Unadhani macho yako yanaaminika?

Nianze kwa kuomba msamaha. Sijakuwepo mtandaoni kwa siku kadhaa. Nikuombeni kutokukata tamaa ya matembezi kibarazani hapa.

Leo ningependa tuangalie suala moja. Kwamba mara nyingi tunavyoyaona mambo sivyo yalivyo. Milango ya fahamu zetu haiaminiki. Hebu tazama picha hii hapa chini. Angalia kwa makini kiboksi A na kiboksi B uone unavyodanganywa na macho.
Angalia viboksi hivi. Hakuna rangi yoyote kati ya kiboksi kimoja na kingine, japo macho yako yanakuambia kuna rangi ya kijivu.Bonyeza na hapa uone picha hii. Unajifunza nini?

Ukweli na uhalisia ni vitu viwili tofauti.

Maoni

 1. Habari za siku kaka,

  Ahsante kwa habari hii ya macho, nimejifunza.
  Vipi mbona ulikuwa kimya kwa kitambo namna hiyo?
  Nimekuwa nikipita hapa kibarazani kwako mara kwa mara lakini sikubahatika kuona jambo lolote jipya!
  Nimefurahi umerejea tena.

  Ni mimi mzee wa utambuzi

  Shabani Kaluse

  JibuFuta
 2. Kaluse,

  Ningependa sana kuwa mtandaoni kwa kadiri iwezekanavyo. Na ndivyo ilivyo. Hata hivyo, hutokea mara nyingine majukumu mengine yananinyima uhuru huo. Nitajitahidi kuwapo iwezekanavyo.

  Tuko pamoja, asante kwa kunitembelea.

  JibuFuta
 3. @Bwaya : Ukipata nafasi tafuta hii kwenye YOUTUBE: Dan Dennett: Can we know our own minds?

  JibuFuta
 4. @ Simon,

  Nitajaribu nione. Bila shaka kuna elimu unanielekezea. Kizuri ule na mwenzio au sio. Asante kaka.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu