Je! Yesu ni Mungu?

Haya ni maoni ya mdau asiyependa jina lake lijulikane. Nimeyatundika hapa kwa sababu ya uzito wa anachokisema. Tafadhali soma na kama unaweza changia maoni yako tuelimike.

Nimshukuru sana kwa kutumia muda wake kuandika maoni yake na hapa namnukuu:

MAKANISA ya Kikristo yanafunza ya kuwa Yesu Kristo si kama kuwa ni Mwana wa Mungu tu, bali hakika ni Mungu khasa. Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ni mmoja. Watatu katika mmoja, na mmoja katika watatu. Wote ni wa milele, wote ni sawa. Yesu ni Mungu, na Mungu ni Yesu. Hiyo ni imani ya Kikristo, ambayo inaaminiwa na karibu Wakristo wote. Hebu tuifunue Biblia tutazame inasema nini katika jambo hili?
Mt Paulo katika barua yake ya kwanza kuwapelekea Wakorintho aliandika:

Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi.
1 Wakorintho 15.15

Juu ya kuwa Paulo anaambiwa ya kuwa akiamini kuwa Masihi (yaani Kristo) na Mwenyezi Mungu ni kitu kimoja hapa anasema: "Tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo." Ikiwa Mungu kamfufua Kristo, hawawezi kuwa wote wawili hao ni mtu mmoja. Mmoja alikuwa ni mtenda, mfufuaji, na wa pili alikuwa ni mtendwa, mfufuliwa. Kama Kristo ni Mungu mwenye uwezo wa kufufua basi maelekeo ni kusema: "Kristo kajifufua", sio kafufuliwa. Mwenye kufufuliwa ni mfu asiyejiweza kitu.
Katika kitabu cha Matendo ya Mitume inasimuliwa kuwa Mt Stefano alisema aliyoyaona yaliyo mbinguni. Alisema:

Tazama! naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
Matendo 7.56

Mwana wa Adamu ndiye Yesu, na kwa jina hilo ndio mwenyewe akipenda kujiita, sio Mwana wa Mungu. Hapo basi huko mbinguni Stefano anasema anamwona Yesu kakaa mkono wa kulia wa Mungu. Mwenye kukaa mkono wa kulia wa fulani hawezi kuwa ndiye yule yule fulani. Hayo ni maelezo ya mbinguni. Ni wazi basi kwa ushahidi wa Biblia kuwa Yesu hakuwa Mungu mbinguni kama alivyokuwa si Mungu duniani.
Yesu alipokimbilia kwenye Mlima wa Zaituni na huku akisakwa na Mayahudi alijitenga na wanafunzi wake. Huko faraghani aliomba hivi:

Ee Baba, ikiwa ni mapenzi yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi yangu, bali yako yatendeke. Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu.
Luka 22.42-43

Hapa tunaona mambo matatu muhimu:

Yesu anamwomba Mungu. Yesu anamwabudu Mungu. Wawili hao ni mbali mbali, na vyeo vyao ni mbali mbali. Yesu ni mtumwa mnyonge mwenye kuomba na kuabudu. Na Mungu ni Mwenyezi Mungu mwenye uwezo wote na mwenye kustahiki kuabudiwa pekee, hata na Yesu, mwenye kutakiwa msaada pekee, hata na Yesu.
Mapenzi ya Mungu ni mbali na yale ya Yesu. Yesu hataki kuuliwa, ananyenyekea na kuomba kwa Bwana wake: "uniondolee kikombe hiki" cha mauti. Yesu hana azma hata chembe ya kufa msalabani, kifo cha mhalifu, kifo cha laana kama maadui zake Mayahudi walivyoazimia kumpatilisha nacho. Lakini anakiri kuwa ni mapenzi ya Mungu sio yake yeye yatendeke. Yeye hana hila wala nguvu za kuzuia kudra ya Mwenyezi Mungu.
Yesu, Mwana wa Adamu, anakata tamaa. Imani inampunguka. Kavunjika moyo. Ikabidi "Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu."
Jee, yaelekea kuwa Yesu ndiye Mungu? Yaelekea kuwa yeye na Mungu kuwa ni sawa? Kama upo wasiwasi wo wote wa kujibu hayo, mwenyewe Yesu anajibu kama anavyo hadithiwa na Yohana kuwa kasema:

