Vitabu 49 Nilivyovisoma Mwaka 2016

Namshukuru Mungu nimeweza kusoma vitabu 49 kwa mwaka 2016. Nimejifunza mengi. Kusoma ni kama kupata nafasi ya kufanya mazungumzo na watu wa kila namna ya uelewa ambao kwa hali ya kawaida usingeweza kuwasikia vijiweni. 

Msisitizo wangu umekuwa kwenye vitabu vinavyochambua tabia katika maeneo mbalimbali ya maisha. Hata hivyo, vipo vichache vya masuala ya imani, falsafa na dini. Sijawa msomaji wa riwaya/novel.

Nikutie moyo wewe mwenye ratiba ngumu kwa siku. Unaweza kufanya maamuzi ya kusoma ikiwa utaamua kuweka ratiba yako vizuri. Nijitolee mfano mimi mwenyewe.
Mbali na majukumu ya mwajiri wangu, nimekuwa nikiandika makala zipatazo nne za magazeti kila wiki. Kuandika kunahitaji muda.

Lakini pia nimekuwa nikifanya kazi za ushauri elekezi katika maeneo yangu ya kitaaluma ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za kuhariri tasnifu za wanafunzi wa Shahada za Uzamili/Umahiri. Si mchezo. Inabidi kusoma machapicho mengi na kupata muda wa kuwa mwenyewe. Lakini pamoja na hayo yote, nimeweza kujitahidi kuhakikisha ninasoma. 

Ujumbe wangu kwako ni kukuhimiza kujenga utamaduni wa kusoma. Hakuna anayezaliwa akipenda kusoma. Tunajifunza. Hata hivyo, tunatambua changamoto ya upatikanaji na gharama za vitabu. Ikiwa tunafahamiana kibinfasi na unahitaji kuazimwa kitabu, karibu tuone tunachoweza kufanya.

Kwako uliye msomaji kama Prof. Mbele mwandishi wa kitabu maarufu cha Africans and Americans: Embracing Cultural Differences nilichokisoma kwa zaidi ya mara tatu, tuendelee kuhimizana kusoma. Mtu anayejua kusoma lakini hasomi hana tofauti na mtu asiyejua kabisa kusoma. Tusome.


Orodha yangu ni kama ifuatavyo:

