Unauelezaje utamaduni wa kusainiwa kitabu na mwandishi?

Profesa Mbele anaeleza vizuri kuhusu utamaduni wa kusainiwa vitabu katika blogu yake:
 "...Suala hili la kusaini au kusainiwa vitabu linastahili  kutafakariwa. Naamini lina vipengele kadhaa muhimu, kama vile kiutamaduni, kisoshiolojia, kisaikolojia, na kifalsafa. Hata katika maduka ya vitabu hapa Marekani, aghalabu utaona vimepangwa vitabu vya mwandishi vikiwa na ujumbe "Signed copy." Jambo hili linaisukuma akili yangu kutaka kulielewa zaidi. Ningependa kujifunza zaidi kuhusu suala hili, kwa kusoma maandishi mbali mbali na kufanya tafakari mwenyewe..." 
Msomaji wa kitabu cha Profesa Mbele, akifurahia nakala ya kitabu. Picha: @hapakwetu

Unaweza kusoma zaidi kwenye blogu yake hapa.

Kama mmoja wa wasomaji waliowahi kupata bahati ya kusainiwa kitabu na mwandishi mwenyewe, mmoja wapo akiwa Profesa Mbele, mwandishi wa kitabu kizuri cha "Africans and Americans Embracing Cultural Differences", nikiri kabisa kwamba suala hili lina muujiza wa aina yake. Muujiza huu, ni vigumu kuuelezea kwa maandishi. Ni kama upako usioelezeka kwa lugha. Hapa ndipo ninapokubali kuwa lugha, pamoja na uzuri wake, ina mipaka yake katika kuelezea hisia za ndani. Ni sawa na muumini aliyejazwa na Roho Mtakatifu, na ukamwomba akuelezee anavyojisikia, na bado ukatarajia kuelewa anavyojisikia.

Ndio maana, kama anavyosema mwenyewe, katika baadhi ya maduka ya vitabu, vitabu hivyo vyenye 'upako' wa mwandishi huuzwa kwa bei ya juu kidogo.

Je, unaweza kuelezea hisia za kuwa kitabu chenye saini ya mwandishi? Unaweza? Mimi siwezi.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?