Baba ni mkuu kuliko mimi.
Yohana 14.28

Na mwishoni naye yupo msalabani:

Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, Mbona umeniacha?
Mathayo 27.46

Yafaa hapa tujiulize: Yesu akimlilia Mungu gani hapo msalabani ikiwa naye mwenyewe ni Mungu? Au nini alikusudia aliposema: "Mungu wangu naye ni Mungu wenu"? Maneno hayo kama yanaonyesha cho chote basi yanaonyesha unyenyekevu wa Yesu mbele ya Mungu wake. La kustaajabisha ni kule kukata tamaa kwake na kuvunjika moyo. Huwaje mtu wa imani, licha ya nabii na mwana pekee wa Mungu, akate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Ama kuwa Mungu akate tamaa na Mungu, na kumyayatikia: "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha", ni jambo ambalo halimkiniki kuwa.
Kwa uthibitisho ulio wazi Biblia inatwambia kuwa Yesu si Mungu, wala Mungu si Yesu."


Mwisho kunukuu.

Maoni

  1. Hapa mimi sipagusi. Namsubiri kwanza Kamala aanze.

    JibuFuta
  2. Mimi naamini ya kuwa Yesu ni mwana wa Mungu.

    JibuFuta
    Majibu
    1. YESU ANA VYEO VYOTE MWANA WA MUNGU, NA BADO NI MUNGU...Lakini kuna jambo la kujua KWANINI anaitwa Mwana wa Mungu...Kuna siri kubwa sana ambayo inafahamika pia na watumishi wa Mungu makini.. Isome hapa >>http://wingulamashahidi.org/2019/01/02/mwana-wa-mungu/

      Futa
  3. yasinta unaamini hivyo au unaaminishwa hivyo?

    Yesu anaweza awe Mungu na Asiwe Mungu pia kutokna na tafsiri yako. cha Muhimu nu kukua kiroho badala ya kubishana. si

    JibuFuta
  4. Mie sie mwanazuoni katika masuala hayo. Mbawa zangu nimezikunja

    JibuFuta
  5. Hivi Yesu ni Mungu Mwana wa MOLA au ni Nabii Issa?
    DUH !

    Na nyege kweli ya kuendelea kuloloma lakini nasita!:-(

    JibuFuta
  6. Chacha Wambura31/8/09 1:48 PM

    Hapo mwanzo alikuwepo NENO...naye neno alikwapo kwa MUNGU, naye neno alikuwa Mungu.

    Je huyo NENO ndo YESU a.k.a Nabii Issa bin Maryamu?

    JibuFuta
  7. Wengine wetu swala hili halitukoseshi usingizi... historia ni historia!

    JibuFuta
  8. haya mambo ukiyafuatilia kwa undani utagundua mambo mengi. la msing kila mmoja ashike alichokishika

    JibuFuta
  9. kweli kabisa yesu si MUNGU?

    JibuFuta
  10. Kwanza achanikujulishe kuwa nasi tuna amini kuwa MUNGU ni moja kwa mjibu wa qur'ann16:51 nafurahi kuona ume tumikisha aya za BIBLIA TAKATIFU ina maana unaamini pia BIBLIA.Marko12:29.lakini kweli YESU si MUNGU?acha nikuulize swali ukigundua kupitia qur'ann na BIBLIA kama yesu ni MUNGU utaamini?aya jibu swali hizo kisha nikueke chuoni,darasani.na kusihi

    JibuFuta
  11. Yesu in mungu mkuu wakristo hawabahatishagi soma tito2:13 inasema tukilitazama tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa kristo yesu,Mungu mkuu na mwokozi wetu mstari wa14amhaye alijitoa nafsi yake kwaajili yetu,ili atukomboe na maasi yote na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe alafu soma kolosai1:16-17inasema:-kwakuwa ktk yeye vitu vyote viliumbwa,vilivyo mbinguni na vilivyo katika juu ya nchi,vinavyoonekana na visivyoonekana ,ikiwa ni viti vya enzi ,au usulutani au enzi,au mamlaka ,vitu vyote viliumbwa kwa njia yake endelea na 17mstari ukitoka hapo soma yohana 1:15inasema:hakuna mtu aliyemwona mungu wakati wowote,Mungu mwana pekee aliye katika kifua cha baba huyu ndie aliye mfunua.tukirudi nyuma kwenye yohana 1:1-5tunaona kuna tafsili kama mbili yesu anatafsirika katika makundi mawili (1)Neno na lapili ni Mungu muumbaji na ndani yake Yesu kuna uzima ebu nililete kama lilivyo yohana1:1-5hapo mwanzo kulikuwako Neno,nae Neno alikuwako kwa Mungu naye Neno alikuwa Mungu.huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.vyote vilifanyika kwa huyo wala pasipo yeye hakukufanyika chochote kilichofanyika.ndani take ndimo ulimokuwamo uzima nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.nayo nuru yang'aa gizani wala Giza halikuliweza.tunasoma tens kwenye yohana3:19-20 inasema: na hili ndiyo hukumu;yakuwa nuru imekuja ulimwenguni,na watu wakapenda Giza kuliko nuru kwa maana matendo yao yalikuwa maovumaovu kwa faida yako soma yohana1:8-9au ukiweza soma yote kwa msaada zaidi muda hautoshi kwa habari ya Uungu wa Yesu maandiko yapo mengi sana yanayosibitisha mnakwama wapi?alafu ni kwamba sifa ya uungu kuu ni uumbaji sifa tunaona pasipo yeye hakukufanyika kitu pili ni upendo yesu alitupenda wanadamu hata akaona heri afanyike kuwa laana kwa ajili ya wanadamu 3ni uzima hivi vyote amevibeba yesu ana kila sababu za kuitwa mungu asenteni

    JibuFuta
  12. Nyie bishaneni lakini mwisho wa siku kila mtu atahukumiwa kivyakeee😜😜😜😜😜😜😜😜😜

    JibuFuta
  13. Ni vizuri kufahamu kwanza kwanini Yesu Kristo alikuja duniani, ukishafahamu kwanini alikuja ndipo utaelewa kama yeye ni Mungu au la!..Biblia inatuambia Siri ya Utaua ni KUU..

    1 Timotheo 3:16 "Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu"

    Sasa huyo Mungu aliyedhihirishwa katika mwili hapo ni Bwana Yesu, akahubiriwa katika mataifa na akachukuliwa juu..huo ndio Msingi wa kumwelewa Yesu..

    Fungua linki hii inaelezea kwa urefu zaidi >>http://wingulamashahidi.org/2018/07/17/kwanini-yesu-kristo-alikuja-duniani/

    JibuFuta
    Majibu
    1. Biblia imeingezwa na kupunguzwa why unaona kuna tofauti nyingi

      Futa
    2. Jeremiah 8:8 wasemaje nyie mna akili angalia mikono ya waandishi yamefanya maneno kua uongo

      Futa
  14. maandiko yoote hayoo yanatoka katika kitabu kimojaa kiitwacho bibiliaa. lakinii kuna utofautii katika maandikoo . ukisoma baadhi yanakubali kuwa yesi n mungu na mengine yanakaataa. sasa swali ni andiko lipi ni la kwelii na lipi sioo lakwelii?? na kama kuna maandikoo ambayoo si yakwelii, inamaana bibliaa inadanganyaa??

    JibuFuta
  15. kuna watu wanamfuata Paulo alieua wanafunzi wa Yesu kwenye masinagogi,swali ni je kwanini paulo aluwaua wanafunzi wa yesu na mda huo huo anakuja na hoja ya kusema kua yesu ni mungu mkuu??swali je yesu alisema uongo kua baba alie mbinguni ndie mkuu..?

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia