Pesa bila kufisidi mali ya umma...


Pesa bila unyonyaji inawezekana? Ninakisoma hiki hivi sasa kwa mara ya pili, cha Napoleon Hill.

Maoni

  1. Nasikia hata mtu asemaje KUFISADI aka KULIA OFISINI bado ni rahisi zaidi hata kwa mafisadi ambao kabla hawajadaka ofisi walikuwa hawafikirii UFISADI kama moja ya njia ya kuwa TAJIRI!:-(

    Kwani KUWA TAJIRI au tu tu GROW RICH ni nini kama utajiri moja ya tafsiri yake ni kuridhika tu na skonzi wakati keki zipo ingawa kuna aridhishwaye zaidi na MAANDAZI?

    JibuFuta
  2. Loooh!! unakisoma kwa mara ya pili mkubwa??? ngoja nami nirejee maktabani nipekuepekua walau mawili matatu, maana ile NADHARIA YA CHANGE YOUR FREQUENCY inanikuna sana. Pamoja sana mkubwa katika kuliendekeza libeneke la kusoma vitabu. amani iwe nawe daima

    JibuFuta
  3. Kinachosikitisha ni jinsi wengi katika jamii yetu wanavyoamini kuwa mafanikio watayapata kwa njia za kishirikina, badala ya kuzingatia elimu inayopatikana vitabuni.

    JibuFuta
  4. @Mkodo, Kufisidi ni tabia unayoweza kuibaini mapema tu.

    @Marcus, nimefurahi kusikia umekisoma! Naomba pendekezo la unachokisoma hivi sasa.

    @Profesa, pengine tumelelewa kishirikina.

    JibuFuta
  5. Pesa unaipataje, unaweza ukaokota, ukiokota kuna kapoteza umadhulumu/fisidi. Ukaamua kufanya kazi, ukapata mshahara, je katika dhima nzima ya kufanya kazi hukuwahi kutega...lazima kutakuwepo na uzaifu fulani, umepata kitu/mshahara lakini ndani yake kuna ufisidi...au sio
    Umefanya biashara, ukauaza na kupta faida kubwa, je hiyo faida ina uhalali , kuna kukwepa kodi, kuna kudanganya kuwa ni kizuri kumbe siku mbili tatu kibovu...umefisidi..
    Lakini kuna ufisadi wa dhahii, mkubwa sana, unafisidi nchi nzima, mama yangu...hata yule asiyejiweza, hata yule asiye na baba wala mama, hata ....mungu wangu utasema nini mbele ya muumba!
    Nimewaza tu mkuu!

    JibuFuta
  6. @Emu three ufisadi, kwa kadri ya maelezo yako ni sehemu ya utamaduni. Je, twaweza kujinasua?

    JibuFuta
  7. Kinatakiwa kuwepo katika maktaba za shule na hasa zaidi katika ile ya Bunge la Tanganyika

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?