Tovuti bure...wahi!

Nimepata ujumbe kutoka wataalamu hawa wa kutengeneza tovuti. Hivi ndivyo wanavyosema:

" Pole na kazi ya kuelimisha na kuburudisha jamii yetu.
Tumekuja na huduma mpya ya BURE kwa watanzania tu tunaomba uwafahamishe.
Kuzingatia umuhimu wa kuwa na tovuti, na ya kwamba ni gharama sana hapa TZ
kupata tovuti, na tena watu wanafanya biashara rasmi kwa barua pepe za
bure kama yahuu na giimeili, hii yote inaonesha ukosefu au gharama kubwa
ya kupata tovuti.
Sisi tumedhamiria kubadili uelekeo mzima wa upepo, na tumepata wasamaria
wema na sasa rasmi tumefanikiwa kuleta ufumbuzi na neema kwa waTZ kwa
suala la tovuti na anuani rasmi za barua pepe.
Na sasa kwa awamu ya kwanza kwa kuanzia tu, WATU 100 WATATENGENEZEWA
TOVUTI BURE. Watu 100 kwa maana ya mtu binafsi, kampuni, biashara,
shirika, asasi zisizochukua faida (NGO), kikundi, duka, mjasiriamali,
saluni, shule ama Saccos n.k. BASI KILA ALIYEDHAMIRIA KUWA NA
WEBSITE/TOVUTI ajiunge na utaratibu huu wetu atengenezewe TOVUTI MOJA BURE
KABISA.
TOVUTI HII YA BURE itamfanya mhusika aweze kupata anuani rasmi za barua
pepe, yaani kama yeye ni Mwanahawa wa Vinyago Suppliers anatengenezewa
anuani zake za barua pepe mfano mwanahawa@vinyagosuppliers.co.tz n.k
kadiri ya atakavyo, nyingi apendavyo. Ataimiliki tovuti na kuiendesha
yeye.
Kumbuka kwa awamu hii ya kwanza TUNATOA BURE TOVUTI 100 TU kisha awamu ya
pili tutatangaza tena. Hebu fikiria kwa mkupuo tukipata tovuti 100 kwa
maana ya kwamba tunakuwa na kurasa mia moja zinazoelezea
watu/kampuni/vikundi mbalimbali na shughuli zao hapa Tanzania, hii ni
hatua kubwa sana na inaongeza maingizo ya utafutaji wa vitu toka Tanzania
katika search engines na tunasogea mbele taratiibu.
Hakuna vigezo vya kupata huduma hii ya bure, na tutahudumia kwa mujibu wa
FIFO (first in first serve/out) wa kwanza kuja, wakwanza
kutoka/kuhudumiwa. Maelezo na ufafanuzi zaidi tafadhali tembelea hapa
ujisomee huduma hii kwa undani. Zipo pia huduma
na bidhaa mbalimbali kwa walio na tovuti tayari"

Haya wahi nafasi yako mapema...

Maoni

  1. Japo nadhani sasa kila mtu anaweza kujitengenezea tovuti yake mwenyewe hii ni hatua nzuri kwani tunahitaji sana nasi kuonekana katika dunia ya mtandao. Naunga mkono na endeleeni kutoa hivi ofa mara kwa mara!

    JibuFuta
  2. wazungu nao wakati fulani huwa wana akili. waliwahi kusema-ga "there is no free lunch". nadhani hii inakuja kwa taswira kama hii ya free lunch halafu jioni you buy two or three dinners.

    Kivipi? Leo unapewa free website. unaitumia. inakutangaza. inakulipa pasi na wewe kuilipa. unaona tofauti ya mapato ya biashara na kadhalika. unaneemeka. halafu wanakuma kina mr free wanakwambia sasa uanza kuchangia "kidogokidogo" utafanya nini? utawaambia wachukue ki-website chao? sidhani.

    tuambiane tu ukweli hii ni janja ya nyani, hapana janja ya biashara. ila umuhimu wa kuwa na website uko pale pala.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu