Je, jamii ingekuwaje bila dini?


Hebu tutafakari ingekuwaje bila dini. Ili kusaili hali hiyo ya kufikirika, hebu tuyasaili masuala haya kuona ikiwa dini inatufaa ama ndilo tatizo linalotukabili.

Je, dini zinamsaidia binadamu kumjua Mungu?

Je, bila dini tunaweza kuwa na uhusiano na Mungu?

Je, dini zinasaidia kujenga jamii ya watu waadilifu na wanyoofu?

Je, dini zinawasaidia waumini wa dini moja kuheshimu mitazamo ya waumini wa dini nyingine?

Je, dini zinasaidia kujenga upendano katika jamii?

Je, dini zinapunguza unafiki katika jamii?

Je, dini zinapunguza migongano na misuguano katika jamii?

Dini ni nini? Ni kumjua Mungu? Ni chama cha wanaomtafuta Mungu? Dini na imani vinauhusiano? Kwa nini dini?

Mimi nafikiri tatizo ni dini zenyewe na sio watu. Wewe unafikiri nini? Tungekuwaje bila dini?

Jumapili njema.

Maoni

  1. Sidhani unaweza, Ndugu yangu, kwongelea dini bila kuhusisha suala la Mungu kwa namna moja au ingine.

    Mimi kinachonivutia sana katika masuala haya ni misingi kadhaa wa kadhaa.

    1. Inasemekana hata wale [wanaosema Mungu hayupo] (ATHEISTS) nao wanadini yao... hiyohiyo ya ATHEISM.

    2. Dini inaweza ikawa dalili ya ugonjwa wa akili. Akianza mtu kutumikia dini badala ya dini kumtumikia yeye ujuwe, kwa mawazo yangu, panamatatizo hapo kidogo kichwani. Maana yake dini sio Mungu, bali ni moja tu katika namna tena nyingi sana za kuyafikia matakwa yaMungu.

    3. Mimi binafsi naamini Mungu yupo; lakini huyo Mungu ni wewe hapo Bwana kwani tusingezumzia hii TOPIC nzuri isingekuwa kama Mungu amekujalia au kukupa msukumo wanzilishe TOPIC hii. Vilevile masomo mengi matakatifu yahimiza binadamu ndiye mtoto waMungu. Mtoto waMungu siMungu naye?

    4. Ya mwisho nayapenda sana maisha aliyekuwa anaishi jamaa fulani wa Ufransa naye kwa jina niFrançois-Marie Arouet (21 November 1694 – 30 May 1778).

    Huyo basi kwa jina lingine ni Voltaire. Vilevile anavuma duniani kwamsemo wake aliposema ["Mungu yupo hayupo binadamu sisi tunamhitaji hivyohivyo maishani mwetu."]


    "Si Dieu n'existait pas, il faudrait l'inventer"

    ("If God did not exist, it would be necessary to invent him")

    http://en.wikipedia.org/wiki/Voltaire

    JibuFuta
  2. Dini zisingekuwepo, imani ingeendelea kuwepo. Nadhani watu wanatumia imani zilizopo katika kufanya dhana ya dini iendelee kuwepo.

    Hivi kabla ya Ukristo na Uislam kuletwa Afrika hususani Tanzania, mababu walikuwa na Dini au walikuwa na imani tu ambazo leo hii ndizo ziitwazo za kishenzi?

    Dini ni bahasha ya imani, waweza kuibeba (imani) bila bahasha hii, na ukafika kule kwa kiimani unapotaka kufika.

    Tatizo kubwa nilionalo mimi ni kuwa, watu huanza kuhatambulishwa kwanza dini kabla ya kuitambua imani yake hasa. Basi kwa kadiri mtu anavyokuwa katika dini fulani, anajikuta anaamini yaendeleayo katika taasisi hiyo kwa maana ya kurithishwa imani, kitu ambacho mimi naona ni kosa kubwa sana. Ndio maana wale wanaotelekeza vile walivyorithishwa huitwa "wasaliti".

    Kwangu mimi, dini si kitu bali kile ninachokiamini ilimradi tu nikiaminicho hakidhuru ubinadamu kwa namna yoyote.

    JibuFuta
  3. kwa kweli dini ni kizungumkuti. pamoja na mengine mema dini zikiachwa zitawaliwe na jazba na ujuaji mara nyingi ndio chanzo cha vurungu na mafarakano

    JibuFuta
  4. Swali lako linaonesha kana kwamba, dini imekuwa msaada mkubwa sana katika jamii, inaonesha kwamba dini imesaidia sana kuleta hali ya utulivu kwa jamii yetu. Sawa kabisa. Ni kweli. Lakini umelitafakari kwa makini jambo hilo?

    Dini badara ya k...uwa msaada mkubwa katika jamii yetu, badala yake imekuwa kama sehemu ya kujificha watu waovu, waliojaa husuda na wazinifu sugu pamoja na wachawi watu ambao ni sumu kubwa katika jamii yetu.

    Nisemapo kuwa watu hao wapo katika dini zetu na hapa haijalishi kuwa ni dini gani, eiza Uhindu, Tao ama Ukristo au Uislam, katika dini hizo kumejaa waovu na waovu japo si wote. Watu wamekuwa hawana hofu kwa MUNGU, bali kwa mwanadam.

    Mfano, Mtu anaweza akawa anatembea tembea, mara akakutana na Ubao wa Jeshi umeandikwa, "Ni marufuku kupita eneo hili, ni eneo la Jeshi" basi nakuambia ndg Mtangazaji ya kwamba, mtu yule mara moja atageuza miguu, ama usafiri wake na kuanza kurudi alikotoka.

    Sasa mtu huyo huyo tena chukulia kuwa ni mtu wa dini. Akasoma katika kitab chake pengine kuna amri ya MUNGU wake imesema, "Usiwe na miungu mingine ila Mimi" basi mwanadamu yule hatoiogopa amri hiyo na ikitokea kuna miungu, anaabudu na wala hana hofu.

    Najaribu kukueleza hayo mtangazaji ili kuonesha jinsi gani dini ambavyo haina msaada wowote katika jamii yetu.

    Na kwa kujibu swali lako kwamba, "Jamii ingekuwaje bila dini" mimi nasema ya kwamba, jamii ingekuwa shwari tu tena sana tu. Kwa maana kuna sheria zinazolinda hali ya amani katika jamii yetu.

    Mtu haogopi kuuwa kisa dini, bali anaogopa kuuwa kwa kuwa anajua kama akiua, basi na yeye pia kuuliwa, ama kufungwa jela maisha.
    Mtu pia anaogopa kubaka, si kwa hofu ya MUNGU, Bali ni kwa sababu kuna sheria inayosema kama ukibaka, ni jera miaka 30.

    Mwanadamu hana hofu kabisa na hukumu za baadaye zinenwazo na BWANA MUNGU. Anaogopa tu zile hukumu za adhabu anazoziona kwa macho, lakini hizi za kusimuliwa, wala hazimpi shida.

    Labda kama ungeuliza ya kwamba, "Jamii ingekuwaje bila sheria", ama hapo pangekuwapo shughuli kubwa, mauaji yangalitapakaa kila sehemu.

    Nahitimisha kwa kuiasa jamii ya kwamba, ni kheli kama wangejenga hofu zao katika sheria za MUNGU, Hapo patakuwa safi sana. Maana kama tukiwa na hofu na amri za MUNGU, Nchi yo yote tutakaa kwa amani, kwa maana hizo nchi zenyewe zimeweka izo sheria kutoka katka sheria za MUNGU. Dini zetu bila shaka zote hutufundisha mambo mema.

    Tusiogope mwanadam, bali tumwogopeni MUNGU na amri zake. Na amri zake wala si nzito. Ni kutokuwa na Miungu wengne isipokuwa YEYE, Kutojifanyia sanamu ya kuchonga, Kutokulitaja Jina lake bure, Kuitunza sabato yake ya jumamosi, kuwaheshimu wazazi, Kutoua, Kutozini, Kutoiba, Kutomsemea mwenzako uongo na Kutotamani vya mwenzako. Kama utataka kuzijua kwa ufasaha, waweza ukazisoma katika Kitabu cha Biblia kitabu cha Kutoka na sura ya 20. Amri rahisi kabisa. Kama jamii itakuwa na hofu na amri hizo, tunaweza tukawa na jamii yenye baraka za BWANA.

    Tena sana zaidi. Jifunzeni kwa hao wazitunzao, muone ile mibaraka waipatayo, kwa maana Mwenye amri aliahidi mibaraka ya kutosha kwa hao watakaozitunza. BWANA awabariki na kuwalinda. Ila ondoka na hili, "Jamii bila sheria, haiwezekani"

    JibuFuta
  5. Nimedokezwa kuwa wote walioingia mikataba mikubwa ya kilaghai kama vile wa Richmond na IPTL wana dini na waliapa kwa kutumia dini zao kuwa watakuwa viongozi waadilifu.

    Wengine almanusura wapigane kule Dodoma wkt wa kumchagua Askofu atakayeongoza imani ya dini yao.

    Kule palestina na Israel yasemekana kuna wengine wamebarikiwa na Mungu wao kuua wanaopingana na imani ya dini zao.

    Hakika nawaelezeni Mungu hana na hajawahi kuwa na dini.

    Dini ni utaratibu wa watu wachache waliojiwekea utaratibu wa kuwatawala watu wengine akili zao.

    JibuFuta
  6. Nimedokezwa kuwa wote walioingia mikataba mikubwa ya kilaghai kama vile wa Richmond na IPTL wana dini na waliapa kwa kutumia dini zao kuwa watakuwa viongozi waadilifu.

    Wengine almanusura wapigane kule Dodoma wkt wa kumchagua Askofu atakayeongoza imani ya dini yao.

    Kule palestina na Israel yasemekana kuna wengine wamebarikiwa na Mungu wao kuua wanaopingana na imani ya dini zao.

    Hakika nawaelezeni Mungu hana na hajawahi kuwa na dini.

    Dini ni utaratibu wa watu wachache waliojiwekea utaratibu wa kuwatawala watu wengine akili zao.

    JibuFuta
  7. mcharia na katawa nimewapenda kama mkokichwani mwangu vile safi kabisa na mimi nasemaga kuwa hakuna mungu ila ni kutiana hofu tu zaidi kama mlivyosema ni kuzitii amri na sheria

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?