Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2007

Unahusianaje na nafsi yako?

Huwa unajisikiaje ukijitazama kwenye kioo? Unaridhika na sura unayoiona? Vipi ukiangalia picha zako za hivi karibuni? Unaridhika na ulivyo? Umbo lako? Mtindo wa nywele zako? Rangi ya ngozi yako? Unajionaje? Watu wengi tunapata shida sana kujikubali. Hatujipendi. Kila tunapojitazama, tunaona kasoro. Wachache wetu huziona kasoro hizo kama vitu vidogo visivyotupa tabu sana. Mtu aweza kujiangalia kwenye kioo, akaona kasoro ndogo, lakini akajipa moyo: "Ngoja nichane, nitapendeza". " Ngoja niende saluni, nikabadili mtindo". Akaziona kasoro na zisimsumbue. Lakini wengi wetu huvunjika moyo kwa kudhani/amini kuwa kasoro hizo hazirekebishiki. Pengine rangi ya ngozi si nyeupe vya kutosha. Ama umbo letu halivutii, na mambo kama hayo. Kuvunjika moyo kwa namna hiyo, husababisha kujengeka kwa hisia hasi kuhusu nafsi ya mtu mwenyewe. Jambo moja kabla hatujaendelea: Mahusiano mema na nafsi zetu hutokana na vile tujichukuliavyo. Mahusiano mabaya na nafsi zetu husababisha kujidh...

Sherehe bila mwenye sherehe, inawezekanaje?

Picha
Umewahi kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mtu fulani bila ridhaa yake? Au unaigeuza kabisa inakuwa sio kumsherehekea yeye, ila kufanya utakayo, kwa mwamvuli wa kumsherehekea yeye! Kama ingekuwa ni wewe ndiye mwenye sherehe, ungejisikiaje? Watu wala, wanywa, hata kadi ya mwaliko hawakupi. Na bado wanadai wanakumbuka kuzaliwa kwako. Kweli? Hivi ingekuwa wewe ungejisikiaje?

Tofautisha dini yako na utamaduni wa "wenye dini"

Wakati umefika wa kuchukua juhudi binafsi za kutenganisha dini na utamaduni wetu kama vitu viwili tofauti. Tuweze kupambanua mambo ambayo ni ya kidini na yale ya utamaduni wa nje, ambayo kwa kujua ama kutokujua tunadhani kwa kuyafanya maana yake tunashika dini. Kuvaa kanzu na baibui si utamaduni wetu. Kuitwa Mathayo hakuhalalishi ukristo wako. Kukaa chini katika ibada, wakati kuna uwezekano wa kupata viti, ni kujaribu kuwaiga wenye dini na mazingira yao. Na bahati mbaya twayafanya hayo tukiamini kuwa tunashika dini kumbe ni ulevi tu wa utamaduni wa watu fulani fulani. Tujielewe.

Tusitegemee uzalendo kwa elimu hii

Kati ya mambo ambayo wana wa Kitanzania wanayakosa katika vyumba vyao madarasa, ni elimu ya kujielewa. Elimu ya kuwafanya waelewe nafsi zao wenyewe. Elimu ya kuwapandikizia falsafa za taifa lao wenyewe. Elimu ya kuwakomboa kimtazamo, wajue umuhimu wa utamaduni wao. Elimu ya kuwafanya waelewe wajibu wao katika kuufufua utamaduni huo ndani yao wenyewe na katika watu wao. Wenye kufundisha, hawajui nchi inayofalsafa gani. Nchi yenyewe haieleweki inayo falsafa ipi. Mitaala nayo haifahamiki imetayarishwa kwa shinikizo la nani na nani atapanda dau lini kuibadilisha. Na matokeo yake ni kwamba kila kijana "huhitimu" na falsafa yake anayoijua yeye na huelekea anakokujua mwenyewe. Kila jambo linakuwa shaghalabagala! Ndani ya mfumo kama huu, haitokaa iwezekane kuwa na Tanzania yenye dira inayoeleweka. Haitokaa itokee kuwa na Tanzania iliyojipembua kwa utamaduni wake. Haitokaa itokee tuwe na Tanzania yenye wazalendo waliotayari kuitetea raslimali za nchi yao kwa dhati ya mioyo. Haitokaa i...

Je, umewahi kuiadhibu nafsi yako mwenyewe?

Wajibu ni nini? Haki ni nini? Je, waweza kudai haki fulani fulani kutoka katika nafsi yako mwenyewe? Je, waweza kujiadhibu wewe mwenyewe kwa kutokutimiza wajibu fulani? Je, ni sahihi kudai haki (zako) kutoka kwa wengine, wakati (wewe mwenyewe) hujitendei haki? Tujielewe.

Unapojielewa nini huwa kimetokea?

Kujielewa. Tunasisitiza sana kujielewa. Lakini je, kujielewa maana yake nini? Unapoelewa jambo nini hasa huwa kimetokea katika ufahamu wako? Je, kuna tofauti gani iliyopo unapolinganisha kabla hujaelewa na baada ya kuelewa jambo? Je, twaweza kuelewa na/au kujua kila kitu? Je, upo ukomo (limit) wa uelewa?

Ukweli ni lazima uwe uhalisi?

Uhalisi (reality) ni nini , na unatofautianaje na ukweli (truth)? Je, uhalisi lazima uwe ukweli? Je, kila ukweli ni halisi? Je, utajuaje kuwa unachojua ni uhalisi usio ukweli ama ukweli usio uhalisi?

Akili hutengenezwa!

Huwezi kufikiri jambo ambalo halipo ubongoni. Haiwezekani. Kufikiria ni kupekua mafaili. Kama mafaili yenyewe hayapo, huna cha kutafuta. Ubongo wa mtoto ni kama ofisi mpya ambayo mamlaka ya kuifanya upendavyo yako mikononi mwako. Unaingiza fanicha uzipendazo, kwa kadiri ya mahitaji ya Ofisi yako hiyo. Unapanga makarabrasha yako kwa utaratibu uupendao mwenyewe. Sababu wewe ndio ofisi. Na unapohitaji sasa kuyatumia makrabrasha hayo, uchaguzi wako utakuwa “katika” yale yale uliyoyihifadhi awali. Pamoja na mapungufu ya mfano huu, bado unaweza kutumika kuelezea hali halisi. Huwezi kutafuta kitu ambacho ni wazi hukukiweka. Au labda tuseme, ubongo wa binadamu ni sawa kompyuta tupu isiyoweza kufanya chochote mpaka mmiliki apandishe (install) programu azipendazo mwenyewe. Na uchaguzi wa kipi akifanyie kazi kwenye kompyuta yake unategemea na yaliyomo. Watafiti wengi wanakubaliana kuwa kila mtoto huzaliwa na ubongo safi. Wenye uwezo safi. Wenye nguvu (potential) ya kuwa chochote. Pamoja na tofaut...

Mkono wa Mama

Picha
Enzi za ujana wangu, mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili, nikiwa mwanafunzi wa "shule za manerumango" nilipoukamata mkono wa mama Migiro mbele ya Pro.Mmuya. Nilikuwa nimeshinda shindano la nsha. Hapa nakabidhiwa "karatasi" la ushahidi kama ilivyo kawaida ya waswahili, kwamba kila kitu lazima kifuatane na cheti. Nimeiweka picha hii kukukumbuka siku nilipozaliwa. Sina hakika kama ndiyo yenyewe, manake naonekana mzee mzee.

Hivi mtoto huwaza kama mtu mzima?

Picha
Kama umewahi kujiuliza swali kama hilo, tafadhali karibu tuchangie mawazo. Mtoto huwaza nini? Mtoto hufikiri nini na kwa upana gani? Katika mambo yanayofurahisha sana katika akili ya binadamu, ni vile ubongo wake unavyoweza kutengeneza mtandao wa kuhusianisha "tukio" moja na lingine, na hivyo kuleta mtiririko wa matukio unaoweza kujulikana kama mawazo. Unapowaza maana yake ni kwamba ubongo wako unao uwezo wa kuunganisha vipande vingi vya matukio (schema) kwa kadiri yanavyohusiana, na hivyo kuleta mtiririko fulani, unaleta mlolongo wa uhusiano wa aina fulani. Inakuwa kama ile mikanda ya sinema yenye picha nyingi zisizotembea zenye mtitiriko wa matendo yanayokaribiana ambayo huunganishwa na kuleta mtiririko unaotembea. Mawazo hapa yakimaanisha mtiririko wa vipande vya habari katika ubongo wa binadamu. Ikiwa ubongo utashindwa kufanya hivyo, kwa maana ya kukosekana kwa mwendelezo wa vipande hivyo, kamwe mwenye ubongo huo hawezi kuwaza jambo. Sababu ni kwamba kati ya kipande kimoj...

UKIMWI una tiba kumbe?

Picha
Sikuandika siku kadhaa zilizopita, kipingamizi kikiwa ni uvamizi wa kirusi. Nafurahi kwamba "tabibu" alipatikana, na tiba sahihi ilifanyika, UKIMWI ukasalimu amri. Shukrani za pekee zimwendee Bwana Minja, msomaji wa blogu (yeye anadai inatosha kuzisoma) na fundi mwanafunzi katika sayansi ya kompyuta. Kwa hakika tunawahitaji sana watu kama hawa katika jamii zetu, watusaidie "kugawana" umasikini wetu. Minja. Minja kaozea katika teknolojia. Minja. Minja na spana. Minja. Ukienda kwa Minja hutathubutu kuongea siasa. Si tu kwamba hatakusiliza, lakini pia mazingira hayatakuruhusu. Bush kafanyeje, wala hajui na hataki kujua. Ongea teknolojia. Ndugu yangu utakoma. Huo ndio mgawanyo wa kazi unaotutofautisha wenyewe kwa wenyewe. Ndugu Minja nakushukuru sana. Nitajaribu kuchukua hatua za dharura, tatizo lisijirudie. Wanasema tubadili tabia ili kuepuka gonjwa lile. Basi huenda tabia yangu ya kunyonya blogu mtandaoni na kuzihamishia kwenye kimeo changu inaniponza. Muhimu, niwe...