Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

Mbinu Nne za Kugundua na Kukuza Kazi ya Wito Wako

Picha
Umewahi kujisikia unafanya kazi isiyokupa utoshelevu? Unaweza kuwa na kiwango kikubwa cha elimu, kazi nzuri yenye heshima na mshahara mkubwa lakini unajikuta hufurahii kile unachokifanya. Ingawa moja ya sababu inaweza kuwa uongozi na mazingira mabaya ya kazi, hata hivyo, mara nyingi, tatizo huanzia ndani yetu  –k ufanya kazi isiyoakisi wito wetu. Mifumo ya elimu hulenga kutuandaa kukidhi mahitaji ya nje matarajio ya jamii, soko la ajira na mengine yanayofanana na hayo –matokeo yake mifumo hiyo inatuchonga kuwa watu tusiokidhi miito tuliyozaliwa nazo. Robert Green, mwandishi wa vitabu maarufu vya “Mastery” na “The 48  Laws of Power” anasema elimu ina nafasi kubwa ya kutupoteza. Kadri tunavyoelimishwa na watu waliotuzunguka ndivyo tunavyojikuta “tumekuwa wageni wa nafsi zetu wenyewe.” Maoni ya wazazi, walimu, marafiki, matarajio ya jamii, mara nyingi, yanatupeleka mbali na wito.  Kwa hiyo, badala ya kuheshimu kile ninachokiita wito, tumefungwa...

Unataka Kumjua Rafiki Atakayekusaliti? Soma hapa

Picha
PICHA: Recycle Coach Katika nyakati kama hizi za Pasaka, mara nyingi, tunasikia marehemu Yuda Iskariote akijadiliwa kama jitu ovu lisilo na maadili lililokuwa tayari kumsaliti Bwana wetu Yesu Kristo. Binafsi naamini, pamoja na ubaya wake, usaliti wa Yuda ulikuwa muhimu katika kuwezesha mpango wa Mungu kwa wokovu wetu. Wakati mwingine Mungu hutumia mabaya kuwezesha mazuri. Hata hivyo, kwa maoni yangu, Yuda hakuwa na nia mbaya kivile. Kwanza, alikaa na Yesu kwa muda wa kutosha na hivyo alifahamu Yesu hakuwa mtu wa hivi hivi anayeweza kuchezewa kienyeji. Yesu alifanya miujiza mingi na Yuda alishuhudia. Yesu alitembea juu ya maji. Yesu alifufua wafu. Si mara moja. Tena kuna wakati Yesu alimfufua mtu aliyekuwa kazikwa siku tatu. Unamkumbuka Lazaro. Aidha, kuna nyakati washikadini na wanafiki walitaka kumshughulikia Yesu, wakashindwa kwa sababu Yesu aliwaponyoka. Yuda aliyafahamu yote haya. Kama baadhi yetu tunavyofanya leo, Yuda aliutazama uwezo huu wa Yesu k...

Kuuishi Wito Wako, Unahitaji Nidhamu ya Kujifunza

Picha
PICHA: findingmastery.net/ Nimekutana na vijana wengi wanaotaka niwaonyeshe njia ya mkato ya kufanya kazi za ndoto zao. Wanafikiri kupata kazi inayoendana na vipaji na tabia zao ni jambo la siku moja. Ingawa huwa ninawasaidia kujiuliza maswali ya msingi yanayowachochea kugundua hazina iliyolala ndani yao, bado husisitiza umuhimu wa kuwa na mtazamo mrefu wa kuona yasiyoonekana kwa macho. Nitatumia mfano wa Robert Green, mwandishi nimpendaye aliyeandika vitabu maarufu vya ‘The 48 Laws of Power, ‘Mastery’ na ‘The Art of Seduction.’ Ingawa tangu akiwa mdogo aligundua alitaka kuwa mwandishi, Robert hakuwa na uhakika anataka kuandika masuala gani.   Baada ya kumaliza chuo, Robert alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Kazi hiyo, hata hivyo, haikumwendea vizuri. Mhariri wake alimshauri, ‘Tafuta kazi nyingine ya kufanya. Wewe si mwandishi. Hujui kupangilia mawazo yakaeleweka. Nakushauri ukatafute maisha mengine.” Robert anasema alijisikia vibaya kwa ...

