Ninapoahirisha mafanikio yangu kwa "kukwepa" kuamua

Mambo mengi yenye matokeo mazuri, si rahisi kuyafanya. Hasa ikiwa utekelezaji wake unadai utashi, “usilolazimishwa” na mamlaka iliyo nje na mtu mwenyewe. Ugumu wa mambo haya, ni zile zinazoonekana kuwa gharama za papo kwa hapo, zinazoweza kutukwaza tukate tama ya kufanya yale tuyapendayo.

Matokeo ya haya yote, ni kujikuta tukiishi maisha yasiyo na utimilifu. Maisha yasiyo yetu.

Pengine uliwahi kusoma maneno ya mtu mmoja aitwaye Albert Gray yanayosema:

The successful person has the habit of doing things failures don’t like to do. They don’t like doing them either necessarily. But their disliking is subordinated to the strength of their purpose.

Nukuu hii imekuwa na maana tofauti kwangu. Kwamba kile ninachokiona kwamba kana kwamba hakivutii kukifanya, ndicho chaweza kufanyika utimilifu wa ninachokikusudia.

Mambo gani ambayo unajua ni ya muhimu yafanyike lakini unayaahirisha? Ni mangapi mazuri unayakosa kwa kule tu kukwepa kulipia gharama ya kuyatekeleza hayo unayoyaona kuwa ni ya muhimu? Je, kama ungeamua leo kukubali kulipia gharama ya kutekeleza mambo hayo, hatua ngapi ungepiga mbele?

Nikijichukulia mfano mimi, ninajua kabisa kuwa huwa ninapokwepa kufanya mambo fulani fulani ambayo nina hiari ya kuyafanya ama kuyaacha, lakini ni ya muhimu, mwishowe hukumbana na gharama kubwa za kulazimika kufanya kitu kile kile nilichokiahirisha mwanzoni ama kuchelewa kutimiza ninachokusudia.

Lakini pale ninapoamua kuweka chini hali ya kuona gharama (za muda, uhuru, kurekebisha ratiba ya siku nk) kama kitu kilichojuu ya kusudi lililo mbele yangu, mambo hubadilika.

Gundua kile unachokikwepa na chukua maamuzi ya kukifanya. Jifunge kibwebwe na usirudi nyuma. Kusudia kutanguliza kusudi mbele ya hizi zinazoonekana kama gharama za muda tu tusizovutiwa nazo sana. Utashangaa kitakachotokea ambacho hakikutokea siku zote kwa sababu tu “ulikwepa kuamua!”.

Maoni

  1. Asante sana Mkuu kwa hili!

    Yani hapa nilipo kuna mengi kweli nimekwepa na hii imenipa munkari mpya kuyaingia kichwa kichwa!

    Kwa bahati mbaya kila mwaka Mpya huwa nakata shauri kuingia mambo kichwa kichwa lakini mara nyingine hata ndani ya mwezi huohuo wa kwanza naanza kukwepa mambo!:-(

    DUH!:-(

    JibuFuta
  2. Mazowea ya kuahirisha mambo ni utumwa, amesema mmoja wao mie hapa!


    Naam, Mkuu Bwaya, mtu atakayenipa dawa ya kuacha kuahirisha mambo, hata milioni nampa kabisa!


    Lakini mpaka leo, mie na watumwa-wenzangu sidhani tumekwishapata tiba!

    Labda wasomaji wengine wanaweza kutufafanulia zaidi ila tupate matibabu tena nadhani hata naye Mkuu Kitururu atafaidi hapo! Si ndio katika hali kama hii ya kuadimika kwa tiba waliposemea Wahenga: KILA SHETANI ANAMBUYU WAKE?




    Wakati tunaposubiri tiba yetu, niruhusu tafadhali Mkuu Bwaya niwafariji waahirishaji wenzangu juu ya baadhi ya njia za ?kumudu? (HOW TO MANAGE THE CONDITION).

    Napakumbuka Ilala Dar es-Salaam mwaka 1992 nilipopewa MWAKA MZIMA kwandika ripoti yangu juu ya utafiti niliokuwa naufanya ili nifaulu DIPLOMA ya Wandishi wa Habari huko TANZANIA SCHOOL OF JOURNALISM, au kama inavyoitwa siku hizi, "School of Journalism and Mass Communication-SJMC" http://www.sjmc.udsm.ac.tz/SJMC-About.php)




    Amini usiamini nilianza kwandika saa kumi ya jioni.

    Wanafunzi wenzangu Idi Rashid Mchatta, Stephen Lyimo, Karim Besta, na wengineo wengi sasa marehemu kama Mwafrika-Kusini-Mwenzangu Monde Tshongweni walipokwenda kulala hapo baadaye mie nikaendelea tu nakuchapa hiyo ripoti usiku mzima.

    Saa nne asubuhi iliyefuata ilikuwa ni muda wa mwisho kumpa Mwalimu Mkuu Bwana Maurice Samwilu Mwaffisi hizo ripoti.

    Mimi mwenyewe nilikuja kushangaa kwani ripoti yangu na ile ya rafiki yangu Bw Herald Tagama, pamoja na ?utetezi? wake (THESIS DEFENCE)ndizo zikawa juu zaidi kiasi cha kutangazwa katika vyombo vya habari Tanzania! (Ilikuwa mara ya kwanza Msouth-Afrika, tena labda mwanafunzi yoyote yule asiyeMtanzania, kupata FIRST CLASS).



    Kwa ujuzi wangu mimi mwenye huo udhaifu wa kuahirisha mambo, lile joto (ADRENALIN RUSH)la kujua mtu uko hatarini usipomaliza kwa wakati, ndilo linakutia nguvu za kiakili kuimaliza hiyo shughuli tena vizuri kuliko pale ungeanza mapema zaidi.

    Yapo lakini muhimu ya kuzingatia:

    1. Uwe na afya nzuri kimwili (PHYSICAL FITNESS) vilevile kiakili (EMOTIONAL STABILITY AND MENTAL SOUNDNESS IN GENERAL).

    2. Uwe na uhakika na ?namna? (SKILLS/KNOW-HOW) ya kufanyia hiyo shughuli. Kama ikiwezekana uwe bingwa wa hizo SKILLS.

    Mfano tena wa 1992, asingekuwepo mwanafunzi-mwenzangu Bi Beatrice Bandawe aliyenilazimisha daima kushika adabu, ningekuwa mimi ndio bingwa wa darasa letu kwa kupiga chapa (TYPING SPEED AND ACCURACY).




    Kwahiyo, Mkuu Bwaya, mimi ninamaoni ya kwamba hata ikiwa kama sasa hivi bado hatujapata tiba ya ugonjwa wetu wa kuahirisha, tusiogope kujitangaza sisi ndio wadhaifu wa hayo mambo. Labda tena ni sifa kwa upande mwingine!

    Vilevile tuwe wajanja kama yule mtoto aliyezubaa na badala yakumchorea mwalimu sungura, yeye alichora jabali.

    "Je, hii ndiyo sungura uliyechora wewe, Mtoto?" Mwalimu aliuliza kwa gadhabu.

    Mtoto kujibu: "Mwalimu, tafadhali tulia kwanza! Sungura yupo, bali amejificha huko nyuma ya jiwe!"

    JibuFuta
  3. Ahsante kaka Bwaya!ninapoyapangia siku naona kama mbali, muda wake ukifikia sasa, unaanza kuchagua hili si lalazima leo nitalifanya nikipata nafasi.Nakuna mengine mapya nazalisha!.mmmhh kazi kwelikweli!.

    JibuFuta
  4. Ni mgonjwa mwandamizi mimi kwa hili, na imefika wakati najiogopa kwa hilo. Tiba ikipatikana tutapona wengi. Haule

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?