Naomba msaada wa lugha

Blogu zetu zinatusaidia kukuza lugha yetu ya kiswahili.

Lazima tuwe wazi kuwa mara nyingine tunalazimika kutumia sentensi nzima kufafanua neno moja.

Hapa nina maneno kadhaa ninayohitaji kiswahili chake.

Conscious, sub-conscious, compulsion na obsession.

Naomba mwenye msaada wa karibu anisaidie kupata maneno fasaha ya kiswahili.


Natanguliza shukrani.

Maoni

  1. Nitajaribu kadiri ambavyo ningetafsiri mimi:

    Concious = -a kujitambua, jifahamu (hali ya kuwa na fahamu)

    Sub-Concious = maluweluwe (hali ya kuwa nusu hai katika fahamu au kiutambuzi katika mfumo wa fahamu). Angalabu wengine waweza sema 'nusu kaputi'.

    Compulsion = shurti, sharti, shuruti, kuwiwa kufanya/kutenda jambo fulani kwa msukumo wa ndani.

    Obsession = zuzuka (kutoka neno 'zuzu') limbukeni, utumwa (unaotokana hasa na nguvu ya msukumo wa fikara/imani zilizoshika mizizi katika kiakili)

    Karibu tena na kwaheri kwa sasa.

    JibuFuta
  2. Dada Subi asante sana.

    Nyongeza:
    Ili kupata msamiati uliokamilika, labda nibadili yale mawili ya mwanzo yawe nomino;

    consciousness na sub-consciousness. Hebu niwekee sawa hapo.

    JibuFuta
  3. subconsciousness mind = mawazo ya kina!

    JibuFuta
  4. Nashukuru da Subi kwa kunisaidia nami pia.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia