Yapo mambo mengi katika jamii zetu yaliyofanyika zamani ambayo tukiyatazama twaweza kujifunza mengi. Mengi ya hayo, si sehemu ya jamii za kisasa hivi leo, lakini yalekuwa na msaada wa namna Fulani kwa jamii. Katika jamii ya asili ya wanyaturu, kabila dogo linalopatika katika wilaya ya Singida (na kidogo manyoni), mahusiano kati ya baba na mama yalikuwa na sura tofauti sana na ilivyo leo. Wakati leo hii, wazazi kulala vyumba tofauti huchukuliwa kama ishara ya kufifia kwa mahusiano baina ya wawili hao, kwa Wanyaturu hiyo ilikuwa na maana tofauti. Kikawaida, wazazi wa Kinyaturu hawakupaswa kukaa nyumba moja (sio chumba kimoja, nyumba moja) ndani ya boma. Katika boma analojenga mwanaume kama himaya ya familia yake, alipaswa kuzingatia uwepo wa nyumba mbili ndnai ya boma moja. Baba ambaye ndiye mkuu wa boma, alilala na wanawe wa kiume katika sehemu maalumu ya nyumba inayojulikana kama "Idemu/Ikumbu". Nyumba hiyo ilijitenga pembeni na nyumba kuu alikoishi mama na wanawe wa...
Ni kweli mwaka huu uanakimbia sana na watu tunazidi kuzeeka. Ni furaha kusikia u mzima ni wapi uhuki ulako asali na maziwa....LOL
JibuFutaNashukuru u buheri wa Afya, nami pia afya najivunia.
JibuFutaKila mmoja anaweza kutafsiri mda unavyokwenda kulingana na mazingira aliyopo, nchi ya ahadi lazima siku zikimbie tu! tena siku inapokwisha unakasirika,asali na maziwa yake! wacha we!
Nchi ya kusadikika, daaaa! Siku kama mwezi vile.
muda bwana! ikiwa unasubiri jambo jema unaenda taratibu, ukiwa haujafaniskisha ama haujakamilisha jambo fulani unaenda kwa kasi mno.
JibuFutainaonyesha orodha ya mambo yako bando ndefu ndio maana muda unakuendea haraka.lakini hapana shaka kwa kuwa huko ulikokuwa kuna asali na maziwa basi nadhani mambo siyo mabaya.
karibu tena.
Mwaipopo umenipa tafsiri nzuri ya muda.
JibuFutaKissima, nchi ya kusadikika si halisi. Hii nilimo i halisi na kweli. Inamiminika asali. Mwezi wa asali ulikuwa...
Mwaipopo - inaonekana kama vile ndiyo umemaliza kumsoma Albert Einstein.
JibuFutaBwaya - hiyo nchi inayobubujika maziwa na asali iko wapi tuhamie? Ni ile nchi ya ari mpya, kasi ....na...?
Profesa Masangu, Mwaipopo ni mzee wa nukuzi.
JibuFutaNadhani unaweza kuwa umekosea. Hiyo kasi mpya na ari yake sikujua(ga) kuwa ni kula rasilimali za nchi kwa nguvu mpya.
Nikuja jua, nchi kama nchi ina maziwa tele yanayonywewa na wenyewe hata kama yako kwako mlangoni. Muhimu ni kujinywesha mwenyewe kila unapopata nafasi. Ukisubiri unyweshwe sahau! Wnakimbia na ng'ombe kabisaaa.... Ha ha haaa!