 1.       Why Nations Fail: The origins of power, prosperity and poverty – Daron Acemoglu & James Robinson (kikubwa nakisoma hatua kwa hatua)
2.       Good to Great – Jin Collins
3.       Built to Last: Successful habits of visionary companies – Jim Collins
4.       Born for This – Chris Guillebeau
5.       Ego is the enemy – Ryan Holiday (nakimalizia)
6.       The curse of the self: Self awareness, egotism, and the quality of human life – Mary Leary (e-book) asante Justine Mwombeki).
7.       Experiencing God together – Harry Blackaby & Melvin Blackaby (kikubwa, nakisoma kidogo kidogo)
8.       Why men don’t listen & women can’t read maps – Allan & Barbara Pease (e-book)
9.       Choosing to see – Mary Beth Chapman
10.   How to stop worrying and start living – Dale Carnergie
11.   Emotional Intelligence – Daniel Goleman
12.   Social Intelligence – Daniel Goleman
13.   Working with Emotional Intelligence – Daniel Goleman
14.   The monk who sold his Ferrari – Robin Sharma
15.   The secret letters of the Monk who sold his Ferrari – Robin Sharma
16.   The leader who had no title – Robin Sharma
17.   Make it stick: The science of successiful Learning – Peter Brown & Henry Roediger
18.   Who will cry when you die? – Robin Sharma
19.   Mlinzi Mkuu wa Mwalimu Nyerere – Peter Bwimbo
20.   Shushushu – Evarist Chahali
21.   Huruma wa Mungu ni kwa watu wote – Fr Innocent Bahati
22.   Good Muslim, Bad Muslim: America, the cold war and the roots of terror – Mahmood Mamdani
23.   Abraham Lincoln – Philip Ostergard (sijakimaliza)
24.   African Pilgrimage: Reports and reflections from Tanzania – Damian Milliken
25.   In the belly of Dar es Salaam – Elieshi Lema
26.   The creator’s code – Amy Wilkinson
27.   In God’s Name: An investigation into the murder of Pope John Paul – David Yallop (nakisoma kidogo kidogo)
28.   If God should choose – Kristen Stagg
29.   Is God an Illusion? The great debate between science and spirituality – Deepak Chopra & leonard Mlodinow  
30.   48 Laws of Power – Robert Greene
31.   Mastery – Robert  Greene
32.   Nomad: From Islam to America (Personal Journey through the clash of civilization) – Ayaan Hirsi Ali
33.   Mother Teresa: A simple path – Lucinda Vardey
34.   The Autobiography of Martin Luther King, Jr – Clayborne Carson (Ed) [sijakimaliza)
35.   No higher Honor: A Memoir of my years in Washington – Condolezza Rice (kikubwa nakisoma kwa hatua)
36.   A brief guide to philosophical classics (From Plato to Winnie the pooh) – James Russell
37.   African – American perspective and philosophical traditions – Joh Pittman (Ed)
38.   Outwitting the Job Market – Chandra Prasad
39.   Rich Dad's Conspiracy of the Rich – Robert Kiyosaki
40.   The White Masai – Corinne Hofman
41.   A long way from Paradise: Surviving the Rwandan Genocide – Leah Chishugi
42.   Your erroneous zones – Wayne Dyer
43.   The rules of life – Richard Templar
44.   The seven habits of highly effective families– Stephen Covey (nimekisoma kwa mara ya pili)
45.   Emotional Infidelity – Gary Neuman
46.   10 secrets of a great marriage – Lilo Leeds & Gerard Leeds
47.   Bring Home the Joy – Larry Grab et al
48.   You, Inc: The art f selling yourself – Harry Beckwith
49.   Attachment Theory, Child maltreatment and family support – David Howe et al  (sijakimaliza)



Maoni

  1. Mwalimu hongera sana kwakuamua kuulisha ubongo wako kupitia vitabu na machapisho mbalimbalili.

    The good thing kuna vitabu umevisoma ambavyo nami kwa mwaka huu nimebahatika kuvisoma. Nilikuwa na ratiba ngumu kwa mwaka huu kijana wako wa march intake (Bios n Computer) ila nilijitahidi kusoma vitabu takribani 19 vitabu 6 zaidi ya vya mwaka jana 13.

    Orodha yangu ya vitabu nilivyosoma.
    1. Why Nations fail
    2. Miseducation of the Negro
    3. The monk who sold his Ferrari
    4. The Secret
    5. Dead Aid (nakimalizia)
    6. Pedagogy of oppressed
    7. Why men dont listen and...
    8. Nimuoe nani?
    9. The seven habits of highly effective...
    Na vinhinevyo 10 sambamba na machapisho mbali mbali ya kitaaluma na kihistoria, mathalani ya Prof. P.L.O Lumumba

    JibuFuta
  2. Pia nikupongeze sana wewe binafsi na Mr. Minja kwa semina ya juzi. Nilitamani sana matukio muhimu kama hayo kwa muda mrefu ila angalau mlitibu kiu yangu japo kidogo

    JibuFuta
  3. nimependa namna mwalim unavotumia mda wako na taaluma yako ktk vitu va msingi kiukweli umenifungua akili na kutambua umhim wa kutumia mda...pongez kwako mwalim hasa kwa kaz kubwa unayoifanya hapa mwecau binafsi napenda ufundishaji wako nakuelewa saana....ntakua baloz mzuri kwa vijana wenzangu juu ya umhim wa kusoma vitabu mbalimbali

    JibuFuta
  4. Nimejifunza kitu na hakika ntakifanyia kazi. hii tabia ni njema na yakupaswa kuigwa.

    JibuFuta
  5. Hongera sana mwalimu Christian- you are inspirational

    JibuFuta
  6. Hongera sana mwl Christina ,,,,,itakuwa vyema zaid vitabu vyoko vika Shamir ktk lughu yet madhubut ,,ili vipatekuzakisha wasomaji weng ,wenye elim tofautitofaut ahsante

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging