PICHA: Elly Prior Chukulia mnajadiliana jambo na rafiki yako. Inaweza ikawa ni mtandaoni, nyumbani, ofisini au mahali kwingineko. Katika mazungumzo yenu unabaini hamuelewani. Kile unachoona ni sahihi, sivyo anavyoona mwenzako. Kila mmoja wenu anajaribu kutetea upande wake kuliko anavyoelewa mtazamo wa mwenzake. Unadhani kipi ni sahihi kufanya katika mazingira hayo? Je, ni busara kuendelea kuthibitisha ulivyo sahihi hata kama ni dhahiri mwenzako hayuko tayari kukuelewa? Unajisikiaje mwenzako akikuonesha haukuwa sahihi? Mara nyingi tunafikiri kushindwa na kutokuwa sahihi ni udhaifu. Tunapambana na wasiotuelewa kwa mabishano na majibizana kwa lengo tu la kuonesha tulivyo kwenye upande sahihi. Unazungumza ili kushinda? Nakumbuka siku moja nilishiriki mjadala mmoja kwenye mitandao ya kijamii. Katika mjadala huo, kulikuwepo na pande mbili zinazotofautiana kimtazamo. Kadri mjadala ulivyoendelea, niligundua hapakuwa na jitihada za pande mbili hizo kuelewana. Kila upande...