Mchango wa msomaji

Jana kuna mchango wa mawazo niliupata kutoka kwa msomaji Prosper Mwakitalima. Huyu ni mwanafalsafa na rafiki yangu wa siku nyingi.

Mjadala wetu ulikuwa katika hoja ya nguvu kuu iliyozungumziwa na Kamala.

Anasema:

"...Kwamba tunapofikia kuamini kuwa ipo nguvu kuu kwa sababu ya kushindwa kuamini kuwa viumbe vyote na asili yake visingeweza kujiratibu vyenyewe, na hapo hapo tukakubali kuwa nguvu hiyo haina chanzo, na mwisho wake hauelezeki, tunashindwa vipi kuamini kuwa hata viumbe navyo vimekuwapo vyenyewe bila nguvu fulani kuu zaidi? Kwa sababu kama tunaamini kuwa hiyo nguvu haina chanzo, kwa nini tushindwe kukubaliana kuwa hata viumbe navyo vyaweza kuwapo bila chanzo?..."

Hiyo ni changamoto nyingine inayohitaji majibu. Najua anachokoza mawazo kwa lengo la kutufikirisha zaidi. Nimetangulia kukujulisheni kuwa yeye ni mwanafalsafa mwenye dini.

Maoni

  1. Changamoto aliyoitoa bwana gwamaka ni nzuri sana.Kwa ninavyoafahamu mimi ili kiumbe kiwepo lazima kuwe na chanzo fulani ambacho ni nguvu.Kwa mfano kuwepo kwa binadamu ni muhimu kuwepo kwa mbegu za kiume na kike ndiyo binadamu anaumbika tumboni mwa mama yake lakini haina maana kuwa ndiyo chanzo chake hizo mbegu kwa maana kabla hazijawa mbegu zilikuwa ni kitu kingine na vivyo hivyo kabla halijawa yai lilikuwa ni kitu kingine na baadaye ndipo zikabadili mfumo wake na kuwa mbegu au yai na kisha binadamu na huyo binadamu akifa hubadika na kuwa kitu kingine tena.Na ndiyo maana tunaambiwa baada ya kifo tunaenda kuishi maisha ya milele yasiyo na mwisho.kwa hiyo kama kuna maisha yasiyo na mwisho basi hata sisi hatuna chanzo tulikuwepo.Huo ni mtazamo wangu.

    JibuFuta
  2. safi nuru, mtizamo wako umetulia lakini kwa kuongeza nadhani tangu hapa tulipo au kabla ya kuwepo, tayari tulisahaanza maisha yasiyo kuwa na mwisho isipokuwa miili yetu hii inamwanzo na mwisho.

    mimi nadhani nguvu hii ipo. kama nilivyotoa mfano wa umeme wa mtera au kidatu ndivyo nguvu hiyo inavyoweza kufananishwa.

    kwa wale wanaofanya meditation, wanaweza kusema ni vitu gani huhisi au hali gani wanapitia wakati wa meditation.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?