Shuzi la mwenye nyumba halinuki?

Kwa wale wenye uzoefu huu, tusaidiane kufikiri.

Baba akichafua hewa (ashakumu si matusi akijamba) mbele ya wageni na wanae, nani hasa huwajibikia tendo hilo? Yeye, ama wanae? Manake mara nyingi hukosi kusikia mzee akijiwahi: ' Nyie watoto, sipendi kabisa hiyo tabia yenu...nendeni mkacheze nje.'

Watoto pamoja na kuujua ukweli kwamba mtumiwa halisi ni baba yao, ambaye anawasingizia wao, huenda nje wakilalamika '...baba sio mimi...mi'shijajamba labda Mangi...!'

Je, kuna ulazima wowote wa baba kukiri kuuwajibikia uchafuzi wake huo wa hewa badala ya kuwabebeshea wanawe?

Maoni

  1. Binafsi sioni sababu ya kuwasingizia watoto. Umenikumbusha kitu hapa kwani hapa swedeni kujamba si kitu cha ajabu lakini kucheua mbele za watu si vyema. kazi kwelikweli..

    JibuFuta
  2. topic za simon kitururu hizi ngoja tumsubiri aje

    JibuFuta
  3. Kamala, mimi si mwenye nyumba.

    JibuFuta
  4. Kimsingi baba ni lazima awajibike moja kwa moja,ishu inakuja namna ya kuwajibika.Baada ya kuweka wazi hakuna kitakachofuata zaidi ya aibu,akikaa kimya,tatizo ni palepale,kashachafua hewa, ukweli ni kwamba wageni hawawezi kuhoji,watavumilia.


    Afrika utamaduni huu upo sana,lakini wakuu hawa wa kaya wawe makini kwani kwani kuna watoto wengine hawana dogo, wanamlipua baba hapo hapo.Ni jambo jema, kwa sababu watoto nao wana haki ya kutambulika kuwa wana heshima, mtoto kama huyu anaonyesha ni MZALENDO kwa thamani na utu wake na pia anawajali watoto wenzake.kwani ni mtetezi wa kweli.

    JibuFuta
  5. Kaka Bwaya naomba nikukumbushe. hivi ule mjadala wetu wa dini umeishia wapi?

    JibuFuta
  6. Je huyo baba pia anayo tabia ya kuchafua hewa ikiwa watoto hawapo? Na je hua anamsingizia nani? mimi ninavyo fikiria hawa watoto wanasingiziwa na baba yoo na mgeni ndio kachafua hewa lakini baba anamfichia aibu kwa watoto.

    JibuFuta
  7. Nafikiri namna nzuri ya kutafakari hichi unachokisema ni kwenda mojakwa moja kwenye hoja. Kiongozi wa taasisi nchi akiharibu, nani wa kumnyooshea kidole? Jibu rahisi atatafutwa kafara wa kumfichia aibu mtawala fisadi ambaye kwa maana hii akiumbuliwa nchi inatetemeka. Read between the lines

    JibuFuta
  8. Chacha Wambura31/8/09 1:55 PM

    Mbusi wa kafara a.k.a BAngusilo hayuko kwenye ushuzi tu hata chumbani na kanithani na kwenye njii n.k

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia