Ijumaa, Agosti 21, 2009

Dini na maoni ya wadau

Ninazo nyaraka kadhaa zilizotumwa kwangu na wadau wa ule mjadala wa dini. Zinafikia kumi.

Wengine hawachelewi. Wamekuja na tuhuma nzima nzima kwa watu, ama vikundi vya watu.

Ninatafakari namna muafaka ya kuwasilisha maoni yao bila upendeleo.

Hata hivyo, ningependa kuwashauri wadau wa dini, kuzungumza mambo ambayo wana hakika nayo, yenye hoja, ambayo hataibua ugomvi usio na tija katika kutuelimisha.


Kwa wale wasioridhika bila kutukana, ujumbe wangu kwao: Dini isipoweza kukusaidia kuitetea kwa lugha rahisi, hiyo haiwezi kuwa pungufu ya ubatili mtupu.

Maoni 1 :

  1. Naona umejihami kabisa na matusi ya wafuasi wa dini!!

    JibuFuta