Matokeo Kidato cha IV 2010: Asilimia 89 wamefeli!

Inasikitisha kuwa katika matokeo ya Kidato cha Nne yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani leo hii, zaidi ya asilimia 50 ya watahiniwa wa mtihani wa kidato cha IV mwaka 2010 wameishia kupata daraja sifuri. Asilimia 39 ya watahiniwa hao (waliozidi 440,000) wameambulia cheti kisicho na tija (yaani Daraja la IV)wakati ni asimilia 11 tu wameweza kupata Madaraja ya I, II na III. Hali hii si ya kufurahia hata kidogo.

Je, tuchukue hatua gani kujinusuru na janga hili?

Maoni

  1. Hii kufeli mimi sioni ajabu, hivi jichukulie wewe kama mwalimu unatoka nyumbani na njaa, unaweza kufundisha kweli, umeacha watoto wanaumwa, kodi inakudai...usafiri ndio usiombe, na sasa gonjwa lisilotibika la mgawo wa umeme,....!
    Ilivyo, watafaulu watoto wa wakubwa wanaosoma centi nanihii na intaneshino skuli...!

    JibuFuta
  2. @M3, kwa mtindo huu watoto wetu wa Seinti Kayumba wasahau kufaulu.

    JibuFuta
  3. Hakuna jibu rahisi kwa tatizo hili kwani sababu zake ni nyingi na tata kuanzia sera yetu ya lugha, jinsi tunavyochagua waalimu wetu (waliofeli ndiyo wanakuwa waalimu), huduma mbovu na mishahara midogo kwa waalimu, elimu kutozingatiwa na wanasiasa, utitiri wa shule za kata zisizo na waalimu na mengineyo mengi. Inabidi tukae na kufikiri kwa makini kisha tuanze kutatua tatizo moja moja kati ya haya. Lakini bila kuwa na wanasiasa ambao wako tayari kutoa msukumo wa pekee kwenye suala la elimu ni kazi bure kwani wao ndiyo wanapitisha maamuzi na kutunga sera. Hata kuamua kuhusu lugha ya kufundishia tumeshindwa na tumekuwa tukibabaishana tangu tupate uhuru kiasi kwamba leo watoto wetu wanamaliza shule wakiwa wahajui Kiswahili (cha kitaaluma) wala Kiingereza.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?