Lugha ya Ubabe Hupunguza Ushawishi Wako

Picha
Niliwahi kusoma barua ya mfanyakazi mmoja kwa bosi wake. Ingawa alikuwa na madai ya msingi aliyoyaelekeza kwa mkuu wake huyo wa kazi, kwa maoni yangu, alikuwa ametumia lugha isiyo na staha. Kwa kufikiri kuwa maneno aliyokuwa ameyatumia yangepunguza ushawishi wake, nilimshauri angebadili lugha kuifanya iwe rafiki zaidi. Hata hivyo, hakukubaliana na maoni yangu. Miezi michache baadae, barua ile ilimgharimu kazi. Wengi wetu huchukulia kirahisi suala la lugha. Tunafikiri kwa sababu tunazo hoja na tunafahamu kile tunachokitetea ndio ukweli wenyewe, basi tuna hiyari ya kutumia lugha yoyote. Hatujali kuchagua maneno ya kusema. Tunasahau kuwa maneno yetu yana athari kubwa katika mawasiliano kama ilivyotokea kwa mfanyakazi yule. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa lugha, mbali na ujumbe, hubeba hisia. Kuna maneno ukimwambia mtu hata kama una hoja hatakuelewa. Nakumbuka siku moja nilimsikia mkubwa wa ofisi mmoja akitoa maelekezo kwa watu waliokuwa chini yake. Nilishangaa. Mkubwa...

Malengo Yanavyoweza Kubadili Tabia ya Mtoto

Picha
Mwanangu wa miaka saba alikuwa na tatizo la kupenda sana kununua vitu vitamu. Kila siku alikuwa ombaomba wa chochote kinachomtosha kwenda dukani. Sikupenda tabia hii. Mbali na kuharibu meno yake, kulikuwa na tatizo la kutokujizuia. Ilifika mahali tunagombana kwa sababu tu hajapata chochote kukidhi hamu yake ya kununua ‘ice cream’, ‘chocolate’ na vinavyofanana na hivyo. Jitihada za kubadili tabia hii ya kupenda vitu visivyo na faida kwake hazikuzaa matunda.

Tunatofautiana sana...

Picha
PICHA: Verastic Mwanamke, kwa asili yake, anajisikia vizuri kusema matatizo yake kwa mtu wake wa karibu anayemwamini –kama, mathalani, mume wake. Ile tu kujua kuna mwanaume yuko tayari kusikia yanayousibu moyo wake kunamfanya ajisikie salama.

Hatua Tano za Kuandaa Wasifu Utakaokupa Ajira

Picha
Moja wapo ya sababu zinazochangia watu kukosa ajira wanazoomba ni uwezo mdogo wa kujenga wasifu wao katika maandishi.   Wasifu ni maelezo binafsi yanayolenga kumshawishi afisa mwajiri kuwa unazo sifa za kutosha kupata ajira unayoomba. Vyuo vyetu, kwa bahati mbaya, haviweki msisitizo katika ‘mambo madogo’ kama haya. Matokeo yake watu wengi wazuri wenye ujuzi wanashindwa kuonekana kwa waajiri.

Ukitaka Kujifunza Waruhusu Watu Waone Usichokiona

Picha
UKIFUATILIA mazungumzo ya wa-Tanzania wengi kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kuona namna watu wanavyojinasibu kujua. Mijadala mingi imejaa ‘ujuaji’ unaofanya watu wajigambe, wadhihaki wengine, watukane na wakati mwingine, kadri ya mamlaka yao, watake kulazimisha kile wanachokiona wao ndio kiwe ukweli usiopingika.  Katika makala haya, ninajaribu kuonesha kuwa ili tujenge jamii ya watu wastaabu wanaoheshimiana lazima tuwe tayari kujifunza hata katika mazingira ambayo tunaamini tunajua.

Tumia Mitandao ya Kijamii Kuboresha Utendaji wa Taasisi, Kampuni Yako

Picha
PICHA: kairalinewsonline.com Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufikia Novemba 2017, Tanzania ilikuwa na jumla ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wapatao 22,995,109.   Moja wapo ya kichocheo kikubwa cha matumizi haya makubwa ya mtandao ni ongezeko la watu wanaotumia simu za viganjani zinazowezesha kuunganishwa na mtandao bila kulazimika kuwa na kompyuta zenye gharama kubwa. Hivi sasa, kwa mfano, takribani   line za simu za kiganjani zinazotumika zinafikia 40,080,954. Uzoefu unaonyesha kuwa wengi wa watumiaji wa mtandao wa intaneti wanatumia zaidi mitandao kama vile WhatsApp, Facebook, Twitter, Instagram na YouTube. Nguvu ya mitandao ya kijamii Nguvu ya mitandao ya kijamii, kwa kiasi kikubwa, inategemea tabia ya watumiaji wake. Inakadiriwa kuwa mtumiaji mzuri wa mitandao hii, huchungulia kinachoendelea mtandaoni zaidi ya mara 20 kwa siku. Makampuni makubwa ya habari kama Mwananchi Communications yanaonekana kuelewa fursa hii...

Mambo Sita Mwanao Anayohitaji Kuyasikia

Picha
PICHA: houstonpress.com Watoto wadogo ni watu kamili wenye hisia kama sisi watu wazima. Hata kama wakati mwingine hawawezi kusema wazi wazi, ukweli ni kwamba akili zao ni kama dodoki linalonyonya kimya kimya yale wanayoona tukiyasema na kuyatenda. Unaweza, kwa mfano, kusema jambo dogo kwa mtoto tena bila kumaanisha lakini jambo hilo likawa sumu itakayoharibu kabisa maisha ya mwanao. Unaweza kuwa na nia njema ya kumlazimisha kufanya kitu fulani sahihi kabisa, lakini kwa sababu hujaweza kuelewa na kujali hisia zake, jambo hilo likakosa nafasi kwenye moyo wa mtoto. 

Zijue Ishara Tano Kuwa Mwajiri Amekuchoka

Picha
UMEWAHI kuhisi huhitajiki kazini? Umewahi kuona dalili kwamba pengine ni muda muafaka kwako kuchukua hatua kabla mambo hayajaharibika? Mwandishi Speancer Johnson aliyeandika kitabu maarufu cha ‘ Who Moved My Cheese ” anasema ni muhimu kusoma alama za nyakati katika maeneo ya kazi. Unapofanya kazi bila kuelewa ishara za awali mambo yanapoanza kwenda mrama, unajiweka kwenye hatari ya kujikuta kwenye mazingira ya kufanya maamuzi kwa kuchelewa. Wafanyakazi wengi huamini mwajiri akiwachoka atawaandikia barua ya kuwafuta kazi. Hawajisumbui kujua kusoma ishara mbaya kwa kuamini mwajiri hawezi kuwachoka na akabaki kimya. Unaweza kujiuliza, kama kampuni haikuhitaji kwa nini hawakuambii? Ukweli ni kwamba, wakati mwingine mwajiri huona ni afadhali akuwekee mazingira ya wewe kuondoka mwenyewe kuliko kukuondoa. Mwajiri anapokuondoa anajiweka kwenye mazingira yanayoweza kumletea usumbufu wa kisheria na wakati mwingine wafanyakazi wanaobaki hupatwa na tahayaruki. Ili kuepuka k...