Mafanikio ni umiliki wa muda wako



Mafanikio ni nini?
Ajira ya uhakika?
Uhakika wa mapato?
Uhakika wa pensheni?
Ongezeko la muamala mwisho wa mwezi?
Tarakimu za shilingi kuongezeka?
Kwa gharama ya kunyang'anywa muda wako?
Si unajua?
Kadri ziongezekavyo ndivyo uuzavyo muda wako?



Mafanikio....
Ni madaraka kazini?
Madaraka yaendanayo na ubize?
Kutwa u ziarani? U angani kikazi?
Waondoka alfajiri, warudi usiku?
Wanao hawakuoni?
Mwenza yu mpweke?
Haidhuru...
Nyumba yanukia noti sio?
Shilingi bila muda, kazi yake nini?

Muda na familia ni sehemu ya mafanikio. Noti ziendazo sambamba na kukunyang'anya fursa hii, faida yake nini? |Picha ya blackmarriageworks.com/







Mafanikio...
Ni kuongezeka kwa kibaba?
Ankara zalipika kibaba kinabaki?
Ni uhuru wa muda wako?
Uhuru wa kujenga familia kwa karibu?
Mwenzi achekelee? Wana wasome?
Uifaidie jamii?
Sadaka utoe?
Wenye shida wakukimbilie?



Si unajua lakini...?
Bila shilingi hayo si mepesi?
Shilingi yatatua vingi
Muda bila shilingi, wa nini?
Muda unao unachotatua hakionekani?
Na wadai umefanikiwa? Kivipi?


Hujanielewa...
Mafanikio ni kuwa na vyote
Ni thamani ya muda wako
Hiari ya matumizi ya muda wako
Mafanikio ni...
Mfumo ukutumikiao wewe
Mfumo ukupao muda wako wote
Si tu kulipa ankara kwa kutumikia shilingi
Bali...
Shilingi zakutumikia wewe
Na uhuru KAMILI wa muda wako uwe nao

Nauliza umefanikiwa?
Kazana kutengeneza mfumo
Usitumikie mfumo

Maoni

  1. Mafanikio vijana Wako Ni wa umiliki

    Nakubaliana na maneno haya

    ni kweli, suala mpya inaweza kuwa alisema kweli kuwa na mafanikio wakati wakati imepata mambo mengi kwa ustadi wa wakati wenyewe kama iwezekanavyo

    Usahihi zaidi Mafanikio katika maisha yetu wakati sisi kupata
    1. kuwa na familia
    2. fedha imekuwa ikifanya kazi kwa ajili yetu, sisi ni kazi tena kwa fedha
    3. wakati huo huo, kugawana wakati wetu pamoja na familia na watu tunapenda zaidi kuliko wakati kazi,
    4. afya
    5. alikutana na mahitaji yote

    kwa bahati mbaya mimi hawajaweza kufikia wote, na tuna imani wanaweza kufikia


    Web Design Development Company in Jakarta | Ecommmerce Services Solution in Indonesia || Balinese Furniture Wholesaler & Craft Exporter Company in Indonesia

    JibuFuta
  2. Nice blog and good information

    JibuFuta
  3. blog nice information, thanks for sharing

    JibuFuta
  4. thak you
    Nice blog and good information

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?