Machapisho

Safari zinavyotukutanisha na mengi

Nimekuwa na pilika pilika za hapa na pale. Sehemu kubwa ya muda wangu nikiutumia katika vijiji vyetu. Nilianzia Morogoro. Tukuyu. Kyela. Baridi ile mbaya. Watu wanalima kahawa wa kununua haonekani. Akiwepo basi bei ni ya kutupa. Mtu unajiuliza hivi ni lini wakulima watapata thamani sawa na watu wengine? Mwananchi anahangaika na mashamba ambayo hayamsaidii kujikwamua. Watu wamekata tamaa. Ndugu zangu tuache kufarijiana. Wananchi wamekata tamaa. Majuma kadhaa ya mwezi Julai nimeyatumia Tunduma na Vwawa. Watu wanaishi maisha magumu sana. Wanajua kuwa nchi yao inazo hela, lakini zinaliwa na walafi wachache. Ukitaka kuijua Tanzania, usiishie dasalama. Vwawa na Mbozi panaweza kukupa picha ya nchi yetu. Nikiwa Mbeya mjini nikajaribu kupandisha picha kwenye blogu, ikawa ngumu. Hata sijui palikuwa na nini hapo. Nikiwa Ipogolo Iringa nako sikuweza kukaa na kuandika. Juma moja likaishia Dodoma nikiwa na heka heka nyingi kidogo. Nikadhani nikiwa Singida ningeandika. Wapi bwana. Singida ndio ...

Sayansi haina wapenzi wake mtandaoni?

Kuna msomaji wangu ameniandikia anasema Sayansi haina wafuatiliaji. Anasema, "Yale madude yanaboa..Sayansi haina wapenzi wengi kabisa." Haya. Asante kwa ushauri.

Ni kweli, Fossils, mabaki ya viumbe wa kale ni ushahidi wa Evolution?

Msomaji mwenye historia ya elimu ya viumbe anaweza kuuliza: Uhusiano tunaouona baina ya viumbe (phylogenetic relationship) una maana gani? Kusema kweli, viumbe wanaonekana kuhusiana kwa karibu. Na uhusiano huo unaleta mawazo kuwa huenda kila kiumbe ametokana na mwenzie. Kwa mfano inavyoonekana, maisha hasa ya viumbe yalianzia baharini. Kwa maana hii, viumbe wa kwanza waliishi majini wakibadilika badilika na kuishia kufanya aina nyingine ya maisha yasiyotegemea maji, yaani maisha ya nchi kavu. Sasa katika kuangalia mlolongo huu, tunaambiwa viumbe walijikuta wakijiongezea “viungo” (adaptive features) vilivyowawezesha kukabiliana na aina vyingine ya maisha. Kwa ule mfano wetu wa samaki, ni kwamba baadhi ya samaki walianza kupoteza uwezo wao wa kupumua kwa kutegemea maji, na badala yake, wakaanza kuwa na vitu kama mapafu vilivyowasababisha kugeukia maisha nje ya maji. Baadae makoleo yao yaliyotumika kuogelea (fins) yakatengenezeka kuwa (miguu?) ili waweze kuishi vizuri nchi kavu. Na...

Ni kweli kuwa viumbe wametokana na mabadiliko 'ya kubahatisha'?

Tulichagua kutumia kanuni za Marehemu Charles Darwin kwa sababu ndiye aliyejaribu kujihusisha kwa kiasi kikubwa na asili ya mabadiliko ya viumbe kwa mtazamo wa kisayansi. Na kwa kuwa lengo letu ni kuitizama sayansi kwa jicho la haki, tunaona na ni vyema “kuweka kumbukumbu sawa”. Marehemu Darwin amejaribu kuonyesha kwamba viumbe vilitokea kwa bahati, vikapitia mabadiliko ya uasili wao kufanya asili nyingine iliosababisha kugeuka na kuwa viumbe vya aina nyingine kabisa. Ili kufafanua anachosema Darwin na rafiki zake, tuchukulie mfano wa viumbe kama samaki. Samaki, kwa mujibu wa kanuni ya “natural selection”, walipitia mageuzi kadhaa yaliyosababisha tofauti katika kundi lao la samaki. Tofauti hizi ziliendelea kuwa kubwa kiasi cha kusababisha kutengenezeka kwa aina fulani ya samaki waliokuja kufanya kundi la viumbe tofauti kabisa na samaki wengine waliobaki. [Kundi hili linafahamika kama amphibia lenye mifano ya viumbe kama mamba na vyura]. Maana yake ni kwamba katika samaki, walit...

