Operesheni ya kilimo cha barabara

Nimerejea tena baada ya kumalizana na Kaizari. Nimepita Moshi kwa ufupi Jumamosi, kisha nikaja Singida, kupitia Arusha.

Njiani nilishuhudia 'maendeleo' ya kilimo cha barabara. Barabara ya Minjingu-Babati inaparurwa kwa kasi. Ile ya Babati - Katesh - Singida nayo haiko nyuma, mkandarasi yuko 'saiti.'

Nakumbuka tukiwa Magugu, abiria mmoja niliyebahatika kukaa naye, mtu wa makamo akaniambia; 'Kijana hivi unajua kwa nini barabara hii inajengwa kwa kasi hivi?' Nikamjibu; '...mzee sina hakika kama najua'
Akafunga gazeti alilokuwa analisoma, akanitazama akisema: '...hii ni operesheni pumbaza kuelekea uchaguzi.' akaendelea; '...Nchi hii haitawaliwi kwa mipango ya muda mrefu. Kila kinachofanywa kina nia ya miaka isiyozidi mitano..' Barabara hii italimwa wee mpaka kampeni zifike, waitumie kama mradi wa kuvunia kura, na usishangae mambo yakiishia hapo hapo...'

Niko Singida mpaka mwezi wa tisa.

Maoni

  1. Karibu saaana. Karibu sana Mkuu.
    Blessings

    JibuFuta
  2. Mkuu, sitaki kuielezea furaha yangu kwa kurejea kwako katika harakati.

    Nakubaliana na huyo mzee.

    Mwenye macho haambiwi tazama. Subiri uone!

    JibuFuta
  3. Hekaheka ziko nchi nzima. juzi nilikuwa mbeya. kipande cha barabara kunzia sehemu panaitwa daraja mbili mpaka ipogolo (hata mbele kidodo) ni heka heka ya 'kilimo' hicho. miaka yote sie wakazi wa huko tumepiga kelele weeeee wapi. saa hizi saa kumi na mbili ndio wanakumbuka. Huko mbeya hakujachacha. nenda uyole uone mtibwiriko wa kupanua huduma ya maji kutoka kiwira. uyole yoote vurugu tupu hamna hata sehemu ya kupita na taksi jinsi barabara zilivyofululilwa kupitisha mabomba. lakini ni siku nyingi sana tulisema tunataka maji kutoka kiwira, wamekumbuka leo. hata hivyo sio vibaya ilimradi mabomba hayo yasiwe na hewa, yawe na maji

    JibuFuta
  4. Hekaheka ziko nchi nzima. juzi nilikuwa mbeya. kipande cha barabara kunzia sehemu panaitwa daraja mbili mpaka ipogolo (hata mbele kidodo) ni heka heka ya 'kilimo' hicho. miaka yote sie wakazi wa huko tumepiga kelele weeeee wapi. saa hizi saa kumi na mbili ndio wanakumbuka. Huko mbeya hakujachacha. nenda uyole uone mtibwiriko wa kupanua huduma ya maji kutoka kiwira. uyole yoote vurugu tupu hamna hata sehemu ya kupita na taksi jinsi barabara zilivyofululilwa kupitisha mabomba. lakini ni siku nyingi sana tulisema tunataka maji kutoka kiwira, wamekumbuka leo. hata hivyo sio vibaya ilimradi mabomba hayo yasiwe na hewa, yawe na maji

    JibuFuta
  5. Nashukuru kwa kupita kwenye ukumbi wangu na kuacha ujumbe maridhawa

    JibuFuta
  6. Hizo barabara ukiongeza na pea za kanga, vitenge, kilo za sukari na chumvi, mabati na baisikeli watakazopewa wapiga kura - jamaa watashinda bila shaka. Halafu baada ya hapo ni business as usual.

    JibuFuta
  7. Huku Moshi nako kapeti za uhakika zawekwa.Barabara ya kutokea Kcmc hospital hadi hospitali ya misheni ya kibosho inawekwa kapeti la kueleweka,nimeshasikia baadhi ya watu wakisifia sana serikali ya Kikwete.Kwa maana hii hawaelewi kabisa fomesheni ya NNE kwa MOJA.


    Kwa upande mwingine kuna mtu aliniambia kuwa baba yake ambaye ni mstaafu amewekewa pesa mara mbili zaidi ya Aliyozoea kupokea, sasa sijui pesa hiyo ya zaidi iliingia kwa bahati mbaya au la? Jamaa huyu alimuuliza baba yake huyu panapo majaliwa atampa nani kura, alisema hamna zaidi ya Kikwete.


    Kwenye vyombo vya habari, yatangazwa kuwa asilimia kubwa ya watu wana imani kubwa na Kikwete,sijui hili linaukweli gani, sample ya watu waliotumika sijui walipatikana vp.Yote kwa yote,ipo vita ya chinichini.



    Yote haya yawezekana vipi,kwa nini akili zetu kutekwa namna hii,danganyatoto hizi tunazozikubali zinatuchora namna gani sisi watanzania?
    Wakati wa uchaguzi kila dalili zikionyesha kuwa upinzani utachukua kiti cha uraisi na matokeo yakatangazwa ndivyo sivyo, je watanzania tutafanya nini?
    Da! Naweza kuandika hapa mpaka kesho.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?