Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2009

Dunia mbili katika nchi moja?

Nilikuwa nikifuatilia namna watuhumiwa 'wetu' wasiohesabika wanavyopata dhamana. Kweli nchi hii ina mambo. Wakati kila mtuhumiwa anaweza kutoa hati ya nyumba (soma hekalu) lenye kukaribia shilingi za kitanzania bilioni moja, asilimia kubwa ya watanzania waliobaki hawana hata uwezo wa kupata milo miwili iliyotimia kwa siku. Wakati kuna wenzetu wachache (hata kama hawana hatia) wanaouwezo wa kujiwekea dhamana ya mabilioni ya shilingi, idadi kubwa ya watanzania waliobaki hawana hata ndoto ya kujenga pango lenye chumba kimoja. Hali hii inatupeleka wapi watanzania? Dunia mbili katika nchi moja? Kwamba katikati ya umasikini huu, wapo wenzetu wachache wanaoogolea ukwasi wa kutisha? Mabilionea hawa wana raha ipi ikiwa wamezungukwa na mafukara pande zote? Tafakari.

TAKE THE RISK - Kitabu kipya

Picha
Kitabu kipya cha Dr. Benjamin Carson. Kitafute ukisome.

Kuwa mwaminifu na mkweli - Dr. Benjamin Carson

Picha
Daktari Ben Carson ni kati ya watu ambao walinisisimua tangu nikiwa kinda. Nimesoma vitabu vyake Gifted Hands, Think Big na the Big Picture. Katika mambo muhimu ambayo huwa nayakumbuka kupitia vitabu vyake ni suala la uaminifu. Kwamba ni muhimu kusema ukweli. Ukisema ukweli hautalazimika kukumbuka ulichosema kabla! Ukweli hata katika mambo madogo kama wakati unapoulizwa ulipo kwenye simu. Uaminifu unalipa. Na kweli nimethibitisha kuwa uaminifu unalipa. Kama unapenda kusoma vitabu hivyo, jaribu kwenye maduka ya vitabu katika mji uliko. DSM - Christian Bookshop, Mtaa wa Mkwepu makabala na Billicanas, au Mlimani city, Barabara ya Sam Nujoma. Arusha- Book Point, Kimahama ama Kase Store. Bonyeza hapa kupata picha ya falsafa yake.

Fikra zimepitwa na wakati?

Picha
Jenerali Ulimwengu ameandika kuzungumzia dhana ya obsikuranti, yaani "... mtu yule anayeshikilia anachodhani kwamba anakijua na akaking’ang’ania kwa nguvu zake zote, na akawa tayari hata kwenda vitani kutetea ‘ujuzi’ wake huo. Ni mtu anayeamini mambo ambayo yanaweza kuwa yamepitwa na wakati, na maarifa ya kuonyesha hivyo yanapatikana, lakini hataki hata kusikia wala kuona jambo lo lote linaloweza kuyumbisha au kuteteresha ujinga wake..." Anasema "...tumezaliwa katika jamii zenye imani kadhaa zilizoandamana na maelekezo pamoja na makatazo kem kem. Tumejamiishwa (socialised) katika imani, sheria, kanuni na taratibu hizo, kimsingi bila kuwa na fursa ya kuhoji ulazima wa kufanya hivyo. Kwa jinsi hii, hata yale maelekezo yaliyo na faida, au makatazo yenye manufaa, tunayafuata na kuyatii bila kujua ni kwa nini tunafanya hivyo. Jamii nyingi za Kiafrika haziruhusu watoto waulize maswali mengi, hasa kama maswali hayo yana mwelekeo wa kusaili misingi ya imani zilizozoeleka. M...

Saa nyingine usipende kuamini unachokiona

Umewahi kumwona kunguni anavyokimbia? Sasa ndugu msomaji huwezi amini spidi yote ya kunguni kumbe anakokwenda ni nyuma ya godoro!? Usipende kuamini unachokiona. Hoji. Tafakari. Utaona kisichoonekana katikati ya mistari.

Urafiki unawezekana bila ngono?

Habari za siku mbili tatu ndugu msomaji. Nafurahi kwamba umeendelea kuwa mtembeleaji wangu kwa kipindi chote nilipokuwa mwituni. Nimerudi na vijiswali hivi vidogo kuhusu suala la urafiki na ngono. Naomba kuyaweka mezani: Je, rafiki ni nani? Ili mtu awe rafiki yako mambo gani ni ya msingi kutimia? Je, rafiki wa jinsia iliyop tofauti na yako ana tofauti gani na rafiki wa jinsia yako? Je, kuna uwezekano wowote wa kuwa na urafiki na mtu wa jinsia nyingine bila ngono? Je, urafiki upi unauwezekano wa kudumu zaidi, ule wenye kuhusisha ngono ama ule usio wa kingono? Kwa nini? Na je, inawezekana kufanya uamuzi wa kuishi bila ngono kabla ya ndoa?

Huu si udhaifu wa kiume?

WANAUME wengi wanapenda kuoa wanawake wanaowazidi sana umri. Ni nadra kukutana na mwanaume aliyezidiwa umri na mke wake. Kama hiyo haitoshi, wanaume wengi wanapenda kuoa wanawake wenye elimu ndogo zaidi yao. Ushahidi ni wewe unayesoma hapa. Ha ha haaha! Vilevile, wanaume wengi wanapenda kama ingewezekana, basi wapate wanawake watakaowategemea wao kiuchumi. Au wawe na ujira mdogo kuwazidi wao. Ni mara chache sana imekuwa kinyume. Swali: Je, hizi si dalili za kutokujiamini? Je, huu si ushahidi kwamba wanaume ni dhaifu, ndio maana wanatafuta mbinu za kujihami?

Kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu?

Napenda kutazama kipindi cha Longa Mwanamume kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV kila Jumatano saa tatu usiku. Mzee Barnabas Maro anakiweza. Pamoja na kwamba mara nyingi wanaume wamekitumia kipindi hicho kuonesha mabavu yao kwenye mahusiano, lakini si kipindi kinachofanana na mavipindi mengine ya nchi za nje yasiyohusiana na utamaduni wetu. Longa Mwanamume ni kipindi kizuri. Jana ulikuwepo mjadala wa ndoa. Swali lilikuwa: Kwa nini ndoa za siku hizi hazidumu? Nilifurahia majadala huo. Wazungumzaji walitaja sababu nyingi ambazo ni za kweli. Nami kama ningeweza kuchangia, ningesema ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu vijana huanza kujuana kimwili kabla ya ndoa. Na kufanya hivyo hujenga tabia ya kutokuaminiana na mwisho wake ni kuvunjika kwa ndoa. Wewe ungesemaje?

Haki ni nini?

SIKU hizi haipiti dakika hujasikia haki zikidaiwa mahali. Kuna haki za watoto. Haki za akina mama. Haki za wafanyakazi wa ndani(Koero analizungumzia hili vizuri). Haki za masikini. Haki za vyangudoa. Haki za maalbino. Haki za wasomaji. Haki za mafisadi (hata fisadi naye ana haki ya kusikilizwa/natural justice). Haki. Haki. Haki. Orodha ni ndefu. Jambo moja. Inapodaiwa haki, ikumbukwe kuwa upo upande ambao utalazimika kunyang'anywa haki zake ili haki ile ya kwanza inayodaiwa ipatikane. Kwa maneno mengine, unajikuta ili kutetea haki, inabidi unyang'anye haki. Na upande huu wa pili unaolazimika kupoteza haki ili kufidia haki inayodaiwa, nao ukiamka, inabidi zoezi liwe mduara. Yaani poteza haki, kuleta haki. Kwa mfano. Mtoto anapodai haki, maana yake inamlazimu mzazi kupoteza haki zake ili kumpatia mwanae haki. Kwa maneno mengine, haki ya mtoto inakuwa utumwa kwa mzazi. Unapoteza haki kuleta haki. Mwanafunzi wa kike anapodai haki ya kusoma kwa upendeleo, inabidi mamlaka zinaz...