Sayansi na imani, mwendelezo

Niliandika mara kadhaa, nikijaribu kuonyesha matatizo ninayoyaona katika sayansi. Kusema kweli siandiki kudhihaki umaana na heshima ya sayansi. Ninaandika kuangalia kwa upya nafasi ya sayansi katika ulimwengu wetu kwa kutizama mipaka yake. Ningeomba msomaji awe mvumilivu tunapoelekea katika hitimisho la mjadala huu. Kama u msomaji mpya, unaweza kupitia hapa na ukaja hapa , kwa mtiririko huo huo ukasoma na hapa pia . Halafu tuendelee.

Urembo kikwetu, unakuwaje hasa?

Nilipodokeza kuhusu suala la mahangaiko ya akina mama na nywele, msomaji mmoja aliniandikia: " Mwanamke gani utaoa mwenye asili kamili ya uafrika?...". Nilimjibu. Katika kumjibu lilinijia swali kubwa: hivi mwanamke mrembo hasa ni yupi? Mrembo/mzuri kwa macho ya kiafrika yukoje? Ukisikiliza maoni ya wanaume wengi utaona namna ambavyo tumeathirika kufikiri kwetu. Utaona namna tusivyoipenda aisli yetu hata kama tunadai kuupenda uafrika kwa maneno yetu. Kwa wengi, mwanamke mrembo ni lazima awe mweupe kadiri iwezekanavyo. Awe mweupe peee hata kama ni kwa kulazimisha. Ndio maana kwa baadhi ya makabila mwanamke mweupe hulipiwa mahari kubwa zaidi ya mweusi. Mwanamke mrembo ni lazima awe mwembamba iwezekanavyo. Ndio maana wengine wanajikondesha sio kwa sababu wanaelewa umuhimu wa kupunguza mafuta mwilini, la hsha. Ni kwa sababu wanadhani ili wavutie ni lazima wakondeane. Kwa lugha rahisi mwanamke mrembo, ionekanavyo, ni yule awezaye kujipamba kwa kila kiwezekanachoo alimrad...

Kwani akina mama wanatumia nywele za bandia? Ni ili iweje?

Kama kuna mambo ambayo huwa yanathibitisha kuwa waafrika wengi hatuoni raha ya kuwa waafrika ni hili la nywele za bandia. Wanawake wa kiswahili wanateketeza muda mwingi na fedha nyingi kutengeneza nywele zao ama 'kununua' nyingine zenye asili tofauti. Kwao huko ndio kupendeza. Ukibaki na za kwako ukazitunza zikawa nzuri, zikabaki za kiafrika, hujapendeza bado. Kwamba kwa kufanya hivyo wanapendeza ama vipi, hilo kwangu sio suala. Kinachonitatiza ni sababu ya kuzitengeneza ziwe na asili tofauti: Hivi ni kwa nini? Hawawezi kupendeza bila kubadili asili ya nywele? Si kwamba ni dalili flani ya kujiona mwenye asili duni kuliko watu fulani? Si kwamba hii ni dalili ya udhaifu wa kujielewa na kujiamini? Wewe unafikiri vipi kuhusiana na hili? Kwangu hii ni aibu moja wapo ya waafrika. Kabisa.

Heri ya mwezi mpya!

Mwezi wa tano ndio huu. Tarehe mbili leo. Kama ulikuwa hujapanga cha kufanya mwezi huu, ndugu, hujachelewa. ( Si unajua haipendezi kufanya chochote bila kupanga?) Tabia ya kusubiri mwisho wa mwaka ndio tuanze kufikiri kupanga mipango mingi ya mwaka mzima ( ambayo hata hivyo haitekelezeki) si nzuri sana. Nakukumbusha mipango yako ya mwaka huu: Ulipanga kufanya nini mwaka huu? Je, umefikia walau nusu ya mipango yako? Una mikakati gani na mwezi huu wa tano? Nusu ya mwaka ndo inayoyoma! Nakukumbusha kutafakari upya mambo yako mwaka huu, uone wapi umefanikiwa na wapi unahitaji kujipanga vyema zaidi. Nakukumbusha kutafakari changamoto ulizokumbana nazo katika sehemu ya kwanza ya mwaka huu, na ufikiri namna ya kukabiliana nazo vizuri zaidi kwa nusu iliyobaki. Na unapofanya hivyo, usiache kupitia hapa kuanzia juma hili kwa ajili ya vipande vya saikolojia na falsafa za kutafakari pamoja namna ya kujielewa. Niwatakieni wanablogu wote heri ya mwezi mpya wenye mafanikio (pamoja na uki...

Tuiamini sayansi? Au ni ghiliba tu?

MIONGONI mwa maeneo ambavyo sayansi imekuwa ikijihusisha nayo, elimu ya viumbe ni mojawapo. Unapozungumzia viumbe unalazimika kuanzia na uhai wenyewe, Uhai ulitokea wapi? Tunaambiwa baharini mahala ambapo viini urithi viitwavyo DNA vinaaminika kutokea kirahisi rahisi. Bahari nayo ilitokea wapi, tunajibiwa utafiti bado unaendelea, tuvute subira. Dunia yenyewe ilitokea wapi, hapo nako tunaambiwa wanaotaka kufanya Shahada ya uzamifu, wazame. Hapo hatujauliza ulimwengu uliobaki (universe). Jambo moja ni wazi. Kuwa katika sayansi, mambo yanapokuwa magumu, rufaa huwa: TUNGOJE, maarifa hukua taratibu! Lakini ni ukweli kwamba kauli hii ni kichaka kile kile cha kukimbiwa maelezo. Tukiachana na asili ya uhai, sayansi inajaribu “kupendekeza” nadharia ya utokeaji wa idai tofauti tofauti ya viumbe tulivyonavyo leo. Mahala pa kuanzia ni kwamba inavyoonekana viumbe vyote vinavyo asili moja (common ancestry). Asili hiyo ilibadilika na kufanya viumbe kwa wingi tuuonao leo. Msingi hapa ni...

Changamoto za kublogu zinaendelea

Kwa siku kadhaa pamekuwapo tatizo la wavu wa mtandao hapa nilipo. Hivyo nilishindwa kuweka chochote hapa. Nadhani hali ni shwari, nitaweka chochote kuanzia sasa. Karibuni tuendelee.

Mpaka upate jibu...!

Picha
Hapa ni leo asubuhi nikiwa katika maabara. Sina hakika kama huu ulikuwa ni uchunguzi unaoitwa wa kisayansi kwa sababu nilikuwa nalazimishwa kutafuta jibu ambalo muuliza swali analitaka. Sayansi ndio ilivyo. Unatafuta kinachojulikana.

Udhaifu wa sayansi (2)

Picha
NIMEKWISHA kueleza kuwa sayansi si njia bora sana ya kuelezea masuala nyeti. Wanaofikiri kwamba sayansi ndiyo hitimisho la ufahamu, ninathubutu kusema kuwa wanakosea sana . Katika kuthibitisha madai haya, naomba kama nilivyoahidi, kukuletea mifano halisi. Tuanze na mwanasayansi maarufu katika elimu ya mada na tabia zake, bwana August Kekule. Huyu bwana (hapa pembeni) aligundua kile kinachoitwa benzene. Benzene ina umbo hili hapa kwa chini kama huwahi kuisikia. Mdude huu ni muhimu sana ( samahani sina Kiswahili chake) katika organic chemistry. Kekule ndiye aliyeugundua mdude huu wa ajabu ambao leo hii umeleta mabadiliko makubwa katika ufahamu wa mambo ya madawa na kadhalika. Itoshe kusema Benzene ni sehemu muhimu ya elimu ya viini mwili. Mvumbuzi wa umbo hili, Bw. Kikule hakuficha ukweli kwamba hilo umbo la benzene alilipata kwenye NJOZI. Huruhusiwi kushangaa. Hakufanya jaribio maabara, hapana, bali aliliota katika ulimwengu wa ndoto! Kuna watu wanadhani nime...

Maajabu ya 'uchawi' wa Sayansi: Inawezeshwa na ndoto mara nyingine!

Picha
Nitaandika habari za bwana mmoja anaitwa Friedrich August Kekule yeliota dude hili hapa pembeni, linaitwa benzene. Huyu bwana ailiita benzene ndio ikawa hivi ilivyo mpaka leo. Ngoja nimalizie kakazi fulani kwanza nitakuambia zaidi.

Udhaifu wa sayansi (1)

Haya tuendelee. Tunahitaji aya nyingi kufafanua dhana ya sayansi. Kwanza nijitete kwamba sina msamiati wa kutosha kukwepa maneno yanayoitwa ya kisayansi ila nitajaribu kadiri niwezavyo. Kwa uchache sana, na katika lugha rahisi zaidi, sayansi ni namna ya upatikanaji wa maarifa kwa njia ya utafiti. Utafiti hapa humaanisha majaribio ambayo hukusudiwa kuchunguza na hatimaye kuthibitisha ama kukanusha bashiri ya kisayansi. Sayansi hutumia mbinu katika kuchunguza dhana, ili kuongeza maarifa ama kurekebisha maarifa yaliyopo. Huanzia katika ukusanyaji wa ushahidi unaochunguzika, unaopimika, na wenye chanzo mahususi kinachokubaliana na ufahamu wa kawaida. ( Sina masamiati sahihi sana ). Ushahidi huo, ndio kile kinachoitwa data, ambazo hupatikana kwa majaribio ambapo bashiri hujengewa hoja ili kufanyika maelezo ya dhana iliyokuwa ikichunguzwa. Majaribio haya hupangiliwa kitaalamu kwa kutumia vibadiliko (variables) ili kuzijaribu bashiri za awali. Majaribio haya hufanyika katika ma...

Utangulizi wa hoja: Tumetokea wapi?

Kujielewa ninakokuzungumzia, kunahusisha na uelewa wa mambo kadhaa yanayoaminika kuongoza maisha ya viumbe katika ulimwengu ( pamoja na dunia) tunamoishi. Kwamba sisi binadamu tulitokea wapi na tunatafuta nini hapa duniani. Huko ni kujielewa. Ulimwengu na viumbe vilitokea wapi? Swali kama hili si rahisi sana, pamoja na umuhimu wake katika kujielewa. Yapo mawazo mengi yanayojaribu kutafuta uhalali wa fikra kadha wa kadha kuhusu chanzo hasa cha ulimwengu wenyewe pamoja na uhai na maisha ya viumbe hai na visivyo hai katika ulimwengu huu. Mawazo haya yanaweza kuganywa katika makundi makubwa mawili: Wanaoamini zaidi pasipo ushahidi, na wanaojaribu kutumia akili zao katika kutafuta ushahidi wa mambo haya. Wale wa kwanza, kwa wingi wa idadi, ni wanadini. Wale wa pili, ni wanasayansi. Mwanadini, anatafuta kujenga imani zaidi hata kama haielezeki. Mwanasayansi anatafuta ushahidi unaoelezeka. Katikati ya hao wawili, wapo wengine ambao kazi yao ni kuhoji uhalali wa mahitimisho yanay...