Mtandao unapokuwa wa manati...

Nilikuwa safarini kwa kama majuma mawili hivi. Kuna "tupicha tuwili tutatu" nimekuwa nikijaribu kutubandika humu bila mafanikio. Jitihada za kugundua kikwazo hiki kimetokana na nini zinaendelea. Ila walau kwa sasa nadhani ni haya mambo ya mtandao wa kuunga na kamba za katani.

Tunablogu katika mazingira magumu saa nyingine. Unapobofya mara nyingine unalazimika kuendelea na shughuli nyingine, wakati ukisubiri kiungo kifunguke! Hapo hujaoongelea kupandisha picha. Lol...

Haya nisilalamike sana. Haya ndio maisha ya watanzania tulio wengi.

Maoni

  1. Kaka Bwaya kweli hii ni shughuli na kama una hasira utaacha kabisa kwenda internet Cafe. Yaani ni taratibu mno lakini kumbuka usemi huu haraka haraka haina baraka polepole ni mwendo.

    JibuFuta
  2. Tukumbuke tulikotoka. Miaka michache tu iliyopita hatukuwa hata na hizi Caffe. Bado safari ni ndefu lakini nadhani tumepiga hatua. Msikate tamaa. Jamii ni lazima ikombolewe!

    JibuFuta
  3. Pole pole ndio mwendo? Nakubaliana na wewe Dada Yasinta. Kufika tutafika hata kwa kuchelewa.


    Profesa Matondo, ni kweli. Pamoja na adha tuipatayo kwenye mitandao yetu; adha ya kupoteza muda mwingi kungoja; mara nyingine tukijikuta tunalipia muda tusioutumia; bado ni hakika kwamba tumepiga hatua.

    Mabadiliko ni dhahiri.

    JibuFuta
  4. Haya yamenikuta nikiwa MOROGORO juzi.....
    Nilichoka......

    JibuFuta
  5. Niaje wakubwa,mimi nilifikiri ili tatizo ni langu tu,ndio maana mimi blog yangu haina picha,kwa sababu inachukua muda mrefu sana,ila kwetu hapa Tanzania tupo juu kwenye kutumia internet.wakubwa barikiweni,na Muwe na cku nzuri.

    JibuFuta
  6. nimezunguka kama nchi tano majirani kabisa na Tanzania. nikaona tofauti kubwa sana ya spidi ya internet. Pia nilibahatika kufanya kazi kwenye makampuni kama mawili ya internet(ISP)nikiwa bado Tanzania. Ukweli kabisa makampuni yetu ya TZ ni waongo sana. Huduma wanayoitangaza sio wanayoitoa. Wahindi wanatuibia sana. Na TCRA hawana sheria yeyote ya kuwabana. Na inapokuja mikoani ambapo ISP wapo wachache, wanafanya wanavyotaka. Hakuna bado ushindani wa soko. ILA NAAMINI HAYA YATABADILIKA KWA MUDA. kama prof walivyosema miaka ya juzi juzi tu hata hizo cafe hazikuwepo. NA HUO MKONGA WA MAWASILIANO UNAOANZA UTABADILISHA KABISA spidi na bei ya mawasiliano Tanzania. TUTAFIKA TU

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?