula tulavyo hufupisha maisha.
JibuFutawewe kama huvuti sigara halafu unakula hovyo unaweza kutangulia kufa ukamuacha mvuta fegi anatesa duniani.
Hebumuangalie mzee Fedel Castro wa Cuba.
mzee anakula SIGA ila mbaya lakini anaendelea kupeta na maisha, hana wasiwasi.
Du picha nzuri ukicheki vizuri sigara inakuwa mwili wa marehemu umelazwa sakafuni.
JibuFutakwaani nani kasema kufa ni kubaya? mnaogopa au kuchukia kufa? kama ni kweli basi mnajichukia wenyewe
JibuFutaKamala kumbe ile elimu ya milo uliyokuwa unatupa ni ili kuharakisha kifo eh?
JibuFutandio
JibuFutaBasi ungefafanua ili wasomaji wako waamue kabla ya kuutumia ushauri wako. Baadhi yetu tulifikiri tofauti. Kwamba elimu ya kula ingesaidia kurefusha maisha.
JibuFutaMimi huwa nafurahi sana napokutana na comments nyingi za Kalama, unakuta ni fupi ila ujumbe ni mzito mno.Nakuaminia brother.
JibuFutaHiyo picha kusema kweli inaonesha kama mtu flani....da kweli hiyo taswira Bwaya.
Thanks Bwaya kwa pic hiyo
MAKULILO Jr,
www.makulilo.blogspot.com
Nani asiejua kama sigara ni mbaya na inauua pole pole lakini waswahili wanalonga kua kufa kufaana, yetu macho tu.
JibuFuta