Unajua wanyaturu walipangaje uzazi?

Yapo mambo mengi katika jamii zetu yaliyofanyika zamani ambayo tukiyatazama twaweza kujifunza mengi. Mengi ya hayo, si sehemu ya jamii za kisasa hivi leo, lakini yalekuwa na msaada wa namna Fulani kwa jamii.

Katika jamii ya asili ya wanyaturu, kabila dogo linalopatika katika wilaya ya Singida (na kidogo manyoni), mahusiano kati ya baba na mama yalikuwa na sura tofauti sana na ilivyo leo.

Wakati leo hii, wazazi kulala vyumba tofauti huchukuliwa kama ishara ya kufifia kwa mahusiano baina ya wawili hao, kwa Wanyaturu hiyo ilikuwa na maana tofauti.
Kikawaida, wazazi wa Kinyaturu hawakupaswa kukaa nyumba moja (sio chumba kimoja, nyumba moja) ndani ya boma.

Katika boma analojenga mwanaume kama himaya ya familia yake, alipaswa kuzingatia uwepo wa nyumba mbili ndnai ya boma moja. Baba ambaye ndiye mkuu wa boma, alilala na wanawe wa kiume katika sehemu maalumu ya nyumba inayojulikana kama "Idemu/Ikumbu". Nyumba hiyo ilijitenga pembeni na nyumba kuu alikoishi mama na wanawe wa kike.

Huko anakoishi mama, ndiko palikuwa stoo ya nafaka na jiko (akipika, chakula huletwa wanakoishi wanaume ambako wangekula wao kwanza na kinachobaki kingerudishwa kwa mama na wanawe wa kike ili nao wale).

Kwa hiyo haikuwa kawaida kwa mume na mke kulala nyumba moja. Chumba kimoja ndio sahau kabisa.

Hata hivyo, pamoja na mazingira hayo ya aina yake, bado uzazi uliwezekana. Ni lini baba na mama walikutana, hiyo ilibaki kuwa siri ya wawili hao na hakuna mtu yeyote katika boma angeweza kubaini.

Namna hii ya maisha iliwasaidia wazazi kupanga uzazi. Maana achano la kawaida la umri wa watoto wanaofuatana katika familia nyingi za Kinyaturu lilikuwa miaka miwili. Nadhani pamoja na sababu nyingine nisizozijua, aina ya mahusiano yaliyokuwepo kati ya wanandoa ilichangia kwa sehemu kubwa.

Lakini leo, pamoja na kusambaa kwa ‘mashinikizo’ ya watu Fulani wanaotamani tupungue kwa mbinu mpya za uzazi wa mpango, as long as wanandoa wanalala pamoja, familia nyingi za Wanyaturu Sasa hivi zinakabiliana na kile kinachoitwa “bebi bum”.

Maoni

  1. Mr. Bwaya,
    Nakubaliana kabisa kuwa kwa kutokulala nyumba moja ilisaidia kupanga uzazi. Lakini ujue kuwa kwa kipindi ambacho mtoto alikuwa bado ananyonya baba na mama walikuwa hawawezi kukutana kutokana na imani kuwa mtoto anaweza kupata magonjwa! Na kwa kipindi hicho ambacho cha mtoto kunyonya, baba aliruhusiwa kuwa na "nyumba ndogo". Na hii ilikuwa inakubalika kwa jamii, hata mama aliweza kumjua mwanamke ambaye mumewe alikuwa na mahusiano! Na hii haikuleta shida kwani jamii ilisema kama wewe kumhudumia mume wako, aende wapi??!!
    Kwa jamii yetu ya leo sio rahisi, magonjwa yako mengi, inabidi tu hizo mila zife na baba na mama walale chumba kimoja!

    Hawa.

    JibuFuta
  2. Bw. Bwaya

    Nasikitika alietoa mchango sasa hivi ni ANONYMOUS, lakini mawazo yake mazuri sana.

    Kwa mchango wangu, sisi Waafrika lazima tuchukue kile kizuri katika mila na desturi zetu na tuchang'anye na elimu pamoja sayansi tuliyekuwa nayo sasa hivi ili twendelee mbele.

    Sijawahi kulala mbali na mke wangu. Lakini nafikiri hiyo inaweza kusaidia mnapolala pamoja tena mmekumbukana. Vilevile itasaidia kwamba mwanauume aliyekuwa safarini asilazimike kutafuta wale dada wenye sifa zao kutokana na kwamba "hakuzowea kulala peke yake".

    Ya mwisho. Nimefurahia kupata undani wa Wanyaturu uliposema "Katika boma analojenga mwanaume kama himaya ya familia yake, alipaswa kuzingatia uwepo wa...'Ikumbu'". KUMKUMBUKA mke wake siku moja hiyo ni lazima tu!!! (LOL)

    JibuFuta
  3. Duuh, mke analala kwenye nyumba yake(boma)..whatever...naona hiyo ndiyo ilikuwa hivyo kwa taratibu zao, lakini kama mke akiamua kuwa na nyumba ndogo, akawa anajiwa usiku wangelijuaje, na ...hata mume akiamua hivyo...nawaza tu!
    Mke na mume ni mwili mmoja, au sio...ok, labda kwa vile waliamini kimila sio kidini...nawaza tu

    JibuFuta
  4. Anonymous, ni kweli mila hii ilikikuwa na matatizo yake kama ulivyoeleza. Nashukuru kwa kutupa upande wa pili. Nimejaribu kuonyesha utamaduni wa kale wa jamii ya Wanyaturu, ambao hata hivyo umekwisha kufa kwa sehemu kubwa kama zilivyo mila nyingine nyingi.

    JibuFuta
  5. @Phiri, ni kweli unavyosema. Pamoja na umuhimu wa kuzitambua na kuziheshimu mila zetu kama Waafrika wenye, ni vyema kuzisaili kiupya kabisa.

    Mfano ni namna uhusiano wa mume na mke ulivyokuwa katika jamii nyingi za Kiafrika zilizomchukulia mwanamke kama mtu duni asiyestahili heshima. Hili hatupaswi kuliacha liendelee katika jamii ya sasa. Ni muhimu kuyasaili upya mahusiano haya kwa lengo la kuyaboresha. Kufanya hivyo kama ulivyoeleza, itapunguza matatizo mengi yasiyo ya lazima.

    @M3, Inawezekana hata akina mama nao waliweza kutumia nafasi hiyo kuja na nyumba ndogo kwenye boma. Kwa vyovyote, madhara ya tabia hii yalikuwa bayana hata kama huenda ilisaidia kupanga uzazi.

    JibuFuta
  6. Ndiyo maana niliwahi kumbishia mwanafunzi aliyekuwa anadai kwamba eti Waafrika hatukuwa na aina yo yote ya uzazi wa mpango wakati watoto wengi wa Kisukuma tulikuwa tunapishana miaka miwili miwili au mitatu mitatu.

    http://matondo.blogspot.com/2010/01/hakukuwa-na-uzazi-wa-mpango-barani.html

    Asante kwa mada nzuri!

    JibuFuta
  7. Ndio tatizo kubwa tunaokabiliana nalo siku hizi,Bw Masangu!

    Mzungu mwenyewe kwa utafiti wake amegundua kwao na Uzungu wake ni Afrika, lakini Waafrika wenyewe wanamkataa Mzungu na kama hawamkatai Mzungu wanapinga kwamba ujuzi wake ulitoka hapahapa Afrika kwa Mswahili.


    Chukulia mfano wa uzazi pitia Caesarian (YAANI KUMPASUA MWANAMKE MJAMZITO ILI AZAE IKIWA ANAKISUKARI NA MAMBO KAMA HAYO YANAOZUWIA UZAZI WA KAWAIDA).

    Yapo maandishi yanaonyesha kwamba wakati Ulaya kulikuwa hamna hata mwanamke mmoja aliyekuwa anapona baada ya oparesheni hiyo, Waswahili waSudan walikuwa wanafanya tu kama kawaida.


    Hata hilo somo la Hesabu zinazowezesha mtu kuwa daktari, ENGINEER na mambo kama hayo lilikuwa imara huko Misri/Kameta wakati Afrika ilipokuwa ni ya Waswahili tupu.


    Tatizo tu ni kwamba ukibishana na watu wavivu kusoma historia ya binadamu utachoka bure tu! Pole!

    Lakini kuwadharau Wanyaturu au makabila mengine yaAfrika kwa kuwa 'eti sisi "tumestaarabika" leo', NDIO UJINGA KABISA.


    "Chema cha jiuza; kibaya chajitembeza!!!"

    JibuFuta
  8. Swali lako linaonesha kana kwamba, dini imekuwa msaada mkubwa sana katika jamii, inaonesha kwamba dini imesaidia sana kuleta hali ya utulivu kwa jamii yetu. Sawa kabisa. Ni kweli. Lakini umelitafakari kwa makini jambo hilo?

    Dini badara ya k...uwa msaada mkubwa katika jamii yetu, badala yake imekuwa kama sehemu ya kujificha watu waovu, waliojaa husuda na wazinifu sugu pamoja na wachawi watu ambao ni sumu kubwa katika jamii yetu.

    Nisemapo kuwa watu hao wapo katika dini zetu na hapa haijalishi kuwa ni dini gani, eiza Uhindu, Tao ama Ukristo au Uislam, katika dini hizo kumejaa waovu na waovu japo si wote. Watu wamekuwa hawana hofu kwa MUNGU, bali kwa mwanadam.

    Mfano, Mtu anaweza akawa anatembea tembea, mara akakutana na Ubao wa Jeshi umeandikwa, "Ni marufuku kupita eneo hili, ni eneo la Jeshi" basi nakuambia ndg Mtangazaji ya kwamba, mtu yule mara moja atageuza miguu, ama usafiri wake na kuanza kurudi alikotoka.

    Sasa mtu huyo huyo tena chukulia kuwa ni mtu wa dini. Akasoma katika kitab chake pengine kuna amri ya MUNGU wake imesema, "Usiwe na miungu mingine ila Mimi" basi mwanadamu yule hatoiogopa amri hiyo na ikitokea kuna miungu, anaabudu na wala hana hofu. Najaribu kukueleza hayo mtangazaji ili kuonesha jinsi gani dini ambavyo haina msaada wowote katika jamii yetu.

    Na kwa kujibu swali lako kwamba, "Jamii ingekuwaje bila dini" mimi nasema ya kwamba, jamii ingekuwa shwari tu tena sana tu. Kwa maana kuna sheria zinazolinda hali ya amani katika jamii yetu. Mtu haogopi kuuwa kisa dini, bali anaogopa kuuwa kwa kuwa anajua kama akiua, basi na yeye pia kuuliwa, ama kufungwa jela maisha.

    Mtu pia anaogopa kubaka, si kwa hofu ya MUNGU, Bali ni kwa sababu kuna sheria inayosema kama ukibaka, ni jera miaka 30. Mwanadamu hana hofu kabisa na hukumu za baadaye zinenwazo na BWANA MUNGU. Anaogopa tu zile hukumu za adhabu anazoziona kwa macho, lakini hizi za kusimuliwa, wala hazimpi shida.

    Labda kama ungeuliza ya kwamba, "Jamii ingekuwaje bila sheria", ama hapo pangekuwapo shughuli kubwa, mauaji yangalitapakaa kila sehemu.

    Nahitimisha kwa kuiasa jamii ya kwamba, ni kheli kama wangejenga hofu zao katika sheria za MUNGU, Hapo patakuwa safi sana. Maana kama tukiwa na hofu na amri za MUNGU, Nchi yo yote tutakaa kwa amani, kwa maana hizo nchi zenyewe zimeweka izo sheria kutoka katka sheria za MUNGU. Dini zetu bila shaka zote hutufundisha mambo mema.

    Tusiogope mwanadam, bali tumwogopeni MUNGU na amri zake. Na amri zake wala si nzito. Ni kutokuwa na Miungu wengne isipokuwa YEYE, Kutojifanyia sanamu ya kuchonga, Kutokulitaja Jina lake bure, Kuitunza sabato yake ya jumamosi, kuwaheshimu wazazi, Kutoua, Kutozini, Kutoiba, Kutomsemea mwenzako uongo na Kutotamani vya mwenzako.

    Kama utataka kuzijua kwa ufasaha, waweza ukazisoma katika Kitabu cha Biblia kitabu cha Kutoka na sura ya 20. Amri rahisi kabisa. Kama jamii itakuwa na hofu na amri hizo, tunaweza tukawa na jamii yenye baraka za BWANA.

    Tena sana zaidi. Jifunzeni kwa hao wazitunzao, muone ile mibaraka waipatayo, kwa maana Mwenye amri aliahidi mibaraka ya kutosha kwa hao watakaozitunza. BWANA awabariki na kuwalinda. Ila ondoka na hili, "Jamii bila sheria, haiwezekani"
    ----------------------------------------------------------------

    JibuFuta
  9. kaka hongera kwa mada nzuri iliyopo sasa imenigusa sana kwani hiyo ndiyo mila halisi ya wanyaturu na hongera kwani mkataa asili ni mtumwa, kujua asili yako ni moja ya ishara za kukomboka kifikra,pamoja na kujiamini kwani u muwazi kuhusu ukweli wako.
    hii inanikumbusha licha ya wazazi kuishi tofauti hata watoto walipofikia umri wa AHOMBA yaani vijana wa kiume wenye umri wa miaka kuanzia mitano hutengwa na mama yao na kuishi katika IKIMBU mpaka pale watakapo fikia umri wa kuoa.

    JibuFuta
  10. Ni kweli kabisa ameongea ukweli na hayo nayasadifu mm kama kijana wa kinyaturu na nayaunga mkono hadi kesho
    ✍kwanza nianze kwa kujibu baadhi ya maswali na pingamizi

    Hivyo ndivyo ilivyosaidia kupanga uzazi kwa wanyaturu
    ✍ifahamike mabinti wa kinyaturu wanajoto kubwa la mwili hivyo kulala muda wote pembeni inaharibu mtajikuta mnazaa kila mwaka

    ✍kuhusu kulala tofauti tofauti hakuwezi kusababisha uzinzi kwa sababu dingi analala na watoto wakiume mnapiga hadithi za kiume hadi mida saa 5 mnalala,,;afu dingi anakua ameambatana na watoto wakiume muda mwing ata porini
    Kama ilivyo kwa mama hivyohivyo
    Na kutoka nje ya ndoa mtoto anakuona haiwezekani ni kujivunjia heshima (inafahamika hii)

    ✍usiku ndo huwa dingi huamka na kumfuta mkewe nyie hapo mmshelala fofo Hamwelewi chochote (akirudi unafikiri alienda msalani tuy)
    Na hii inawajengea watoto taswira nzuri ya tabia nzuri kutokujua mambo mapema
    Tofauti na saivi mambo yalivyo mtoto mdogo tuy shida!!!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?